Kwenye Haki za Wanyonge, Magufuli ni Kama Khalifa Mkuu Harun El Rashid wa Alfu Lela Ulela!.

Pole sana Pascal naona huna upeo hata wa kufikiri kumfananisha Khalifa Harun Bin Rashid na Magufuli umekosea sana tena sana Khalifa Harun bin Rashid ni kati ya warithi wa Mtume wetu Muhammad (S.A.W) kwahivyo mtu ukipewa Cheo cha Ukhalifa manake una Maamuzi, Busara, Hekima na Peo za Mtume kama Ibrahim, Musa, Issa au Muhammad so pale Magufuli hakuhukumu chochote na ukitazama katika matendo yake na matamko yake yuko mbali na sifa za Khalifa Harun bin Rashid
 
Kilichofanyika jana kinatoa somo kubwa sana kwa wanawake wengine na wanyonge wanaoteswa kwa kukosa haki, jinsi yule mama alivyoonyesha ujasiri na ushujaa kudai haki mbele ya rais ni uthibitisho kuwa haki hailetwi kwenye kisahani cha chai, haki inadaiwa kwa nguvu zote, na ikibidi inapiganiwa, hata ukifikia mahali, unaweza kujikuta uko tayarri kuutoa uhai wako kupigania haki, watakaofaidika ni watoto wako na watoto wa watoto wako!. Hivyo linapikuja suala la kupiganbia haki, kutetea haki, hata sisi jf, tusiwe na mswalie Mtume na mtu yoyote mminyaji haki!.!
Ni vyema kujua undani wa stori yenyewe kwanza kabla ya kumuita huyo mama kuwa ni 'mnyonge'. Kuna habari nyingine zinazopingana na 'unyonge' huo, na zinaeleza kwamba huyo mama ni tapeli anayejifanya mke wa marehemu mmoja ili awe msimamizi wa mirathi. Nitaendelea kuwa kimya hadi nipate uhakika kama kweli huyo mama ni mnyonge au mnyongaji
 
Paskali ww ni msomi.Mm nahisi kwa tukio la huyu mama tusiwe wepesi wa kutoa suluhu kwamba kuna haki ananyimwa.Kote alikoanzia hawawezi kuwa na roho ngumu ya kupoteza haki.Vumilia tupate ukweli na nadhani ww mwenyewe unaweza rudi hapa na kututahadharisha kwamba si wote watoao machozi huwa ndo wafiwa.Tuachie mahakama zetu zifanye kazi.
Mkuu Lubamba nakubaliana na wewe, na nimeshangazwa kidogo na andishi na mwanasheria msomi Paskali Mayalla kumpa haki yule mama katika hatua hiyo kwa kumuita kuwa ni mnyonge na aliyenyimwa haki! Ukisikiliza vizuri alichoongea IGP jana kuhusiana na sakata la mama yule, inahitaji kuwa na subira! Hata hivyo, hoja ya Paskali bila shaka ililenga zaidi kuonyesha kwamba kilichofanyika ni kinampa "credit" JPM, lakini bado tunaweza kuhoji pia katika mazingira ya tukio la jana lililohusu "sheria na haki" ni nani miongoni mwa marais waliotangulia angeruhusu yule mwanamke akose "haki" ya kusikilizwa pale? Inawezekana, katika yote mawili-kwamba mwanamke yule mjane aliyekuwa katika ndoa ya mitaala kanyimwa haki yake, na JPM ni mtetezi wa wanyonge, Paskali ameshindwa kulenga shabaha!
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la simulizi ya Kayafa Mkuu wa Bhaghdad enzi za simulizi za Alfu Lela Ulela, Khalifa Harun El Rashid, lengo likiwa ni kuwahamasisha wana jukwaa kuwa kwenye mazuri tupongeze, kwenye mabaya tukosoe na kwenye maovu tulaani, hivyo linapokuja suala la haki bin haki zikiwemo haki za wanyonge, naombeni muungane nami kumpongeza sana, rais wetu Dr.John Pombe Joseph Magufuli kwa kuwa ni mtetezi wa kweli wa haki za wanyonge.

Kitendo alichokifanya jana rais Magufuli cha kumsikiliza yule mwanamama ndicho alichokifanya Kayafa Mkuu Khalifa Harun el Rashid kwa yule mwanamke mjane masikini, na kiukweli kitendo kile kimenigusa sana, angekuwa mwingine, angeachia yule mwanamama ashughulikiwe kikamilifu na vyombo vya dola na isingekuwa rais kumkomboa, hapo ambapo angelalia usiku wa jana, ni Mungu tuu pekee angejua kilichomkuta!, sijui hata kama angefika asubuhi maana hawa polisi wetu sometimes ni machoni tuu ndio kama watu lakini mioyoni mwao ni ma beast ya ajabu kabisa!.

Kilichofanyika jana kinatoa somo kubwa sana kwa wanawake wengine na wanyonge wanaoteswa kwa kukosa haki, jinsi yule mama alivyoonyesha ujasiri na ushujaa kudai haki mbele ya rais ni uthibitisho kuwa haki hailetwi kwenye kisahani cha chai, haki inadaiwa kwa nguvu zote, na ikibidi inapiganiwa, hata ukifikia mahali, unaweza kujikuta uko tayarri kuutoa uhai wako kupigania haki, watakaofaidika ni watoto wako na watoto wa watoto wako!. Hivyo linapikuja suala la kupiganbia haki, kutetea haki, hata sisi jf, tusiwe na mswalie Mtume na mtu yoyote mminyaji haki!.

Mnaweza kuuliza haki za wanyonge, sawa kweli ni mtetezi, sasa inawezekanaje mtu huyo huyo ni mtetezi wa haki za wanyonge kwa upande mmoja, lakini hapo hapo akawa ni mminyaji mkubwa wa haki za kisiasa?!, inawezekana, wale mnaowadhania hawa wanasiasa ni wanasiasa wa kweli, kumbe wameshtukiwa sio wanasiasa chochote, wala lolote bali ni wapiga dili tuu, ila wao ni wapiga dili tuu kwa mgongo wa siasa, if that is the case, then, kama mkuu ameamua kuwashughulikia wapiga dili wote, ni wapiga dili wote, hadi wapiga dili za kisiasa, hivyo ni halali kwa kuminywa kwa demokrasia, kwa sababu hata wapigania demokrasia nao usikute ni wapiga dili tuu, nao wameshtukiwa!.

Kwa upande wa rais Magufuli ameendelea kuthibitisha yeye ni mtu wa watu, he is a man of the people.

NB. Kwa pongezi hizi simaanishi kuwa sasa rais Magufuli ndio kawa malaika!. No, kama rais Magufuli ni dikiteta, pamoja na wema wake huu, bado ni dikiteta vile vile, ila ni dikiteta mzalendo.

Hongera sana kwa Rais wetu mpendwa, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, jana umeonyesha utu wa hali ya juu sana kumsikiliza yule mama na unastahili pongezi za dhati kutoka kwa wapenda haki wote.

Paskali
Rejea

Rais Magufuli ni Simple, Genuine & Down To Earth-He is Simply A Man of The People!

Magufuli Kama Nyerere: Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'unyi, Ni Kazi Tuu, Ila Pia sio Kama Nyerere!

Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!

1. Tunampongeza Rais kwa kumsikiliza huyo mjane na yote aliyoyasema juu yake. Inatia moyo, ila itampa pia wasiwasi mwingi maana baadhi ya wakereketwa wanaweza kumwambia 'anajitia kimbelembele ataona'. Najaribu kujiuliza tu kwamba aliwezaje kujua afike mahali pale na apewe mic na amweleze Rais yaliyompata! Namwomba Rais atoe rai kwa wote ambao haki zao zinapondwa ili wakipata nafasi kwenye matukio kama hilo la jana ili nao pia wawe waweze kutumia fursa kama hiyo ili Rais apate kujua kitu gani kinaendelea na taratibu mambo kama hayo ya uonevu au ucheleweshwaji wa haki yanaweza kupungua au kukoma.
2. Kitu kingine ambacho ningependa kusema, pamoja na kumpongeza Rais, ni "ujumbe" kuhusu 'mtu akikamatwa red-handed na pembe za tembo' hakuna haja ya kufanya uchunguzi wala kuahirisha kesi maana ushahidi upo wazi. Kama hili litatekelezwa (kama lile la kufungua matairi kwenye pikipiki zinazokutwa kwenye njia ya magari yaendayo kasi maana agizo la Rais limeanza kutekelezwa) wengi watakaokamatwa red-handed pia ni wanyonge anaowatetea. Mfano, mara nyingi watu wanabifu na majirani wenzao wanaoweza kuchongeana kwa vyombo vya dola na kuanza kuwindwa. Mtu x anaweza kutayarisha bangi (madawa ya kulevya), mifupa ya mtu mwenye albinism au kitu chochote cha wizi na kukiweka karibu na nyumba ya y, ndani ya compound yake au kuiingiza kupitia mlango au dirisha au ufa au namna yoyote anayojua yeye (achilia mbali kwenye mfuko au begi analopendelea kutembea nalo) na kama atatoa ripoti polisi na wakija kufanya search, sijui kama huyo y aliyefanyiwa hayo atasalimika maana naye itaonekana kwamba ushahidi uko wazi - atajinasuaje kama hivyo vitu vimekutwa kwake? Kwa hiyo, moja ya yale Rais aliyoyasema watu wengine wanaweza kuyatumia isivyo na badala ya kuwakamata tu wahalifu red-handed, itakuwa pia kuwakama watu wema red-handed. Na haya mambo si mageni katika maisha yetu ambapo tunashuhudia wakati mwingine 'the guilty are made innocent and the innocent are made guilty'.
3. Napenda maneno ya Judge Mwalusanya: anasema - our courts must not only be courts of law, but also courts of justice. Pia, kwenye rule of law anasema it should also mean the rule of justice. Na mara nyingi tunakumbana na matatizo katika maisha yetu kwa sababu haki haikutendeka au haijatendeka au haitatendeka kabisa. Na 'haki' ni msamiati mgeni kwa viongozi wengi. Sidhani kama nilishasikia wakisema watatenda haki au watasimamia haki. Badala yake mara nyingi tunawasikia viongozi wakisema watalinda amani kwa gharama zote. Nawaomba waweze pia "kulinda haki kwa gharama zote".
 
Bandiko hili japo ni la miaka miwili iliyopita lakini bado liko valid. Kuna kitu nitakisema hapa baada ya siku saba in relation to huu msamaha huu mpya wa rais Magufuli kuwasamehe wenye kesi za uhujumu wa uchumi na utakatishaji fedha haramu.

P
 
Bandiko hili japo ni la miaka miwili iliyopita lakini bado liko valid. Kuna kitu nitakisema hapa baada ya siku saba in relation to huu msamaha huu mpya wa rais Magufuli kuwasamehe wenye kesi za uhujumu wa uchumi na utakatishaji fedha haramu.

P
Kwa vile zimeongezwa siku saba, nitarejea hapa baada ya kukamilika kwa zoezi hili, ili rais Magufuli atende haki ya ukweli, lazima awe kama Kayafa Khalifa Mkuu Harun el Rashid.
P
 
Paskali ww ni msomi.Mm nahisi kwa tukio la huyu mama tusiwe wepesi wa kutoa suluhu kwamba kuna haki ananyimwa.Kote alikoanzia hawawezi kuwa na roho ngumu ya kupoteza haki.Vumilia tupate ukweli na nadhani ww mwenyewe unaweza rudi hapa na kututahadharisha kwamba si wote watoao machozi huwa ndo wafiwa.Tuachie mahakama zetu zifanye kazi.
Umenikumbusha yule mama wa Tanga...
 
Bandiko hili japo ni la miaka miwili iliyopita lakini bado liko valid. Kuna kitu nitakisema hapa baada ya siku saba in relation to huu msamaha huu mpya wa rais Magufuli kuwasamehe wenye kesi za uhujumu wa uchumi na utakatishaji fedha haramu.

P
Kwa vile zimeongezwa siku saba, nitarejea hapa baada ya kukamilika kwa zoezi hili, ili rais Magufuli atende haki ya ukweli, lazima awe kama Kayafa Khalifa Mkuu Harun el Rashid.
P
Kwa vile sasa zoezi limekamilika, leo ndio nakisema nilichikisema.
Katika wahujumu na watakatishaji fedha, kuna makundi matatu ya watu na aina tatu za wahujumu.
Tukianza na makundi ya wahujumu, kuna wahujumu wakubwa, matajiri wenye uwezo wa kulipa chochote. Kuna wahujumu wa kati ambao ni watu wa kawaida, na wahujumu wadogo, masikini wa kutupwa hata wakiandika barua za msamaha, hawana uwezo wa kulipa chochote.
Tukija makosa ya uhuhujumu ya kuombea msamaha
1. Wahujumu kweli na watakatishaji kweli pesa, hawa wataomba msamaha na pesa wanazo na watalipa pale pale watakuwa huru.
2. Wahujumu waliohujumu kidogo na kubambikiwa kesi kubwa, hawa pia wataandika barua na kulipa kulipa kidogo kidogo.
3. Waliobambikiwa kesi za uhujumu, kwenye kundi hili la waliobambikiwa, nako kuna makundi matatu yake.
1 Waliobambikiwa lakini ni matajiri, hawa wataandika barua na kukiri uhujumu ili tuu kuununua uhuru wao kwa gharama yoyote, hawa watalipishwa na watalipa ila kwa vile wamelazimika kukubali tuu ili wawe huru, fedha zao zina bad karma ya malipizi, Mungu tawalipia.
2. Kuna waliobambikiwa ni watu wa kawaida na wengine ni masikini, hawa pia wangetamani kuandika barua wakiri watoke na wengine watakuwa wameandika barua kukiri kwa kusisitiza kuwa wamesingiziwa, ili watoke, lakini pia watakiri kuwa wangekuwa na fedha pia wangelipa, hawa pia wanapaswa kuachiwa bila kulipa chochote.
3. Hawa ni watu wakweli, ambao wataamua kusimama na ukweli mpaka mwisho kuwa wao wamesingiziwa, sio wahujumu, hawataandika ba kukiri makosa ya kubambikiwa, au wakiandika sio kukiri bali kusisitiza wamezingiziwa, hawa ndio Mungu atasiimama nao.

Sasa kwa kuutumia uadilifu na busara kama za Khalifa Harun el Rashid, natoa wito kwa rais Magufuli atumie huruma yake na busara zake kuwasamehe kwa kumuelekeza DPP (japo DPP hatakiwi kuelekezwa, siki hixi DPP anaelekezeka!), kutumia powers zake za Nolle kwa kuwatendea haki kwa kuzifuta kesi zao.

Hivyo rais aombe kupewa majina ya wahusika wote wa kesi za uhujumu aangalie ni wangapi hawajakiri na hawajaandika barua, hao wote waachiwe watakuwa ni kweli wamesingiziwa.
Mungu mbariki rais Magufuli,
Mungu ibariki Tanzania.
P
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la simulizi ya Kayafa Mkuu wa Bhaghdad enzi za simulizi za Alfu Lela Ulela, Khalifa Harun El Rashid, lengo likiwa ni kuwahamasisha wana jukwaa kuwa kwenye mazuri tupongeze, kwenye mabaya tukosoe na kwenye maovu tulaani, hivyo linapokuja suala la haki bin haki zikiwemo haki za wanyonge, naombeni muungane nami kumpongeza kwa dhati, rais wetu Dr.John Pombe Joseph Magufuli kwa kuwa ni mtetezi wa kweli wa haki za wanyonge.
Naomba kabla sijakisema nilichokusudia, kwanza soma hii simulizi hapa chini

Baada ya simulizi hiyo, sasa shuhudia kitu kilichofanyika jana kwa huyu mwanamke mjane, halafu angalia rais Magufuli alifanya nini.

Kitendo alichokifanya jana rais Magufuli cha kumsikiliza yule mwanamke ndicho alichokifanya Kayafa Mkuu Khalifa Harun el Rashid kwa yule mwanamke mjane masikini, na kiukweli kitendo kile kimenigusa sana, angekuwa mwingine, angeachia yule mwanamke mjane ashughulikiwe kikamilifu na vyombo vya dola na isingekuwa rais kumkomboa, hapo ambapo angelalia usiku wa jana, ni Mungu tuu pekee ndiye angejua kilichomkuta!, sijui hata kama angefika asubuhi salama, maana hawa polisi wetu sometimes, ni machoni tuu ndio kama watu, lakini mioyoni mwao ni wanyama kabisa!, ma beast ya ajabu!.

Kilichofanyika jana kinatoa somo kubwa sana kwa wanawake wengine na wanyonge wanaoteswa kwa kukosa haki, jinsi yule mama alivyoonyesha ujasiri na ushujaa kudai haki mbele ya rais ni uthibitisho kuwa haki hailetwi kwenye kisahani cha chai, haki inadaiwa kwa nguvu zote, na ikibidi inapiganiwa, hata kuweza kukifikia mahali, unaweza kujikuta uko tayari kufa kwa kuutoa uhai wako kupigania haki, watakaofaidika ni watoto wako na watoto wa watoto wako!. Hivyo linapokuja suala la kupigania haki, kutetea haki, hata sisi jf, tusiwe na mswalie Mtume na mtu yoyote mminyaji haki, tupiganie haki zetu kwa nguvu zote!.

Mnaweza kujiuliza hivi kweli ni Magufuli huyu huyu dikiteta, sasa ndiye mlinzi wa haki za wanyonge?!, sasa inawezekanaje mtu huyo huyo ni mtetezi wa haki za wanyonge kwa upande mmoja, lakini hapo hapo akawa ni ndiye mminyaji mkubwa wa haki za kisiasa?!.

Usikute inawezekana, ameamua kuminya demokrasia na haki za kisiasa, kwa sababu, hao political players, mnaowadhania ni wanasiasa wa kweli, kumbe Magufuli amewashitukia kuwa sio wanasiasa chochote, wala lolote bali ni wapiga dili tuu za kisiasa, kwa mgongo wa siasa, if that is the case, then, kwa vile Magufuli ameamua kuwashughulikia wapiga dili wote, then, ni wapiga dili wote wanashughulikiwa, hadi wapiga dili za kisiasa!, hivyo kuhalalisha kuminywa kwa demokrasia, kuvunja katiba kwa kupiga marufuku mikutano ya kisiasa kwa sababu hao wanasiasa wote wa vyama vingine, kwake ni wapiga dili tuu, wanasiasa wa ukweli ni CCM tuu pekee!. Tumshukuru pia kwa hatua hii ya kuwashtukia wanasiasa wapiga dili za kisiasa waliokuwa wanawapamatumaini Watanzania kuwa kuna siku moja CCM itaondolewa madarakani, kumbe walikuwa wanatuingiza chaka!. Ukweli ni kuwa CCM, itatawala milele!. Ndicho chama pekee chenye hati miliki ya kutawala Tanzania, hivyo Magufuli analisimamia hili kuhakikisha CCM haisumbuliwi na haibughudhiwi!.

Kwa upande wa rais Magufuli ameendelea kuthibitisha kuwa, when it comes kwenye manyanyaso ya wanyonge, yeye ni mtu wa watu, he is simply, a man of the people. Kama akiendelea hivi na kisha Roho wa Mungu wa kweli, akamuingia na kuachana na udikiteta wake wa asili, ambao ni kama ushetani fulani, na akazirudisha haki zote za msingi zilizoainishwa kwenye katiba yetu, mnaweza kushangaa by 2025 akawa kama ndiye Mfalme Suleman wa Tanzania!, hivyo Watanzania tukapiga kelele za kubadili katiba Magufuli aendelee milele na milele mpaka pale Mungu atakapoona inatosha na kumuita kwake!.

NB. Kwa pongezi hizi simaanishi kuwa sasa rais Magufuli ndio ghafla kageuka kuwa malaika!. No, kama rais Magufuli ni dikiteta, pamoja na wema wake huu, bado ni dikiteta vile vile, ila ni dikiteta mzalendo mwenye huruma fulani kwa watu fulani, lakini ni katili kwa wengine wakiwemo wapiga dili!.

Hongera sana kwa Rais wetu mpendwa, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, jana umeonyesha utu wa hali ya juu sana kumsikiliza yule mama mjane, na unastahili pongezi za dhati kutoka kwa wapenda haki wote, tunakuomba ujue tuu kuna makumi kwa mamia na maelfu ya Watanzania masikini wa kutupwa ambao wamedhulumiwa haki zao, na hawana courage kama ya huyo mama kukufikia, wengine hawa hata access ya kusikilizwa na wasaidizi wako, kuna mamia wanaozea magerezani kwa kesi za kubambikiwa, kuna mamia ni mahabusu wakuozea magerezani kwa kisingizio upelelezi haujakamilika mfano mzuri ni ni yule wakili wa Arusha Medium Mwale, huu ni mwaka wa 7 yuko mahabusu kwa kosa ambalo adhabu yake ni faini na kufungo cha mwaka mmoja!.

Tunakuomba huruma yako kwa wanyonge wanaonyimwa haki zao, ielekeze kwa wasaidizi wako ili Watanzania wote watendewe haki na sio kusubiri hadi kilio kikufikie wewe. Angazia watuhumiwa wa kesi za uhujumu, fuatilia uone ni wangapi wanaozea mahabusu kwa miaka na miaka bila hata kesi kuanza kusikilizwa. Justice delayed ni justice denied.

Mungu ibariki Magufuli aendelee kuhakikisha hata masikini na wanyonge, wanatendewa haki.
Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
Rejea

Rais Magufuli ni Simple, Genuine & Down To Earth-He is Simply A Man of The People!

Magufuli Kama Nyerere: Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'unyi, Ni Kazi Tuu, Ila Pia sio Kama Nyerere!

Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!.

Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

kwa sasa utaimba mapambio ya kila namna, huna jinsi mkuu!
 
Mkuu Mkulungu Mkuyengo, mimi ni binadamu, na huma beings wote, are not static, they are dynamic, and hence they change with time, for the better or for the worse na mimi vivyo hivyo ninakwenda nikibadilika, au for the better, or for the worse!.

Kwa wanye uwezo wa kunisoma kijuu juu kama wewe, utaniona nimebadilika, hivyo you are very right kusema I have changed for the worse!. Lakini kwa wenye uwezo wa kusoma na kuzama deep in between the lines, na kubaini the motive behind, wanajua Paskali ni yule yule juzi, jana na leo, and has changed for the better!.

Tofauti yangu kubwa na members wengi humu jf, wengi wetu wamechagua upande, wakiamua kuponda wao ni kuponda tuu mwanzo mwisho, hata mtu afanye mazuri vipi wao wataponda tuu!. Mimi sina upande, nasimama kwenye kwenye ukweli na haki bin haki, kwenye mazuri napongeza, kwenye mabaya nakosoa, na kwenye maovu, nalaani!.

Paskali
si kweli kwamba unaweza ukasimama kwenye ukweli na haki bin haki only God can, wewe ukishakuwa corrupt unasomeka vizuri kabisa aisee!! Hata Li-pumba na Silaha wako kama wewe tu!
 
si kweli kwamba unaweza ukasimama kwenye ukweli na haki bin haki only God can, wewe ukishakuwa corrupt unasomeka vizuri kabisa aisee!! Hata Li-pumba na Silaha wako kama wewe tu!
No kuna kitu kinaitwa perspective vision, uoni na muona, kwanza kila mtu has the right of his/her own opinion, hivyo nayaheshimu mawazo yako kuwa mimi ni corrupt, Dr. Silaha na Prof. Lipumba nao wako kama mimi.

