kwenye interview panel huwa wanaangalia kitu gani?

kyagata

JF-Expert Member
Oct 18, 2016
6,338
12,371
samahani kama nitakua nimekosea jukwaa jamani.
hivi panelists huwa wanaangalia nini hasa ili waweze kumpa mtu kazi?nauliza hivi kwa sababu nimehudhuria interview nyingi na unakuta tumepambana kuanzia mchujo wa kuandika na mpaka tunabaki labda watatu kwenye final stage ila kazi nakua sipati na nikiangalia anaekua amepata kazi anakua ni mtu wa kawaida tu yaani hana chochote cha ziada kunizidi.
Jamani sasa hawa watu huwa wanataka mtu ujibuje yale maswali yao au huwa wanataka nini zaidi?
 
Unajuaje? au mwenzetu unapaniaga na kuvunja kabatiiii basi unajiona uko zaidi ya wengine? Kama amepata we umekosa jua anakuzidi.
 
Inabidi utafute dawa ya mvuto tu maana hakuna namna tena. . . . . . . . . .
 
samahani kama nitakua nimekosea jukwaa jamani.
hivi panelists huwa wanaangalia nini hasa ili waweze kumpa mtu kazi?nauliza hivi kwa sababu nimehudhuria interview nyingi na unakuta tumepambana kuanzia mchujo wa kuandika na mpaka tunabaki labda watatu kwenye final stage ila kazi nakua sipati na nikiangalia anaekua amepata kazi anakua ni mtu wa kawaida tu yaani hana chochote cha ziada kunizidi.
Jamani sasa hawa watu huwa wanataka mtu ujibuje yale maswali yao au huwa wanataka nini zaidi?

Unakosea sana kwa kusema unakuta mtu yupo hivi au vile.

Ni muhimu kuomba ripoti ya matokeo yako ya intavyuu ili ujiongeze. Hakuna lingine, utajiuliza kila mara na labda unakuwa haujui ya kusema unapotakiwa. Kubali hauna ujuzi wa kazi na mengineyo sasa yajue

Jibadilishe usidharau watu, wewe ndio bado unashindwa mwenyewe kwa kutoweza. Kubali jiongeze fatilia
 
asa mtu kama hana ujuzi wa kazi,kwa nin wamsumbue kumuita kwenye interview tena wanaenda nae mpaka stage ya mwisho kama alvyosema mleta uzi hapo juu?
 
Kiongozi jua tu kwamba muda wako wa kupata kazi unakua bado maana binafsi nilikua najiuliza sana lakini mara nyingi ukitoka kwenye final interview kuna kuaga na. doubts tu kwamba pale naweza kupata au naweza nisipate ila sehemu zingine hua ni waswahili wanakua washapanga wanafanya formality...we chukulia nafasi yako bado ikifika itakua tayari....
 
asa mtu kama hana ujuzi wa kazi,kwa nin wamsumbue kumuita kwenye interview tena wanaenda nae mpaka stage ya mwisho kama alvyosema mleta uzi hapo juu?

Unapotuma maombi unakuwa unajiona unalo, ila tatizo kwa wengi ni katika kujieleza. Hata mtu mwenye top marks za shahada anaweza akawa bomu kwenye interview n.k.

Ndio maana kwa mtu ukiona kila wakati unashindwa ni muhimu kuuliza uambiwe wapi ilikuwaje ujue unapojiangusha.

Hii haitaki ubishi kama unajipenda.

Unaweza kukuta kuna vipengele labda vitano, kimoja haswa ndio tabu. Au hata nisrme kimoja au viwili kila wakati wewe unasaka kazi sawa... Bila kujua unamapungufu hapo unaona itakuwaje? Mie jibu ni utaendelea kutopasi tu.
 
Pia kabla hujaingia kwenye chumba cha interview hakikisha Cv yako unaifahamu vizuri sana.Hata job descrption za hiyo kazi hakikisha unazijua na unaweza kuzilink na skills au experience zako.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom