Kwenye hili la COVID19, naweza kuona mahesabu ya Rais Magufuli. Je, tumuunge mkono?

Amen! Zimetua wapi boss
ITV wametangaza zimetua KIA, moja kutoka Marekani na moja kutoka SA, na wakaonesha wakifanya mahojiano na baadhi ya abiria. Ila kuna bandiko humu JF linakanusha ati Kigogo2014 kwenye twitter yake amekanusha ndege iliyooneshwa ni ile iliyotua Ujerumani na kuruka hadi Ugriki.

Hayo ndiyo mambo ya media.
 
Dah! Inabidi tupate uhakika kiongozi, halafu tuwakate kilimilimi hao kina Kigogo2014
 
Maisha yanaendelea kama kawa. Jisogeze kwenye biashara yako, kumekucha

Wanabodi, Tulileta uzi hapa wa malalamiko ya watu kuzikwa usiku huko kondo ununio, Mamlaka ilikiri makosa na kulishughulikia kwa uungwana zaidi

Kuna hii taarifa au tetesi zinasambaa kuwa Wagonjwa ambao hawajapona vizuri corona wameondolewa vituoni au karantini na kuruhusiwa waende majumbani kujifukiza yaani uraiani

Hii hali ya kuruhusu Wagonjwa wa corona warudi majumbani sio ndio hatari zaidi kwenye jamii husika kwa ndugu na jamaa

Tunaomba mamlaka waifikirie hii order kwa jicho la tatu,Lengo linaweza likawa kupunguza hofu kwa Raia, Lakini ni vyema Raia wakaambiwa ukweli kuwa Wagonjwa wanarudishwa majumbani toka vituoni

Nakubaliana na Mamlaka kuwa corona ipo na wananchi wachukue tahadhari zaidi

Je wananchi baada ya kuambiwa corona imeisha watachukua tahadhari?

Je ni mikakati gani imewekwa kwa hawa wagonjwa kuugulia majumbani baada ya kuondolewa kwa order karantini?

Wameambiwa wajifukize na kujifungia ndani kutokana na order, Je huko mitaani na majumbani nani atawafuatilia hawa wagonjwa

Hizi ni tetesi zinazosambaa kwa kasi huko Dar es Salaam na Arusha baada ya majirani kuona wagonjwa wameruhusiwa kurudi mitaani huku hali ikiwa bado tete na hawajapona vizuri

Tunaambiwa vituo au karantini havina watu, Kwa mfumo huu wa kuwaondoa Wagonjwa kwa order sio ni hatari zaidi

Je vituo au karantini havina watu ni kutokana na hii order ya kuwarudisha wagonjwa wasiopona vizuri majumbani au ni hofu tu ya Raia kukutana na mtu aliyepona korona

Yeyote aliyeshuhudia hali ya wagonjwa kurudishwa majumbani, Tunaomba asaidie mbinu alizotumia kwa mgonjwa kutotoka na kutoambukiza ndugu na jamaa

Hii order kama imetolewa ina lengo gani? Tahadhari gani zimezingatiwa kwenye order hii?

Je Vihatarishi Uchunguzi au Risk assessment ya order hii imeangaliwa na wataalamu kuwa kuna Madhara gani baadae ya kuwaruhusu Wagonjwa wasiopona wakachangamane na jamii
courtesy seedfarm
 
Jmushi1, ndege za watalii zimeanza kutua, unarudi kibaruani. Kila la kheri
Unadhani kama serikali ingetoa taarifa ndo ugonjwa ungesambaa zaidi? Maana kwenye utalii hili linaweza kutuletea shida. Mfano Europe wenyewe wanataka kuwazuia wamarekani kwasababu ya ongezeko la maambukizi. Sasa ambao hatutangazi si itakuwa shida sana kwenye utalii? Ama hapo tunafanyaje?
 
Nchi zinazotangaza zimepata mabadiliko gani katika kupunguza au kuongezeka maambukizi. Nadhani mkakti sahihi ni wa rasimali nyingi kutumika katika kudhibiti maambukizi na si kuyashangilia.
 
Back
Top Bottom