Kwenye hili nahitaji ‘Critical Thinking' tafadhali kama unajijua huna au hujabarikiwa nayo usipoteze muda wako

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,418
108,517
Je, Kujitokeza kwa mara ya Kwanza kwa Mwenyekiti Taifa CHADEMA Ndugu Freeman Mbowe na Chama chake hicho Kumruhusu Kuhudhuria Sherehe za Uhuru wa Nchi yetu tofauti na alivyokuwa akigoma na Chama chake pia Kutomtambua Rais Dkt. Magufuli Kunaashiria nini ndani ya CHADEMA, Demokrasia ya Tanzania, Ustawi wa Kisiasa nchini na Taswira nzima ya Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwakani 2020?

ANGALIZO

Kama unajijua huna ' Critical Thinking ' ya Kutukuka acha Kutupotezea muda na waachie Werevu wachangie bakia msomaji.
 
Mada zako ni nzuri sana. Ila unavyowapopoa wachangiaji haipendezi.

Anyways, kuhusu hili tukio naona mambo mawili. Kwanza ni upinzani kujaribu njia ya kumsogelea rais ili ageuze msimamo na jicho lake dhidi yao au kwamba sasa wakabiliane na mfumo wa siasa hizi za nginja nginja kwa kuwa na wapinzani wao jirani.

Pili kuelekea 2020 n uelekeo wa chama mbeleni hasa baada ya njia za misuli kuonekana kufua dafu na mwenyekiti wa Chadema kuinekana amepoteza kiasi fulani cha weledi wa uongozi, ameamua "kuiba" uelekeo unaoonekana kuungwa mkono na wabunge wengi na ambao ndiyo uelekeo wa mgombea mwingine wa nafasi ya uenyekiti Chadema ndugu Mwambe.

Ni move yenye lengo zaidi kurudisha ushawishi wa chama kwa wanachama na ushawishi wa mwenyekiti pia.
 
Huwezi kupigana na adui ukiwa mbali! Jisogeze kwake, msome na muelewe vizuri then rudi panga mashambulizi! This means jiwe ataamini kuwa wako pamoja hivyo ule ujingwa wa kuwafunga na kuwasumbua kila Mara hautakuepo maana yake ni kwamba chadema itapata muda wa kujiimarisha zaidi. Muda huo CCM watabweteka wakiamini kuwa wamesjamshinda Mbowe na Chadema....
 
Mkuu GENTAMYCINE unawatisha wachangiaji.

Critical thinking inatofautiana Kati ya mtu na mtu.

Waache watu watoe maoni yao.

Hapana Mkuu nikiwaachia Watu wote kuna wengine ' naturally ' tu ni ' Mapopoma Waandamizi ' hivyo watanikera na kuharibu.
 
Mada zako ni nzuri sana. Ila unavyowapopoa wachangiaji haipendezi.

Anyways, kuhusu hili tukio naona mambo mawili. Kwanza ni upinzani kujaribu njia ya kumsogelea rais ili ageuze msimamo na jicho lake dhidi yao au kwamba sasa wakabiliane na mfumo wa siasa hizi za nginja nginja kwa kuwa na wapinzani wao jirani.

Pili kuelekea 2020 n uelekeo wa chama mbeleni hasa baada ya njia za misuli kuonekana kufua dafu na mwenyekiti wa Chadema kuinekana amepoteza kiasi fulani cha weledi wa uongozi, ameamua "kuiba" uelekeo unaoonekana kuungwa mkono na wabunge wengi na ambao ndiyo uelekeo wa mgombea mwingine wa nafasi ya uenyekiti Chadema ndugu Mwambe.

Ni move yenye lengo zaidi kurudisha ushawishi wa chama kwa wanachama na ushawishi wa mwenyekiti pia.

Hizi ndizo ' Critical Thinking ' ninazozitaka. Asante Mkuu wa Uchambuzi wako ulioenda Shule na kwa Kunielewa vyema kabisa.
 
Kwa upande wangu naona ni approach nzuri huwezi kumkataa mtu wakati yeye ndio rais, mbali na hivyo ujumbe aliompa pale kuhusu demokrasia na ustawi wa nchi una uzito zaidi kuliko ingekua ni kupitia mitandao ya kijamii.

Hongera kwa Kujaribu Kuchangia Mkuu.
 
Tukio la leo lina maana nyingi, BINAFSI niainishe CHACHE.

1. Tukio hili linatokea wakati Mh. Lowassa na Mh. Sumaye tayari wamejiweka pembeni ndani ya CHADEMA.

✓ Sasa inawezekana CHADEMA wanajaribu kumuonyesha Mh Raisi kuwa watu hawa wawili walikuwa wakiwachonganisha CHADEMA, CCM na SERIKALI.

2. Tukio hili pia linatokea wakati CHADEMA wanakaribia kufanya Mkutano Mkuu kwa ajili ya kuchagua Viongozi wakuu wa Chama.

✓Implication yake inaweza kuwa, kwamba Mh. Mbowe na Kamati Kuu wameamua kushiriki SHEREHE HIZI ZA UHURU ili kumnyima CREDIT mpinzani wa Mh. Mbowe.

3. Msuguano wa kisiasa, wakati tukio hili linatokea kuna msuguano mkubwa wa Kisiasa.

✓ Inawezekana CHADEMA wameamua kushiriki ikiwa ni sehemu ya mbinu yao kujiimarisha kichama kwa WANANCHI.

4. Inawezekena pia CHADEMA wametumia siku ya leo kuwasilisha kilio Chao.

✓ Ukisikiliza vizuri hotuba ya Mh. Mbowe kuna ujumbe mzito sana ndani yake. Ujumbe huu umewasilishwa mbele ya Mabalozi wa Nchi mbalimbali pamoja na Viongozi mbalimbali wa Vyama na Serikali.

CHADEMA kuhudhuria Maadhimisho ya leo ni SPECIAL MISSION.
 
Mi naona mheshimiwa Mbowe kashauriwa aende na wakati maana siasa alizokuwa anafanya hazijaleta matunda kabisa zaidi ya kupoteza wabunge pamoja na mdiwani.
 
Siyo UTI tu mkuu.
Na leo mh MBOWE alienda huku akijua atapata nafasi ya kuongea. Matokeo yake amewapopoa kwa nondo za uhakika hata na wewe ukapata cha kuandika.

Jiulize kama asingeenda leo ungeandika nini wewe Gentamicine (jina ambalo ni dawa ya kutibu UTI) na unajimwambafai kuwa critical tenkers

MATAGA
 
ANGALIZO langu la katika huu Uzi ulilisoma na Kuliewa vyema? Kuna Watu hapa Jamvini huwa mnanilazimisha niwajibu hovyo.
 
Tukio la leo lina maana nyingi, BINAFSI niainishe CHACHE.

1. Tukio hili linatokea wakati Mh. Lowassa na Mh. Sumaye tayari wamejiweka pembeni ndani ya CHADEMA.

✓ Sasa inawezekana CHADEMA wanajaribu kumuonyesha Mh Raisi kuwa watu hawa wawili walikuwa wakiwachonganisha CHADEMA, CCM na SERIKALI.

2. Tukio hili pia linatokea wakati CHADEMA wanakaribia kufanya Mkutano Mkuu kwa ajili ya kuchagua Viongozi wakuu wa Chama.

✓Implication yake inaweza kuwa, kwamba Mh. Mbowe na Kamati Kuu wameamua kushiriki SHEREHE HIZI ZA UHURU ili kumnyima CREDIT mpinzani wa Mh. Mbowe.

3. Msuguano wa kisiasa, wakati tukio hili linatokea kuna msuguano mkubwa wa Kisiasa.

✓ Inawezekana CHADEMA wameamua kushiriki ikiwa ni sehemu ya mbinu yao kujiimarisha kichama kwa WANANCHI.

4. Inawezekena pia CHADEMA wametumia siku ya leo kuwasilisha kilio Chao.

✓ Ukisikiliza vizuri hotuba ya Mh. Mbowe kuna ujumbe mzito sana ndani yake. Ujumbe huu umewasilishwa mbele ya Mabalozi wa Nchi mbalimbali pamoja na Viongozi mbalimbali wa Vyama na Serikali.

CHADEMA kuhudhuria Maadhimisho ya leo ni SPECIAL MISSION.

Hizi ndizo ' Critical Thinking ' ninazozitaka. Asante Mkuu wa Uchambuzi wako ulioenda Shule na kwa Kunielewa vyema kabisa.
 
Mbowe, Lowassa, Sumaye, na kundi lao ni waumini wa dini zinazohubiri kusamehe wamekuwa wakihubiri kusamehe, ng'ambo ya pili naye Mfalme anahubiri kusamehe, hivyo basi imefika mahali wote wamejitambua kuwa wanachokuhubiri sicho wanachokitenda, yawezekana dhamira zimewasuta wakaamua kutazama maslahi ya nchi badala ya mizozo na kuumizana.
 
Sababu za Chadema kuazimia kuhudhuria kwa maoni yangu ni kama zifuatazo;

1. Hoja za Chadema kukosa nguvu.
Hii ni kutokana na Chadema wenyewe kuanza kukosa uhalali wa kuhoji suala zima la demokrasia.
Wengi walikuwa na hamu kuona jinsi Chadema kinavyokuwa mstari wa mbele kuonesha demokrasia ya kweli lakini umekuwa kinyume chake.Sababu zipo na mifano ipo wazi.
Hoja kama ya kupinga ufisadi imekufa na siyo agenda ya Chadema tena.CCM wameiteka na tunaona wanavyoifanyia kazi kwa spidi kama askari wa miavuli.

2. Kuonekana wazi kwa maendeleo ya miundo mbinu kama barabara,reli,nishati na kuimarika kwa usafiri wa anga na maji.Hii inafanya iwe vigumu sana kuwashawishi wananchi wasione na waanze kufikiri chama mbadala.Pamoja na kuwepo ugumu wa maisha lakini dalili zilizopo zinawapa matumaini wananchi wakiamini huenda huu ni mwanzo tu na hali itakaa sawa.

3. Kuimarika kwa nidhamu ya kazi serikalini ikiwa ni pamoja na kupungua sana kwa uonevu,kutotoa haki kwa waliopewa dhamana,na urasimu usiokuwa na sababu.Hata kama kuna sehemu bado hazijakaa sawa lakini ile hali ya mh.Magufuli kuchukua hatua za haraka kukemea na kuonya mara agunduapo 'madudu' ya jinsi hiyo yanafanywa,kunawafanya wananchi wawe na matumaini sana.Na zaidi pale wananchi wanapoona safu aliyonayo ikiongozwa na mh.Kassim Majaliwa jembe jingine hatari sana.

4. Faida za Chadema kuhudhuria ni nyingi na zinafanya wananchi waone kwamba kumbe ni wastaarabu licha ya kukutana na changamoto nyingi katika utendaji wao kisiasa.Hasara ya wao kutohudhuria ingekuwa kubwa zaidi kwani wananchi wengi hawaguswi sana na maumivu wanayoyapata wao Chadema na hivyo wangebaki wakiwashangaa tu kwa nini wanasusia ili hali Rais akitekeleza mambo mengi ya kimaendeleo na yanaonekana.

5. Mh.John Pombe Magufuli licha ya mambo ya maendeleo,ameonesha kuwa yeye ni binadamu mwenye huruma na mwenye msamaha.
Kuna mambo kama ya kusamehe wafungwa ambao walihukumiwa kunyongwa tangu enzi za Utawala wa awamu ya kwanza hadi leo yameleta hisia sana kwa wananchi na kumuona mtu huyu ni mwenye moyo wa pekee sana.
Kwa mambo kama hayo amejipatia wafuasi wengi sana na hivyo wanamchukulia kama mzazi hata kama atateleza katika kauli,watanzania wengi walishamsamehe pia
 
Sawa Mkuu nimekupata.

Mliokuwa mnasema kuwa niache kila Mtu ( hata Mapopoma ) kwa mfano mmeona sasa shirima Mathias alivyochangia kwa Dhihaka na Uchokozi dhidi yangu? Siku zingine ninapokuwa nasema kuwa kuna Watu tunao hapa wana ' Upumbavu ' mwingi na ndiyo huwa wananikera hadi nawajibu hovyo muwe mnanielewa tafadhalini sawa? Huu Uzi nimeuanzisha ' Makusudically ' kabisa ili utusaidie kwa vingi na mengi hasa kama ' Great Thinkers ' lakini linatokea tu ' Popoma Jiandamizi ' Moja kama hilo hapo juu linaanza ' Kupopomika ' zake hapa.
 
Back
Top Bottom