Tatizo kubwa la wengi ni kitu kinaitwa mind set, ukiisha amua kuamini jambo fulani utaamini ulichoamini au aminishwa no matter what. Ukiwa ndani ya box, mwisho wa vission yako ni kwenye kingo za box ulilomo, huwezi kuona nje ya box mpaka utoke nje. Dr. Slaa na Chadema wote waliokuwa ndani ya box, uwezo wao ni kingo tuu za box, waliotoka nje wakaona a different perspective wanaona vitu ambavyo ndani ya box hamuoni, ndio maana kwa Chadema walio ndani ya box nikawashauri hivi

Wenzenu waliochungulia nje ya box waliona picha tofauti kabisa na kuamua kufanya uamuzi sahihi.

Endelea kubakia ndani ya box ukiangalia kingo za box.
P
 
Wanabodi,

Hongera sana kwa Rais wetu mpendwa, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, jana umeonyesha utu wa hali ya juu sana kumsikiliza yule mama mjane, na unastahili pongezi za dhati kutoka kwa wapenda haki wote, tunakuomba ujue tuu kuna makumi kwa mamia na maelfu ya Watanzania masikini wa kutupwa ambao wamedhulumiwa haki zao, na hawana courage kama ya huyo mama kukufikia, wengine hawa hata access ya kusikilizwa na wasaidizi wako, kuna mamia wanaozea magerezani kwa kesi za kubambikiwa, kuna mamia ni mahabusu wakuozea magerezani kwa kisingizio upelelezi haujakamilika mfano mzuri ni ni yule wakili wa Arusha Medium Mwale, huu ni mwaka wa 7 yuko mahabusu kwa kosa ambalo adhabu yake ni faini na kufungo cha mwaka mmoja!.

Tunakuomba huruma yako kwa wanyonge wanaonyimwa haki zao, ielekeze kwa wasaidizi wako ili Watanzania wote watendewe haki na sio kusubiri hadi kilio kikufikie wewe. Angazia watuhumiwa wa kesi za uhujumu, fuatilia uone ni wangapi wanaozea mahabusu kwa miaka na miaka bila hata kesi kuanza kusikilizwa. Justice delayed ni justice denied.

Mungu ibariki Magufuli aendelee kuhakikisha hata masikini na wanyonge, wanatendewa haki.
Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
Wanabodi, mimi ni miongoni mwa wana jf, tuliandika mengi kumhusu rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, hivyo kipindi hiki cha maombolezo, napitia baadhi ya mabandiko kwa ajili ya kumuaga rasmi.

Japo umetangulia, lakini kauli zako, maono yako na kile ulichokiamini, kitabaki na sisi Milele.
Sisi tulikupenda, lakini Mungu amekupenda zaidi.
Bwana Alitoa, Bwana Ametwaa, Jina Lake Lihimidiwe!.
Raha ya Milele Umpe Ee Bwana, na Mwanga wa Milele, Umuangazie, Apumzike kwa Amani...Amina x3.
RIP Dr. John Pombe Joseph Magufuli
Buriani ya kuonana...
Paskali
Wanabodi, mimi ni miongoni mwa wana jf, tuliandika mengi kumhusu rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, hivyo kipindi hiki cha maombolezo, napitia baadhi ya mabandiko kwa ajili ya kumuaga rasmi.

Japo umetangulia, lakini kauli zako, maono yako na kile ulichokiamini, kitabaki na sisi Milele.
Sisi tulikupenda, lakini Mungu amekupenda zaidi.
Bwana Alitoa, Bwana Ametwaa, Jina Lake Lihimidiwe!.
Raha ya Milele Umpe Ee Bwana, na Mwanga wa Milele, Umuangazie, Apumzike kwa Amani...Amina x3.
RIP Dr. John Pombe Joseph Magufuli
Buriani ya kuonana...
Paskali
 
Back
Top Bottom