jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 24,967
- 22,476
Tanzania Demographics
Tanzania has a very low median age with more than 44.8% of the population under 15, 52% between 15 and 64 and just 3.1% over the age of 64.
Wanajamvi, nimeona nianze kwanza na hako kakipande hapo juu ili niweze kwenda kwenye hoja yangu moja kwa moja!
Kwanza niseme nimekuwa nikisumbuka sana na hali inavyoendele nchini, kana kwamba kiongozi mkuu na wasaidizi wake kuna jambo wao wanalifahamu lakini sisi hatulifahamu!
Hata hivyo, juhudi zote za kujiuliza na kijifikirisha, zimepelekea mimi kuja na wazo hili. Kwasababu ni wazi tumetofautiana wengi wetu na kama Taifa kuhusiana na namna serikali yetu inadeal na hii world pandemic!
Scenario ninayodhani inachukuliwa Tanzania.
Kama data zinavyoonyesha, ni kwamba Tanzania ina idadi ya vijana ambao ni asilimia 90 ya Watanzania wote. Wazee wenye miaka 64 na kuendelea, ni asilimia 3.1 tu ya wananchi wa Tanzania. Ina maana tuna risk ndogo sana inapokuja kwenye corona. Na wengi wenye magonjwa sugu wanaangukia kwenye group la wazee.
Sasa kuna aina mbili za immune ambazo zinafahamika na kukubalika duniani kote, nazo ni...
I)kupitia chanjo(vaccine)
II)Kupitia “herd immunity” ama kinga inayopatikana baada ya kupona gonjwa hilo.
Kila gonjwa, huwa linapewa asilimia zake za kufikia kutokana na jinsi ambavyo lina kasi katika maambukizi, mfano ugonjwa huu wa covid-19, wataalam wanasema kutokana na kasi yake ya maambukizi, basi ni lazima asilimia 70 ya wananchi wote wapate corona ndipo tunaweza kusema Tanzania tuna kinga kupitia “herd immunity”. Hapo ikiwa ina maana asilimia 30 iliyobakia inaweza kulindwa mfano wazee, wenye magonjwa sugu nk. Lakini kwasababu tuna vijana asilimia 90, basi ina maana hatutapata shida hata kidogo kuzipata hizo asilimia 70 zinazohitajika na WHO.
Nearly 44% of the population is under the age of 15. The median age of the Tanzanian population is only 17.7 years of age,
Kwasababu vijana hawaathiriwi sana na corona, ina maana tuna faida inapokuja kwenye “herd immunity”, ama huu mfumo unaotumika sasa nchini kwasababu kama tuna vijana asilimia 90, hatuwezi kukosa asilimia 70 za kutuwezesha kupata herd immunity na kuishinda corona.
Lakini hata hivyo data ni muhimu kufahamu tulipofikia. Pengine viongozi wameliona hilo kwasababu wao ndo wenye kuziona data, na ndiyo maana wanakuwa optimistic na kutangaza kuwa tumeishinda corona.
hata hivyo, pia ukifuatilia kauli zao na matendo, ni kama vile wanataka wananchi wengi kadri iwezekanvyo, waupate ili tufikie ile asilimia 70 inayotakiwa.
To be continued...
Tanzania Population 2020 (Demographics, Maps, Graphs)
Nguruvi3 Kalamu1 JokaKuu Daudi Mchambuzi