Kwenye hii scandal ya escrow tusiishie na maadhimio ya bunge tu

Uthman

Member
Apr 24, 2012
83
201
Kwa hakika tumezoea scandal mbali mbali kwisha punde tu mawaziri wanapojiuzulu au Bunge linapotoa maadhimio baada ya kamati zake kufanya uchunguzi.Lakini ndugu zangu kwa uzito wa hii scandal ya ESCROW nawaombeni tuunganishe nguvu ili twende mbali zaidi kuhakikisha hatua zaidi zinachukuliwa kwa wahusika wote zaidi ya kuondolewa nafasi zao.

Haiwezekani Watanzania wote tufanywe wapumbavu na singa singa mmoja akishirikiana na wasomi wetu wa makaratasi halafu tukubali kiwepesi kabisa mambo yaishe kwa watu wachache kuwajibishwa.

Hivi tunavyozungumza tayari Standard Chartered Bank-Hong Kong kupitia kwa mwanasheria wao Mathew Weiniger,wameleta barua rasmi kuitaka TANESCO ihakikishe kuwa pesa zimerudishwa kwenye account ya escrow haraka sana.Tusipofanya juhudi za kuwanyanganya pesa hawa majambazi,itabidi wananchi watanzania tulipe hizo pesa zote.

Mapendekezo yangu kwenu wanajamii ni kwamba tuishinikize serikali kupitia asasi za kiraia,vyama vya siasa,mitandao ya kijamii na vyombo huru vya habari kuchukua hatua zifuatazo:-

i.) Mwanasheria mkuu wa serikali,Waziri wa Nishati na Katibu mkuu wake,bodi ya wakurungenzi wa Tanesco, wafilisiwe mali zao zote ili pesa zitakazo patikana zirudishwe kwenye mfuko wa TANESCO.

ii.) Menejimenti nzima ya TANESCO ivunjwe,wafilisiwe na wafikishwe mahakamani kwa kosa la kutosimamia mali za shirika ipasavyo.Tukumbuke tayari kuna hukumu ambayo TANESCO wameshinda ya kwamba IPTL ilikuwa ina wa OVERCHARGE kipindi chote cha uzalishaji wake.Walipewa siku 90 wakubaliane formula mpya ya kukutoa malipo stahili ya umeme lakini wamekaa mpaka hivi leo hawajakokotoa.Hii ni hujuma kwa nchi kwani tunaendelea kulipa gharama kubwa bila sababu.Vile vile kama wangefanikiwa kukutoa mapema basi Tungejuwa pesa halis tunazowadai IPTL.Profesa Lipumba anasema pesa zote za ESCROW hazitoshi kwa IPTL kuwalipa TANESCO kama wakikokotoa gharama halisi.
Mkurugenzi mkuu wa TANESCO na watu wake wasipone katika hili.Wao kama wahusika namba moja walikuwa na nafasi ya kuwajulisha watanzania mashinikizo yoyote ya kutoa pesa kinyume na mkataba.

iii.) Tuhoji umakini wa ofisi ya Rais katika kubariki wizi mkubwa kama huu.Hatuwezi kumuwajibisha kikatiba lakini tuandae utaratibu wa kukusanya saini za kutokuwa na imani na ofisi yake, au tuandae electronic voting ya rating ya utendaji wake.

iv.) Wabunge wote waliokuwa wakiona wizi huu sio tatizo tuwashtaki kwa wapiga kura wao ili waadhibiwe kwa kutorudishwa bungeni kipindi kijacho.Vile vile twende mbali katika kuwashauri umuhimu wa kuwa na makatibu katika ofisi zao na kuwatumia ipasavyo kufanya research na kukusanya data mbali mbali kwa hoja muhimu zinazowasilishwa bungeni.Kwakweli michango ya wabunge wetu wengine ni aibu kubwa kwetu kama taifa.Inabidi kujiuliza hivi kweli sisi watanzania ufahamu wetu ni mdogo kiasi hiki mpaka tunafikia kuchagua mbunge ambaye hajui hata anawasilisha nin bungeni.

iv.)Tuishinikize serikali ianike hadharani watu wote waliopokea fedha za ESCROW kupitia STANBIK na MKOMBOZI ,na wabanwe wazirudishe zote.

v.) BOT izipige faini benki za MKOMBOZI na STANBIK kwa kuruhusu account moja kutoa kiasi kikubwa mno cha pesa kwa muda mfupi sana bila kuzuia na kuvishirikisha vyombo vya ulinzi na usalama.Haiwezekani mtu aweke kwenye account Bilioni 75 na azitoe ndani ya siku mbili, hata kama ni zako hii ni money laundering.


Nawasilisha kwenu kwa michango zaidi ya hatua za kuchukua ili wezi na mafisadi wengine waanze kuziogopa rasilimali za watanzania.
 
Watanzania tusiwe waoga katika kusimamia rasilimali zetu,Leteni maoni tutengeneze response kali ili heshima kwa mali zetu irudi japo sawa na kipindi cha marehemu Edward Moringe Sokoine,kipindi ambacho mali zetu ziliogopwa na kuhifadhiwa kwa sababu tu ya ushupavu wa mtu mmoja.
 
Siyo adhimio mkuu...Ni Azimio.
Makosa ya kisarufi kama hayo yanapunguza ladha ya thread yako Ingawa content ni nzuri...

Ni muhimu kupunguza papara na kuongeza umakini.
 
Back
Top Bottom