Kwenye Haki za Wanyonge, Magufuli ni Kama Khalifa Mkuu Harun El Rashid wa Alfu Lela Ulela!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,180
Wanabodi,

Hili ni bandiko la simulizi ya Kayafa Mkuu wa Bhaghdad enzi za simulizi za Alfu Lela Ulela, Khalifa Harun El Rashid, lengo likiwa ni kuwahamasisha wana jukwaa kuwa kwenye mazuri tupongeze, kwenye mabaya tukosoe na kwenye maovu tulaani, hivyo linapokuja suala la haki bin haki zikiwemo haki za wanyonge, naombeni muungane nami kumpongeza kwa dhati, rais wetu Dr.John Pombe Joseph Magufuli kwa kuwa ni mtetezi wa kweli wa haki za wanyonge.
Naomba kabla sijakisema nilichokusudia, kwanza soma hii simulizi hapa chini
Kayafa Mkuu Khalifa Harun El Rashid.
Kwa wale wa zamani waliosoma vitabu hadithi vya Hekaya za Abunuwas na Alfu Lela Ulela, hadithi nyingi zimemzungumzia Kayafa Mkuu wa Baghdad enzi hizo kwa jina la Khalifa Mkuu, Kayafa Harun El Rashid alivyokuwa ni mtu wa kutenda haki bin haki kwa kutoa haki kwa wote wakiwemo wanyonge, maana kikawaida mnyonge huwa hana haki mpaka mwenye nguvu aseme.

Moja ya simulizi hizo ni kisa cha mwanamke mjane masikini aliyeachwa kizuka na msiba wa mumewe mpenzi waliopendana sana na kuishi muda mrefu bila kujaaliwa kupata mtoto hadi mumewe anafariki hawakubahatika kupata mtoto.

Katika mji huo kukawa na tajiri mkubwa mwenye mali nyingi, wake wengi, watumwa wengi, mifugo mingi, in short alikuwa na kila kitu isipokuwa hakubahatika kupata mtoto na sasa umri umekwenda. Akatoa nadhiri kwa mke wake yeyote atakaye mzalia mtoto, mtoto huyo ndie atakuwa mrithi wa kila kitu pale atakapofariki na ni mama atakayepata mtoto ndio atarithi kasri lake. Then just imagine harakati za kusaka ujauzito miongoni mwa wake wa tajiri huyo. Huku na kule mara paa!, mke mdogo wa tajiri huyo kashika ujauzito, (wanawake wakisasa wakigundua kushika ujauzito wa tajiri ni dili, hata kama tajiri mwenyewe hawezi kushikisha ujauzito, atashikishishwa or ikishindikana kabisa kumshikishisha, then, atashikishiwa!).

Mwanamke wa Kiislam akifiwa na mumewe, hukaa edda siku 90 ili kujiridhisha mwanamke huyo yuko ok na hana kiumbe cha al marhum, baada ya siku 90 akiwa OK, anaruhusiwa kuolewa tena, lakini alikutwa na ujauzito wa marehemu mumewe hivyo anakuwa hawezi kuolewa tena mpaka baada ya uzazi.

Yule mwanamke masikini alifiwa na mumewe, hivyo akakaa edda siku 90, ni kwenye edda, ndipo ikagundulika mwanamke huyo akakutwa na kiumbe, akailea mimba yake kwa taabu, shida, dhiki na mateso hadi siku ya kujifungua.

Kule kwenye kasri la Tajiri nako bi mdogo, mrembo mrembo kweli, akashika ujauzito. Taarifa kumfikia mumewe tajiri, alipata furaha isiyo kifani, akaamuru kuanzia siku hiyo, bi mdogo asifanye kazi yoyote hadi siku ya kujifungua. Mumewe akamuwekea wajakazi wa kutosha hadi kuoga alikuwa haogi tena bali anaogeshwa!. Kwa vile kati ya wake zote wa tajiri yule, ni yeye pekee amebahatika kushika ujauzito, hivyo kuna hatari ya wake wenzie kumuonea vivu, wakamdhuru hivyo akamletea wapishi maalum kumpikia chakula chake, alikuwa na wahudumu zaidi ya 10 wakimuhudumia.

Kufuatia tajiri huyo kuoa wake wengi bila kufanikiwa kupata mtoto, hivyo ujauzito wa mke mdogo ukatiliwa mashaka kama kweli ni wa tajiri, hivyo ikasomwa itkafu, kama kiumbe sio cha tajiri, Allah afanye yake kwa kumtuma Israel kutimiza wajibu wake.

Siku ya uchungu kwa bi mdogo tajiri, ika coincide na siku ya uchungu kwa mwanamke masikini, wakajikuta wamelazwa hospitali moja na usiku huo wakajifungua pamoja, vichanga vya kiume.

Katika kujifungua yule mwanamke tajiri kutokana na kubweteka, hakuwa na mazoezi yoyote, akashindwa ku push, na matokeo ya mwanamke mjamzito akishindwa ku push, tunayajua ndio maana inasisitizwa sana mazoezi ni muhimu kwa wamama wajawazito. Yule mwanamke masikini kutokana na shita, taabu na matatizo, alikuwa ngangari, akajifungua salama bila tatizo lolote, akakiangalia kichanga chake na kukiona kina birth mark ya baba yake kwenye paji la uso wake, hivyo ni copyright ya mumewe kipenzi, akafarijika sana, na kukabidhi kichanga kwa wakunga kikaoshwe.

Kwa vile kichanga cha tajiri ni sii riziki, kichanga cha masikini bukheri wa afya. Mwanamke tajiri, kwa kuijua sababu ya kichanga chake kuwa sii rizki, na lengo ni kuwa mrithi wa utajiri wa mumrwe, huku akiamini kukipora kichanga cha masikini ni kukinusuru kugeuka chokoraa kama mama yake na pia ndio kumsaidia huyo mwanamke masikini asije kitumbukiza kwenye shimo la choo, au kukitelekeza, hivyo akatumia jeuri ya pesa zake, akahonga wakunga kubadilisha vichanga yule bukheri akapewa mwanamke tajiri na yule sii riziki akapewa mwanamke masikini. Yule mwanamke masikini akalia sana kwa uchungu kuwa kichanga bukheri ndie mtoto wake, hakuna aliyemsikiliza!. (masikini huwa hana sauti mbele ya tajiri mwenye pesa),

Kayafa alikuwa na tabia ya kutoka under disguise na kujichanganya na watu wa hali zote na kupata first hand info kwa masikio yake na sio kusubiri kuletewa. Hivyo siku hiyo katika tembea tembea zake, akainyaka hiyo ya kugombea mtoto, kesho yake akatuma ujumbe, wanawake wote wawili waje, waletwe mbele ya baraza lake, tajiri na kichanga bukheri na masikini na maiti.

Khalifa akawasikiliza wote wawili na kusikiliza ushahidi wa mkunga wote wakamkandamiza yule masikini.

Kayafa akatoa hukumu ya haki bin haki kuwa ili kumaliza huo mgogoro mtoto anayegombewa bora agawanywe nusu kwa nusu ili kila mwanamke apewe nusu ya mtoto.

Ukumbi mzima ukazizima kwa makofi na vigelegele kuwa kwenye kila mgogoro wa kugombea kitu, haki bin haki ni kugawana pasu kwa pasu kwa kitu kinachogombewa, ili kila mmoja apate nusu, yaani a win win situation!.

Baada ya ukumbi kutulia akatoa fursa kwa washitaki kutoa neno la mwisho kabla ya utekelezaji wa hiyo hukumu.

Akaanza mwanamke tajiri, huku akionyesha uso wa furaha alimshukuri Khalifa Mkuu Kayafa Harun el Rashid kwa kutoa hukumu ya haki, hivyo mtoto akigawanywa kila mmoja atakuwa ametendewa haki. Ukumbi makofi na vigelegele.

Ilipokuja zamu ya yule mwanamke masikini, yeye aliendelea kulia tuu kwa uchungu na kumuomba Khalifa Mkuu kuwa anaomba kufuta kesi ya kugombea mtoto, na kusema basi yuko tayari kupokea ile maiti ya kichanga ndiye mwanaye na kile kichanga bukheri ni cha mwanamke tajiri, hivyo anaomba msamaha kwa kugombea mtoto wa mwenzake, hivyo hagombei tena na yuko tayari kupokea adhabu ya kifo kwa kusema uongo mbele ya Kayafa.

Ukumbi mzima ukaibuka na kelele za zomea zomea huku wakiimba "asulubiwe!, asulubiwe!". Kwa kawaida mtu ukisema uongo barazani kwa Kayafa Khalifa Mkuu, unahukumiwa kifo kwa kusulubiwa! .

Ndipo Khalifa Mkuu akaunyamazisha ukumbi huku watu wakitaraji hukumu ya kusulubiwa kwa mwanamke masikini ndio inatangazwa kwa sababu ameisha kiri kosa la kusema uongo mbele ya kayafa.

Khalifa akasema kabla sijatangaza hukumu ya kusulubiwa ningependa kumsikia huyu mwanamke kwa nini amedanganya na kuja kukiri barazani ambapo anajua hukumu yake ni kifo?.

Ndipo yule mwanamke masikini huku akiendelea kulia kwa kububujikwa machozi akasema kiukweli kabisa, mtoto hai ni wakwake, na alipozaliwa alimuona na ile alama ya marehemu baba yake kwenye paji la uso wake, lakini kwa vile hukumu ni ya mtoto kugawanywa nusu kwa nusu kila mtu apate nusu, kitendo cha kumgawanya mtoto kwa kuchinjwa, hivyo mwanaye kuuwawa, kuliko mwanae kuuwawa bora akubali tuu kuwa mtoto ni wa mwanamke tajiri ili aendelee kuishi kwa alelewe na mwanamke mwenzake angalau atabaki hai kuliko kuridhia utekelezwaji wa hukumu ile, na kwa jinsi anavyompenda mwanae, baba yake ameishakufa, kama mtoto atagawanywa, na yeye atakufa kwa kihoro, hivyo ameamua bora aseme kuwa amedanganya, ili akubali kuutoa uhai wake kumuokoa mwanaye.

Ndipo Kayafa Mkuu Khalifa Harun El Rashid akatoa hukumu ya haki bin haki. Akaamuru mtoto akabidhiwe kwa mwanamke masikini na atahudumiwa na serikali maisha yake yote na kibao kikamgeukia mwanamke tajiri na wakunga waliokula ile dili.
Baada ya simulizi hiyo, sasa shuhudia kitu kilichofanyika jana kwa huyu mwanamke mjane, halafu angalia rais Magufuli alifanya nini.

Kitendo alichokifanya jana rais Magufuli cha kumsikiliza yule mwanamke ndicho alichokifanya Kayafa Mkuu Khalifa Harun el Rashid kwa yule mwanamke mjane masikini, na kiukweli kitendo kile kimenigusa sana, angekuwa mwingine, angeachia yule mwanamke mjane ashughulikiwe kikamilifu na vyombo vya dola na isingekuwa rais kumkomboa, hapo ambapo angelalia usiku wa jana, ni Mungu tuu pekee ndiye angejua kilichomkuta!, sijui hata kama angefika asubuhi salama, maana hawa polisi wetu sometimes, ni machoni tuu ndio kama watu, lakini mioyoni mwao ni wanyama kabisa!, ma beast ya ajabu!.

Kilichofanyika jana kinatoa somo kubwa sana kwa wanawake wengine na wanyonge wanaoteswa kwa kukosa haki, jinsi yule mama alivyoonyesha ujasiri na ushujaa kudai haki mbele ya rais ni uthibitisho kuwa haki hailetwi kwenye kisahani cha chai, haki inadaiwa kwa nguvu zote, na ikibidi inapiganiwa, hata kuweza kukifikia mahali, unaweza kujikuta uko tayari kufa kwa kuutoa uhai wako kupigania haki, watakaofaidika ni watoto wako na watoto wa watoto wako!. Hivyo linapokuja suala la kupigania haki, kutetea haki, hata sisi jf, tusiwe na mswalie Mtume na mtu yoyote mminyaji haki, tupiganie haki zetu kwa nguvu zote!.

Mnaweza kujiuliza hivi kweli ni Magufuli huyu huyu dikiteta, sasa ndiye mlinzi wa haki za wanyonge?!, sasa inawezekanaje mtu huyo huyo ni mtetezi wa haki za wanyonge kwa upande mmoja, lakini hapo hapo akawa ni ndiye mminyaji mkubwa wa haki za kisiasa?!.

Usikute inawezekana, ameamua kuminya demokrasia na haki za kisiasa, kwa sababu, hao political players, mnaowadhania ni wanasiasa wa kweli, kumbe Magufuli amewashitukia kuwa sio wanasiasa chochote, wala lolote bali ni wapiga dili tuu za kisiasa, kwa mgongo wa siasa, if that is the case, then, kwa vile Magufuli ameamua kuwashughulikia wapiga dili wote, then, ni wapiga dili wote wanashughulikiwa, hadi wapiga dili za kisiasa!, hivyo kuhalalisha kuminywa kwa demokrasia, kuvunja katiba kwa kupiga marufuku mikutano ya kisiasa kwa sababu hao wanasiasa wote wa vyama vingine, kwake ni wapiga dili tuu, wanasiasa wa ukweli ni CCM tuu pekee!. Tumshukuru pia kwa hatua hii ya kuwashtukia wanasiasa wapiga dili za kisiasa waliokuwa wanawapamatumaini Watanzania kuwa kuna siku moja CCM itaondolewa madarakani, kumbe walikuwa wanatuingiza chaka!. Ukweli ni kuwa CCM, itatawala milele!. Ndicho chama pekee chenye hati miliki ya kutawala Tanzania, hivyo Magufuli analisimamia hili kuhakikisha CCM haisumbuliwi na haibughudhiwi!.

Kwa upande wa rais Magufuli ameendelea kuthibitisha kuwa, when it comes kwenye manyanyaso ya wanyonge, yeye ni mtu wa watu, he is simply, a man of the people. Kama akiendelea hivi na kisha Roho wa Mungu wa kweli, akamuingia na kuachana na udikiteta wake wa asili, ambao ni kama ushetani fulani, na akazirudisha haki zote za msingi zilizoainishwa kwenye katiba yetu, mnaweza kushangaa by 2025 akawa kama ndiye Mfalme Suleman wa Tanzania!, hivyo Watanzania tukapiga kelele za kubadili katiba Magufuli aendelee milele na milele mpaka pale Mungu atakapoona inatosha na kumuita kwake!.

NB. Kwa pongezi hizi simaanishi kuwa sasa rais Magufuli ndio ghafla kageuka kuwa malaika!. No, kama rais Magufuli ni dikiteta, pamoja na wema wake huu, bado ni dikiteta vile vile, ila ni dikiteta mzalendo mwenye huruma fulani kwa watu fulani, lakini ni katili kwa wengine wakiwemo wapiga dili!.

Hongera sana kwa Rais wetu mpendwa, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, jana umeonyesha utu wa hali ya juu sana kumsikiliza yule mama mjane, na unastahili pongezi za dhati kutoka kwa wapenda haki wote, tunakuomba ujue tuu kuna makumi kwa mamia na maelfu ya Watanzania masikini wa kutupwa ambao wamedhulumiwa haki zao, na hawana courage kama ya huyo mama kukufikia, wengine hawa hata access ya kusikilizwa na wasaidizi wako, kuna mamia wanaozea magerezani kwa kesi za kubambikiwa, kuna mamia ni mahabusu wakuozea magerezani kwa kisingizio upelelezi haujakamilika mfano mzuri ni ni yule wakili wa Arusha Medium Mwale, huu ni mwaka wa 7 yuko mahabusu kwa kosa ambalo adhabu yake ni faini na kufungo cha mwaka mmoja!.

Tunakuomba huruma yako kwa wanyonge wanaonyimwa haki zao, ielekeze kwa wasaidizi wako ili Watanzania wote watendewe haki na sio kusubiri hadi kilio kikufikie wewe. Angazia watuhumiwa wa kesi za uhujumu, fuatilia uone ni wangapi wanaozea mahabusu kwa miaka na miaka bila hata kesi kuanza kusikilizwa. Justice delayed ni justice denied.

Mungu ibariki Magufuli aendelee kuhakikisha hata masikini na wanyonge, wanatendewa haki.
Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
Rejea

Rais Magufuli ni Simple, Genuine & Down To Earth-He is Simply A Man of The People!

Magufuli Kama Nyerere: Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'unyi, Ni Kazi Tuu, Ila Pia sio Kama Nyerere!

Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!.

Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?
 
Paskali ww ni msomi.Mm nahisi kwa tukio la huyu mama tusiwe wepesi wa kutoa suluhu kwamba kuna haki ananyimwa.Kote alikoanzia hawawezi kuwa na roho ngumu ya kupoteza haki.Vumilia tupate ukweli na nadhani ww mwenyewe unaweza rudi hapa na kututahadharisha kwamba si wote watoao machozi huwa ndo wafiwa.Tuachie mahakama zetu zifanye kazi.
 
Pascal Shemeji yangu ambaye eti nasikia jina lako ni NJAA wakati wapwa zangu na mdogo wangu wala mpaka wasaza huko kwa makao yako!Leo nitatofautiana na wewe,nimekaa nikajiuliza maswali mengi na kukosa majibu:
1.Kama huyu Mama alikuwa na miradhi iliyoandikwa na Mumewe nani alibadili miradhi hii??
2.Kwa sheria za Kiislamu zinasemaje??Je,kesi yake iliamriwa kwa sheria zipi??Je Kulingana na matakwa ya sheria za kiislamu yametimilika yote??
3.Miaka 10 alikuwa anahangaika kupata haki yake kwanini hakufanya alichofanya jana??
4.Je ni kweli Hukumu ziko mbili??
5.Hii ya madawa ya kulevya imeingiaje pale ilhali anadai Mirathi na si issue ya Madawa ya kulevya??.
6.Kama IGP,AG,RPC,Judge Mkuu,DPP na Waziri wa Sheria wote wanajua kesi hii ilikuwaje watu wote hawa wakashirikiana kutompa huyu Mama haki yake??Jamani kwa jinsi ninavyoujua utendaji kazi wa kupenda SIFA hili ilikuwaje lisishughulikiwe hata na Mkuu wa Wilaya au Mkuu wa Mkoa kabla halijafika jana uwanjani??

Shemeji yangu nimeona kama picha fulani hivi isiyo na sterling,maswali ni mengi kuliko majibu.Ngoja tuusubiri ukweli isisje ikawa tunapotezea ili Kaka yako aonekane ni yule Hakimu muovu aliyempa haki yake Mjane aliyemlilia kwa siku nenda rudi.

Shemeji in short na nusa harufu ya moshi wa BANGI.
 
Aliona rais ndo angemsikiliza, maana yake ni kwamba wateule wa rais na mahakama hazitoi haki kwa sababu ya kuangaliana usoni. Wapo wengi wenye malalamiko kama hayo na hawawezi kumuona rais au wanaona aibu kujitokeza mbele ya Camera za wanahabari lakini hiyo haiondoi kiu ya haki zao. Mifumo ya utoaji haki nchini ni mibovu, na rais alitakiwa amhoji yule mwanamke aseme matatizo aliyoyapata kufuatilia haki yake.
 
Mkuu huyo ndiye JPM masifa

1. Kama anajua mapungufu ya mahakama na jeshi la polisi mbona hatua muafaka hajazichukua ?

2. inakuwaje anazlitumia mahakama na jeshi la polisi hizo hizo kukandamiza haki?

3. Wakristo wana hadithi hiyo hiyo ni moja ya hekima za Mfalme Suleiman. Kwa tafakuri yangu yule mama masikini ndiye jasiri ana hekima busara kiasi cha kumshawishi Khalifa.

4. Mfumo uliozaa maovu hauna namna ya kujisafisha. Magu anafaidika na mfumo wakiovu; watawaliwa wote hatuwezi fika mbele yake kwa matatizo ya kimahakama na uonevu wa jeshi la polisi.

MAGU HASTAHILI CHEMBE YA KUSIFIWA.
 
paskali post zako kuanzia 2015 way back zilikua za ukweli sana lakini za kipindi hiki zimejaa unafiki na kujipendekeza badilika brother achana na huo upuuzi protect your integrity cause huyo unaejipendekeza kwake doesn't give a https://jamii.app/JFUserGuide about you kujipendekeza na unafiki sio tabia za kiume #no offense#don't get it twisted
 
paskali post zako kuanzia 2015 way back zilikua za ukweli sana lakini za kipindi hiki zimejaa unafiki na kujipendekeza badilika brother achana na huo upuuzi protect your integrity cause huyo unaejipendekeza kwake doesn't give a **** about you kujipendekeza na unafiki sio tabia za kiume #no offense#don't get it twisted
Mkuu Mkulungu Mkuyengo, mimi ni binadamu, na huma beings wote, are not static, they are dynamic, and hence they change with time, for the better or for the worse na mimi vivyo hivyo ninakwenda nikibadilika, au for the better, or for the worse!.

Kwa wanye uwezo wa kunisoma kijuu juu kama wewe, utaniona nimebadilika, hivyo you are very right kusema I have changed for the worse!. Lakini kwa wenye uwezo wa kusoma na kuzama deep in between the lines, na kubaini the motive behind, wanajua Paskali ni yule yule juzi, jana na leo, and has changed for the better!.

Tofauti yangu kubwa na members wengi humu jf, wengi wetu wamechagua upande, wakiamua kuponda wao ni kuponda tuu mwanzo mwisho, hata mtu afanye mazuri vipi wao wataponda tuu!. Mimi sina upande, nasimama kwenye kwenye ukweli na haki bin haki, kwenye mazuri napongeza, kwenye mabaya nakosoa, na kwenye maovu, nalaani!.

Paskali
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la simulizi ya Kayafa Mkuu wa Bhaghdad enzi za simulizi za Alfu Lela Ulela, Khalifa Harun El Rashid, lengo likiwa ni kuwahamasisha wana jukwaa kuwa kwenye mazuri tupongeze, kwenye mabaya tukosoe na kwenye maovu tulaani, hivyo linapokuja suala la haki bin haki zikiwemo haki za wanyonge, naombeni muungane nami kumpongeza sana, rais wetu Dr.John Pombe Joseph Magufuli kwa kuwa ni mtetezi wa kweli wa haki za wanyonge.

Kitendo alichokifanya jana rais Magufuli cha kumsikiliza yule mwanamama ndicho alichokifanya Kayafa Mkuu Khalifa Harun el Rashid kwa yule mwanamke mjane masikini, na kiukweli kitendo kile kimenigusa sana, angekuwa mwingine, angeachia yule mwanamama ashughulikiwe kikamilifu na vyombo vya dola na isingekuwa rais kumkomboa, hapo ambapo angelalia usiku wa jana, ni Mungu tuu pekee angejua kilichomkuta!, sijui hata kama angefika asubuhi maana hawa polisi wetu sometimes ni machoni tuu ndio kama watu lakini mioyoni mwao ni ma beast ya ajabu kabisa!.

Kilichofanyika jana kinatoa somo kubwa sana kwa wanawake wengine na wanyonge wanaoteswa kwa kukosa haki, jinsi yule mama alivyoonyesha ujasiri na ushujaa kudai haki mbele ya rais ni uthibitisho kuwa haki hailetwi kwenye kisahani cha chai, haki inadaiwa kwa nguvu zote, na ikibidi inapiganiwa, hata ukifikia mahali, unaweza kujikuta uko tayarri kuutoa uhai wako kupigania haki, watakaofaidika ni watoto wako na watoto wa watoto wako!. Hivyo linapikuja suala la kupiganbia haki, kutetea haki, hata sisi jf, tusiwe na mswalie Mtume na mtu yoyote mminyaji haki!.

Mnaweza kuuliza haki za wanyonge, sawa kweli ni mtetezi, sasa inawezekanaje mtu huyo huyo ni mtetezi wa haki za wanyonge kwa upande mmoja, lakini hapo hapo akawa ni mminyaji mkubwa wa haki za kisiasa?!, inawezekana, wale mnaowadhania hawa wanasiasa ni wanasiasa wa kweli, kumbe wameshtukiwa sio wanasiasa chochote, wala lolote bali ni wapiga dili tuu, ila wao ni wapiga dili tuu kwa mgongo wa siasa, if that is the case, then, kama mkuu ameamua kuwashughulikia wapiga dili wote, ni wapiga dili wote, hadi wapiga dili za kisiasa, hivyo ni halali kwa kuminywa kwa demokrasia, kwa sababu hata wapigania demokrasia nao usikute ni wapiga dili tuu, nao wameshtukiwa!.

Kwa upande wa rais Magufuli ameendelea kuthibitisha yeye ni mtu wa watu, he is a man of the people.

NB. Kwa pongezi hizi simaanishi kuwa sasa rais Magufuli ndio kawa malaika!. No, kama rais Magufuli ni dikiteta, pamoja na wema wake huu, bado ni dikiteta vile vile, ila ni dikiteta mzalendo.

Hongera sana kwa Rais wetu mpendwa, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, jana umeonyesha utu wa hali ya juu sana kumsikiliza yule mama na unastahili pongezi za dhati kutoka kwa wapenda haki wote.

Paskali
Rejea

Rais Magufuli ni Simple, Genuine & Down To Earth-He is Simply A Man of The People!

Magufuli Kama Nyerere: Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'unyi, Ni Kazi Tuu, Ila Pia sio Kama Nyerere!

Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!
Ng'wana wane Mayalla usibetweke na sarakasi za msukuma mwenzio, huyu jamaa hana la maana katika hili zaidi ya kutaka kujiongezea ratings. wewe ni broadcaster unajua nini umuhimu wa ratings katika television. Huyu ni mtu aliyewaambia wahaya kule Bukoba watafute njia kujijengea nyumba zao wakati ambao walitaka msaada kutoka serikalini (usisahau walichangiwa na ndugu zao watanzania na pesa yao ikapigwa na serikali inayozuia ma deal) . Huyu ni mtu aliyemwambia Mbunge na muwakilishi wa wana Bukoba mjini aliyemuomba rais awasaidie wahanga wa tetemeko kwa kuwapunguzia gharama za vifaa vya ujenzi (hapa Lwakatare alichokiomba ni serikali ku subsidise gharama za vifaa vya ujenzi) matokeo yake alikejeliwa. Halafu unaniaminisha kuwa huyu ni mtetea wanyonge labda wanyonge wa Chato. Mayalla ujue huyu jamaa amejaa misifa tu ni Mbowe peke yake anayemuweza huyu jamaa. Mbowe anamvika kilemba cha ukoka na kwa kutojielewa Magufuli anaingia king, ndiyo uzuri wa kuingia mjini mapema unavyomsaidia Mbowe. Magufuli ni chunusi mkubwa kwa hii nchi hana hata maana kabisa na wala hana hata mapenzi wa hili Taifa na watu wake.

Japo Bush alikuwa hamnazo lakini alijitahidi kuwasaidia wahanga wa Mississippi lakini huyu jamaa kwanza hakufika katika maeneo ya maafa na hatujui nini kilimzuia kufika hapo. Mafuriko ya marekani Obama aliacha kampeni na alienda kuungana na wahanga, Mafuriko ya England David Cameron na Prince Charles walienda kuungana na wahanga na kuwafariji walijeruhiwa. Tetemeko la Italy waziri mkuu wa Italy alifika sehemu ya tukio na hao wote waliwahakikishia waathirika kuwa serikali itawasaidia kujenga miundo mbinu na majengo yaliyoathirika na maafa. Hapa kwetu Rais kaenda baada ya hata watu waliokufa walianza kuoza na ujumbe aliokwenda nao ni acheni wafu wajizike wenyewe halafu leo unataka tumpongeze kwa huyu mama na nina imani kubwa aliwekwa pale kama sarakasi ama maigizo.

Pascal nilidhani wewe ni mtu ilye elimika ungeweza kutambua ukweli na utapeli wa huyu msukuma mwenzio. kama ninyi waandishi na ma Broadcaster mnahadaiwa kirahisi je sisi wengine ambao hatuna hizo fani itakuwaje????????

Mungu Ibariki Tanzania
 
Ng'wana wane Mayalla usibetweke na sarakasi za msukuma mwenzio, huyu jamaa hana la maana katika hili zaidi ya kutaka kujiongezea ratings. wewe ni broadcaster unajua nini umuhimu wa ratings katika television. Huyu ni mtu aliyewaambia wahaya kule Bukoba watafute njia kujijengea nyumba zao wakati ambao walitaka msaada kutoka serikalini (usisahau walichangiwa na ndugu zao watanzania na pesa yao ikapigwa na serikali inayozuia ma deal) . Huyu ni mtu aliyemwambia Mbunge na muwakilishi wa wana Bukoba mjini aliyemuomba rais awasaidie wahanga wa tetemeko kwa kuwapunguzia gharama za vifaa vya ujenzi (hapa Lwakatare alichokiomba ni serikali ku subsidise gharama za vifaa vya ujenzi) matokeo yake alikejeliwa. Halafu unaniaminisha kuwa huyu ni mtetea wanyonge labda wanyonge wa Chato. Mayalla ujue huyu jamaa amejaa misifa tu ni Mbowe peke yake anayemuweza huyu jamaa. Mbowe anamvika kilemba cha ukoka na kwa kutojielewa Magufuli anaingia king, ndiyo uzuri wa kuingia mjini mapema unavyomsaidia Mbowe. Magufuli ni chunusi mkubwa kwa hii nchi hana hata maana kabisa na wala hana hata mapenzi wa hili Taifa na watu wake.
Japo Bush alikuwa hamnazo lakini alijitahidi kuwasaidia wahanga wa Mississippi lakini huyu jamaa kwanza hakufika katika maeneo ya maafa na hatujui nini kilimzuia kufika hapo. Mafuriko ya marekani Obama aliacha kampeni na alienda kuungana na wahanga, Mafuriko ya England David Cameron na Prince Charles walienda kuungana na wahanga na kuwafariji walijeruhiwa. Tetemeko la Italy waziri mkuu wa Italy alifika sehemu ya tukio na hao wote waliwahakikishia waathirika kuwa serikali itawasaidia kujenga miundo mbinu na majengo yaliyoathirika na maafa. Hapa kwetu Rais kaenda baada ya hata watu waliokufa walianza kuoza na ujumbe aliokwenda nao ni acheni wafu wajizike wenyewe halafu leo unataka tumpongeze kwa huyu mama na nina imani kubwa aliwekwa pale kama sarakasi ama maigizo.
Pascal nilidhani wewe ni mtu ilye elimika ungeweza kutambua ukweli na utapeli wa huyu msukuma mwenzio. kama ninyi waandishi na ma Broadcaster mnahadaiwa kirahisi je sisi wengine ambao hatuna hizo fani itakuwaje????????
Mungu Ibariki Tanzania
 
Aliona rais ndo angemsikiliza, maana yake ni kwamba wateule wa rais na mahakama hazitoi haki kwa sababu ya kuangaliana usoni. Wapo wengi wenye malalamiko kama hayo na hawawezi kumuona rais au wanaona aibu kujitokeza mbele ya Camera za wanahabari lakini hiyo haiondoi kiu ya haki zao. Mifumo ya utoaji haki nchini ni mibovu, na rais alitakiwa amhoji yule mwanamke aseme matatizo aliyoyapata kufuatilia haki yake.

Binafsi siamini katika kutafuta suluhu ya matatizo kama hayo kwenye mikutano ya hadhara. Hii naifananisha ni ile mikutano ya Mh. Makonda akiwa ziarani DSM. Kwa maoni yangu kuomba majibu hadharani kama ilivyofanyika haiwezi kuleta suluhu ya mara moja na IGP alijitahidi sana kuchagua cha kusema na cha kuacha na maneno ya kutumia. Suala kama la yuele mama ni mtambuka. Linagusa maeneo maengi sana. Kuna cha kujifunza kutokea kwenye mifano kama ya handling ya issue ya Faru John. Haikuwa na haraka kuitisha press conference kuweka tuhuma wazi kabla ya uchunguzi wa umakini ziadi kabla ya viongozi kutoa matamko.
 
Pascal nakuomba jaribu kusoma mchango wa mawazo aliyoutoa Tetty.Tetty kaeleza vizuri sana na kaangalia mbali sana.Kwani watu wote hao Tetty aliyowataja kwa nyazifa zao lazima ujue kuna shida mahali.Usikute huyo mama ndiye anayetaka kudhulumu haki wenzake.Kwanza jiulize alipataje namba ya Mh Raisi na kumtumia Msg.Ameweza kuonana na AG na Waziri wa katiba na Sheria na kudai wameshindwa kumsaidia.Pascal naomba kabla hujafanya uchunguzi wa kina kuhusu jambo hili hukupaswa kuandika uliyoandika.Sikuzote nimekuwa naunga mkono habari unazoleta lakini kwaleo naomba nitofautiane nawe.
 
Kwa mtu aliyemsikiliza IGP kwenye hii issue alipata mashaka sana kuhusu huyu mama. Hii issue ilikuwa kwenye finder tips za Mangu maana yake aliifanyia kazi na ilifuatiliwa sana. Kwa hali ya kawaida ni ngumu sana watu wote waliotajwa ku -conspire against huyu mama tena kwa issue iliyotoka kwa mtu wa caliber na tabia za Mh. Rais. Mimi naamini IGP alitumia busara kuliongelea hilo katika mazingira hayo aliyolazimika kuliongelea tena bila kutarajia. Tusubiri maana yameshaanza kujitokeza mane maneno yanayoleta mashaka lakini tusubiri taarifa rasmi. Na nyie wenye hivi vi house vidogo vidogo muwe mnaacha will.
 
Binafsi siamini katika kutafuta suluhu ya matatizo kama hayo kwenye mikutano ya hadhara. Hii naifananisha ni ile mikutano ya Mh. Makonda akiwa ziarani DSM. Kwa maoni yangu kuomba majibu hadharani kama ilivyofanyika haiwezi kuleta suluhu ya mara moja na IGP alijitahidi sana kuchagua cha kusema na cha kuacha na maneno ya kutumia. Suala kama la yuele mama ni mtambuka. Linagusa maeneo maengi sana. Kuna cha kujifunza kutokea kwenye mifano kama ya handling ya issue ya Faru John. Haikuwa na haraka kuitisha press conference kuweka tuhuma wazi kabla ya uchunguzi wa umakini ziadi kabla ya viongozi kutoa matamko.

Msiwe na akili nzito. Magufuli kampatia mama nafasi ya kujieleza. Magufuli hakutosa maamuzi bali maelekezo kwa vyombo na ngazi husika kufuatilia suala hilo. Asingemsikiliza mmngemnanga wiki nzima humu.Kamsikiliza bado mnakosoa. Watu gani nyie?
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom