Kwenye hili Freeman Mbowe ulitudanganya Watanzania

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
5,687
15,108
Habari Wadau,

Kutokana na kasi ya serikali ya awamu ya tano katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi, sasa nashawishika kusema kuwa tulidanganywa kwamba matatizo ya Watanzania kutopata maendeleo yanasababishwa na MFUMO.

Chadema walikuwa wanahubiria Watanzania kuwa maendeleo hayatawezekana mpaka mfumo mzima wa CCM uondolewe madarakani na kuingia chama kingine.

Freeman Mbowe aliitisha press conference na kuwashawishi wa Tanzania kwamba Chadema itampokea Lowassa hata kama ni fisadi na akiwa Rais kupitia mfumo wa Chadema atakuwa ametakaswa na kuacha ufisadi wake kwa sababu Chadema ina mfumo mzuri. Mbowe alisema hata kama Magufuli siyo fisadi lakini akiwa rais kupitia mfumo wa CCM uliooza basi atageuka kuwa rais fisadi na wa Tanzania wasitegemee maendeleo yoyote kwa miaka mitano ijayo.

Lakini baada ya CCM kurudi madarakani mwaka 2015 wakiwa na rais Magufuli mambo yamebadilika kabisa.

CCM hiyo hiyo iliyokuwa imeoza kabisa, sasa wanatoa elimu bure, wananunua ndege, wanajenga, bwawa la umeme, flyovers na hata maofisini utendaji kazi umeimarika kabisa tofauti na zamani. Ujenzi wa SGR sasa umefika Dodoma na muda siyo mrefu wa Tanzania watakuwa wana-enjoy ndani ya treni umeme, machinga na mama ntilie hawanyanyaswi tena na mgambo etc.

Swali: Ni nini kimeibadilisha CCM?

Jibu: Ni usimamizi na ufuatiliaji imara wa rais Magufuli na siyo mfumo kama tulivyokuwa tunaaminishwa na wasaka madaraka.

Ufisadi ni tabia ya mtu na siyo mfumo kama tulivyokuwa tunadanganywa na kina Mbowe, mtu kama ni fisadi atakuwa fisadi tu hata kama atakuwa rais kupitia Chadema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maendeleo hayaji bila Uwazi, hata yakija ni kwa kuchelewa sana na kuacha makovu makubwa kwa watanzania!

Ndio maana unaona takwimu zetu hazipo sawa hata kidogo, tunacheza na taarifa za kupika,CAG anazuiwa kufanya ukaguzi baadhi ya maeneo nyeti.

Kiufupi ndio maana hata wewe unasifia kila kitu kwa sababu ya mfumo.
 
Kuziona ndege,elimu bure ,SGR mpaka usubiri CAG?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wadau,

Kutokana na kasi ya serikali ya awamu ya tano katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi, sasa nashawishika kusema kuwa tulidanganywa kwamba matatizo ya Watanzania kutopata maendeleo yanasababishwa na MFUMO.

Chadema walikuwa wanahubiria Watanzania kuwa maendeleo hayatawezekana mpaka mfumo mzima wa CCM uondolewe madarakani na kuingia chama kingine.

Freeman Mbowe aliitisha press conference na kuwashawishi wa Tanzania kwamba Chadema itampokea Lowassa hata kama ni fisadi na akiwa Rais kupitia mfumo wa Chadema atakuwa ametakaswa na kuacha ufisadi wake kwa sababu Chadema ina mfumo mzuri. Mbowe alisema hata kama Magufuli siyo fisadi lakini akiwa rais kupitia mfumo wa CCM uliooza basi atageuka kuwa rais fisadi na wa Tanzania wasitegemee maendeleo yoyote kwa miaka mitano ijayo.

Lakini baada ya CCM kurudi madarakani mwaka 2015 wakiwa na rais Magufuli mambo yamebadilika kabisa.
CCM hiyo hiyo iliyokuwa imeoza kabisa, sasa wanatoa elimu bure, wananunua ndege, wanajenga, bwawa la umeme, flyovers na hata maofisini utendaji kazi umeimarika kabisa tofauti na zamani. Ujenzi wa SGR sasa umefika Dodoma na muda siyo mrefu wa Tanzania watakuwa wana-enjoy ndani ya treni umeme, machinga na mama ntilie hawanyanyaswi tena na mgambo etc.

Swali: Ni nini kimeibadirisha CCM?

Jibu ni usimamizi na ufuatiliaji imara wa rais Magufuli na siyo mfumo kama tulivyokuwa tunaaminishwa na wasaka madaraka.

Ufisadi ni tabia ya mtu na siyo mfumo kama tulivyokuwa tunadanganywa na kina Mbowe, mtu kama ni fisadi atakuwa fisadi tu hata kama atakuwa rais kupitia Chadema.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ni mjinga na mpumbavu
IMG_20200422_202414.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zuzu kaanzisha Uzi eti alidanganywa na Mbowe!What a classical moron!Maendeleo?Unataka kueleza maendeleo gani sasa?Hayo uliyoeleza hata Ethiopia yamefanyika ila kila siku wanapanda malori kuitoroka nchi yao.Umejiuliza kwa nini?Akili zenye matege.
 
Back
Top Bottom