Kwenye hili sitaki nifeli, naombeni ushauri wenu waungwana

kikoozi

JF-Expert Member
Jun 24, 2015
2,030
2,926
Nimemaliza chuo muda (2016) kidogo, nimesota sana kupata ajira, nimesota sana mpaka nilifikia kukata tamaa ya maisha, Mungu mkubwa mwaka jana mwezi wa 5 nikaja kupata kazi kwenye mradi mmoja hivi, kutokana na mapito ya kukosa kazi na kuangaika mtaani, nilijichanga mnooo mnoo nilijichanga kupita maelezo na sikutaka kupoteza hata sent tano kijinga.

Mwishoni nimefikisha kiasi cha sh Milion 10 cash.

Sina uzoefu na biashara kiukweli kabisa

Nina kiwanja kipo Dar (kama asset yangu nilikinunua nikiwa chuo kwa bumu), natamani sana nijenge (napenda sana sana nyumba)

Naombeni ushauri wenu; ni biashara gani nikifanya kwa siku naweza kulaza sh elfu 50 kama faida kupitia hiyo pesa milion 10 (naombeni ushauri wenu uwe mzuri mkuu maana hii ela ikipotea pasipo kupiga atua naweza kufa kwa pressure maana nimeipata kwa tabu mnoo)

Maeneo ya kimakazi ni mawili Dar es Salaam pamoja na Mwanza.

Karibuni kwa ushauri.
 
Kwa Dar unaweza usipate hiyo faida unayo utaka ya elfu 50 lakini ukapata elfu 20 to 25 ukipata eneo zuri

Tafuta mashine ya kusaga juice ya miwa tafuta sehemu yenye mchanganyiko mkubwa sana mfano k koo Mbagara Rangi Tatu Temeke, Buguruni na mfano wa hizo

Ukipata kijana mzuri wa kusimamia biashara yako unaweza usikose elfu 20 kwa siku mtaji wake weka 1 million ambapo unapata mashine ya umeme around laki 6 mpaka 7 nzuri aisumbui

Unapata vifaa machujio ndoo mtaji wa kununua miwa kununua umeme na kulipa kodi eneo husika ambapo ni elfu 2 mpaka 3 kwa siku kwa maelezo zaidi njoo DM.

Ni biashara me nafanya nina miaka miwili kwa siku kipindi cha kiangazi nimemwambia kijana me nataka 20 tu zikizidi zote zako na tunafanikiwa kila siku kwa uwezo wa Mungu. kikoozi
 
Kwa Dar unaweza usipate hiyo faida unayo utaka ya elfu 50 lakini ukapata elfu 20 to 25 ukipata eneo zuri

Tafuta mashine ya kusaga juice ya miwa tafuta sehemu yenye mchanganyiko mkubwa sana mfano k koo mbagara rangi tatu temeke buguruni na mfano wa hizo

Ukipata kijana mzuri wa kusimamia biashara yako unaweza usikose elfu 20 kwa siku mtaji wake weka 1 million ambapo unapata mashine ya umeme around laki 6 mpaka 7 nzuri aisumbui

Unapata vifaa machujio ndoo mtaji wa kununua miwa kununua umeme na kulipa kodi eneo husika ambapo ni elfu 2 mpaka 3 kwa siku kwa maelezo zaidi njoo dm

Ni biashara me nafanya nina miaka miwili kwa siku kipindi cha kiangazi nimemwambia kijana me nataka 20 tu zikizidi zote zako na tunafanikiwa kila siku kwa uwezo wa Mungu.
Shukrani mkuu
 
Njoo mtera tufanye biashara ya samaki wa kubanikwa,soko lipo songea ni uhakika,tukianza na 500k siyo mbaya. Bei ya samaki bwawani 30-35/= na bei ya kuuzia Songea ni 100-200/=

Nipo tayari kusimamia hiyo biashara,karibu sana
 
Nimemaliza chuo muda (2016) kidogo, nimesota sana kupata ajira, nimesota sana mpaka nilifikia kukata tamaa ya maisha, Mungu mkubwa mwaka jana mwezi wa 5 nikaja kupata kazi kwenye mradi mmoja hivi, kutokana na mapito ya kukosa kazi na kuangaika mtaani, nilijichanga mnooo mnoo nilijichanga kupita maelezo na sikutaka kupoteza hata sent tano kijinga.

Mwishoni nimefikisha kiasi cha sh Milion 10 cash.

Sina uzoefu na biashara kiukweli kabisa

Nina kiwanja kipo Dar (kama asset yangu nilikinunua nikiwa chuo kwa bumu), natamani sana nijenge (napenda sana sana nyumba)

Naombeni ushauri wenu; ni biashara gani nikifanya kwa siku naweza kulaza sh elfu 50 kama faida kupitia hiyo pesa milion 10 (naombeni ushauri wenu uwe mzuri mkuu maana hii ela ikipotea pasipo kupiga atua naweza kufa kwa pressure maana nimeipata kwa tabu mnoo)

Maeneo ya kimakazi ni mawili Dar es Salaam pamoja na Mwanza.

Karibuni kwa ushauri.
Usiingie kwenye biashara kwa kutegema faida tupu usishangae hizo ten zote zikakata kwahy ten chukua 5ml uingize kweny biashara

Sent from my TECNO WX3 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu kikoozi , ukiweza kujibu maswali haya matatu kiuhalisia, utatumia chini ya laki 5 kuanza kuingiza kipato japo elf 20 kwa siku.
Swali1: unatatua tatizo gani kwenye soko?( Mfano: kupunguza uzito,kuwaweka wajasiriamali online n.k)
Swali2: unawalenga kina Nani wateja wako? ( Mfano: waliotoka kujifungua, wastaafu, wajasiriamali n.k)
Swali3: wanapatikana wapi unaowalenga ( both online na offline) vipi utawafikia? ( Mfano free physical seminar na automatic emails marketing

Kutokea hapo utakuwa unakuza timu ya wasaidizi Kadri wateja wanavyokuelemea. Karibu kwa msaada BURE wa online marketing
0713039875
 
Na pia naomba usiingize pesa yote kwenye biashara, weka pesa kiasi kwenye biashara then pesa nyengine wekeza hata kwenye vipande hili iwe inakuletea faida kidogokidogo huku ukiangalia upepo wa biashara ukoje
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom