Kwenye historia ya nchi yetu kuna mbunge amewahi peleka muswada na ukawa Sheria? Mwananchi wa kawaida anaweza andaa muswada akapeleka Bungeni?

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,889
Bunge ndiyo linatunga sheria lakini mimi nimeona sehemu kubwa miswada huwa inatoka wizarani au kwenye taasisi za serikali. Sijawahi sikia mbunge ametoa mswada na baadaye umekuwa sheria.

Imewahi tokea kwenye historia yetu mbunge katoa mswada na umekuwa sheria? Wenzetu unakuta hata hiyo sheria inaitwa kwa jina la mbunge huyo.

Halafu mwananchi kama siridhiki na jambo fulani nataka itungwe sheria ya kulihusu naweza peleka mswada bungeni? Kuna utaratibu labda wa kukusanya sign kadhaa na Ikifika unaweza peleka mswada?
 
Mwanzoni hata mimi niliamini kuwa bunge ndio linatunga sheria. Baada ya kufuatilia nikajua bunge ni rubber stamp tu ya serikali, kwani sheria zote hutungwa na serikali, na hapo bungeni inapalekwa ili kuhalalisha wabunge kuchukua posho, lakini hawabadili chochote, tena hili bunge kibogoyo la sasa ndio bure kabisa. Kwa maneno marahisi hilo bunge ni kijiwe cha kulia pesa za wananchi kisheria.
 
Kwahiyo mkuu unataka kuniambia sheria haziruhusu mbunge kuja na mswada wa sheria bungeni? Mbona ni hatari hii!
 
Mbunge hawezi kupeleka Muswada,sheria za bunge letu hazina fursa hiyo!Sana sana anaweza kutoa hoja binafsi au kwenye kamati za bunge kupendekeza mabadiliko ya sheria au kupendekeza kutungwa kwa sheria mpya!
Mbona imekaa vibaya hii au ndiyo utaratibu wa mabunge?
 
Kwahiyo mkuu unataka kuniambia sheria haziruhusu mbunge kuja na mswada wa sheria bungeni? Mbona ni hatari hii!

Ipo kinadharia zaidi, na kama ukifanikiwa ujue ina mkono wa kiongozi wa serikali. Mwenye maamuzi na hilo bunge sio spika wala nini, bali ni mwenyekiti wa bunge ambaye ni mwakilishi wa rais. Mwenyekiti wa bunge ndio muamuzi ni hoja ipi ijadiliwe bungeni.
 
Nimekumbuka hoja ya Tanganyika ya Marehemu Njelu Kasaka na G55 mwaka 1993! Walikomaa mpaka ikapita bungeni.

Mwalimu Nyerere baada ya kushindwa kuwashawishi waitoe Bungeni aliandika kitabu cha Uongozi Wetu na Hatma ya Tanzania! Akawasulubu Malecela na Kolimba kwa kumyumbisha Rais Mwinyi na utekelezaji wa maamuzi ya Bunge ukaishia hapo.
Mbunge hawezi kupeleka Muswada,sheria za bunge letu hazina fursa hiyo!Sana sana anaweza kutoa hoja binafsi au kwenye kamati za bunge kupendekeza mabadiliko ya sheria au kupendekeza kutungwa kwa sheria mpya!
 
Kanunu za kumudu za bunge yaani standing order zinaruhusu mswaada binafsi
Mnyika aliwahi kupeleka muswada binafsi lakini haukuingizwa bungeni. **** utaratibu mgumu sana kwa mbunge lakini unaoipa serikali uhuru wa kuamua muswada upi uingie bungeni
 
Kwa hyo kazi ya bunge kutunga sheria nayo imeshindikana? Maana kuisimamia serikali ilishindikana zaman kidogo
 
Kwa hyo kazi ya bunge kutunga sheria nayo imeshindikana? Maana kuisimamia serikali ilishindikana zaman kidogo
Bunge la Tanzania haijawahi kutunga sheria bali kupitisha sheria. Sheria zote za nchi hii hutungwa/drafted na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
 
Subiri mswada wa kumuongezea JPM miaka ya uongozi utaona utakavyopelekwa na wabunge.
 
Back
Top Bottom