Kwenye hili la mtoto wa Rais Magufuli kuumwa Corona na Kabudi kufuata dawa Madagascar nimeamini Rais hana upendeleo

Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Mar 16, 2015
1,393
3,234
Baada ya kumsikiliza Rais John Pombe Magufuli akizungumzia jinsi mwanaye alivyojitibia corona nimeamini kweli Mheshimiwa Rais hana upendeleo kwenye hili swala.

Nilitegemea Rais angesema mwanangu alipewa ile dawa ya utafiti niliyomtuma Kabudi kuchukua kule Madagascar lakini kumbe mwanaye naye alitumia hizi hizi nyungu na malimao kama walalahoi wengine tu.

Huu aliofanya Rais ni uzalendo na uungwana wa hali ya juu. Angekuwa Rais mwingine ile dawa ya Madagascar ingeishia kwa mwanaye lakini Magufuli ameacha dawa ya Madagascar itumike kwa ajili ya utafiti na mwanaye ajitibie kwa malimao na nyungu kama watu wengine.

Tumpongezeni Mheshimiwa Rais kwa kutokuwa na upendeleo katika hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mataga rahisi sana kuyatapeli na kiyadanganya
Madem wa MATAGA watakuwa wanapigwa sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa, sijaelewa, kilichomuaminisha ni nini kuwa huyo mtoto alitumia NYUNGU badala ya hizo dawa za Madagasca?
Hajui pia, inawezekana hata kuzifuata huko, ni kwa ajili ya huyo mtoto?
Na jana likanijia wazo kuwa mkuu amejikarantini huko kwao baada ya mwana wa nyumbani kwake kuugua huo ugonjwa!
 
Rais mwenyewe amesema ina maana wewe humwamini mkuu wa nchi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom