Kwenu wenye nafasi za kazi Serikalini au kwenye Mashirika Binafsi

Ndolezi

Senior Member
Oct 15, 2019
134
98
Mimi ni kijana wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 26, elimu yangu ni shahada ya maendeleo vijijini kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine.

Dhumuni la kuandika uzi huu ni kuomba nafasi ya kazi au Internship serikalini au kwenye mashirika binafsi, uzoefu wangu wa kazi ni kama ifuatavyo:-

  • Ufuatiliaji na utathmini wa miradi.
  • Kutoa elimu mbalimbali kama vile elimu ya afya ya uzazi, kilimo.
  • Udodosaji na ukusanyaji wa taarifa hasa mijadala ya makundi (Focus Group Discussion).
  • Utatuzi wa migogoro.
  • Kazi za field hasa maeneo ya vijijini, hapa nina uzoefu na uwezo mzuri wa kusafiri umbali mrefu pamoja na kukabiliana na changamoto zote za vijijini na kuweza kukamilisha kazi kwa ufanisi mkubwa.
  • Kuandika ripoti vizuri pamoja na kuiwasilisha.
  • Matumizi ya computer pamoja na packages zake kama vile Ms word, Excell, SPSS, internet etc.

Hizo ni baadhi ya kazi ninazo weza kuzifanya lakini pia ninaweza kufanya kazi nyingine nitakazopewa, kwa sasa ninapatikana Mbeya mjini Ila nipo tayari kusafiri mkoa wowote ndani ya Tanzania.

Wenu katika ujenzi wa taifa.

Ndolezi.
 
Mimi ni kijana wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 25, elimu yangu ni shahada ya maendeleo vijijini kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine...
Ungekua na uwezo mzuri wa kuandikia mirad ningekuona inbox..nina shida na mtu wa aina yako ila kina vigezo kidoogo
 
Najarubu kuuvaa uhusika, naona machungu!

Watu wanaripoti kazini wenye wajomba zao vigogo.
Kiuhalisia inaumiza sana mkuu kwa sisi tusio na 'connection', anyways kila mja na fungu lake nina imani ipo siku nitapata nafasi pia japo siku zinayoyoma umri unasogea mwaka wa pili sasa mtaani bila ajira. Kama una connection mkuu naomba unisaidie.
 
Wenzako wako kitaa tangu 2015 mpk leo bado ni bila bila we miwili tu unapaniki?

Yajayo yanafurahisha.
 
Kiuhalisia inaumiza sana mkuu kwa sisi tusio na 'connection', anyways kila mja na fungu lake nina imani ipo siku nitapata nafasi pia japo siku zinayoyoma umri unasogea mwaka wa pili sasa mtaani bila ajira. Kama una connection mkuu naomba unisaidie.
keep hope kaka maisha ni mapambano na ukiumbwa mwanaume sio kusimamisha tu hapana maan hata mbuzi dume anasimamisha umefanya uamuzi mgumu sana ambao wengne akina sie hatuna uwezo huo..big up mkuu
 
keep hope kaka maisha ni mapambano na ukiumbwa mwanaume sio kusimamisha tu hapana maan hata mbuzi dume anasimamisha umefanya uamuzi mgumu sana ambao wengne akina sie hatuna uwezo huo..big up mkuu
Ahsante sana mkuu kwa kunifariji nina imani siku ipo yaja,bado naendelea kutafuta.
 
anachosema ni yyte yule mwenye kazi sehemu husika huko sasa ukisema kaombe sua ameshayaona hayo na kuna uwezekano amejaribu lakini ameshindwa

tafakari kwanza kaka tusijibu tu ilimradi kufurahisha genge..tupende kuwa na genge la wasomi sio kujifurahisha tu
🙏
 
Ahsante mkuu, sijawa expert wa uandishi wa miradi bado najifunza.
Sasa mkuu utajifunza vipi kama unapewa kazi unasema bado najifunza? Unekua serious ungechukua kazi, piga kazi ukikwama unaomba ushauri kwa wenzako... ukikwama una google, ukikwama unaingia youtube..

Sasa wewe umeishia kusema bado najifunza.. sijui utajifunza mpaka lini!
 
Ahsante sana mkuu kwa kunikumbusha, nachukua huu ushauri na ninakuahidi kuufanyia kazi.
 
Mimi ni kijana wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 25, elimu yangu ni shahada ya maendeleo vijijini kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine.

Dhumuni la kuandika uzi huu ni kuomba nafasi ya kazi au Internship serikalini au kwenye mashirika binafsi, uzoefu wangu wa kazi ni kama ifuatavyo:-

- Ufuatiliaji na utathmini wa miradi.
- Kutoa elimu mbalimbali kama vile elimu ya afya ya uzazi.
- Udodosaji na ukusanyaji wa taarifa hasa mijadala ya makundi (Focus Group Discussion).
- Utatuzi wa migogoro.
- Kazi za field hasa maeneo ya vijijini, hapa nina uzoefu na uwezo mzuri wa kusafiri umbali mrefu pamoja na kukabiliana na changamoto zote za vijijini na kuweza kukamilisha kazi kwa ufanisi mkubwa.
- Kuandika ripoti vizuri pamoja na kuiwasilisha.
- Matumizi ya computer pamoja na packages zake kama vile Ms word, Excell, SPSS, internet etc.

Hizo ni baadhi ya kazi ninazo weza kuzifanya lakini pia ninaweza kufanya kazi nyingine nitakazopewa, kwa sasa napatikana wilaya ya Kasulu-Makere Ila nipo tayari kusafiri mkoa wowote ndani ya Tanzania.

Wenu katika ujenzi wa taifa.

Ndolezi.
Ukiweza nenda Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya Kasulu huwa kuna Mashirika mengi sana huwa wanasaidiana na Volunteers,Ukiweza unaweza kwenda Idara ya Kilimo hapo Kasulu kaulizie wanaweza kukuconnect na Wadau wa Maendeleo ukawa unapiga part time ukijenga uzoefu.Utakutana na WASUASO pale watakupa connection tu,you will thank me later.
 
Ahsante mkuu, sijawa expert wa uandishi wa miradi bado najifunza.
Dogo acha Ujinga wewe, unataka kazi na unakataa kazi? Wewe ni Graduate kweli?
Huwezi kuandika mradi kivipi? Huwezi hata kutafuta format mitandaoni, huwezi husisha mzoefu akakuandikia wewe ukawa kama Custodian?
Huhitaji uzoefu kufanya Jambo, Yaani unabadilikia humohumo kwenye Game kama Naco2Naco wanavyosema.
Lingine, Usione soo kujichanganya kitaa.. wakati unasubiri hiyo Ajira,
Kalime hata Mpunga, Muda unaenda mbio utajikuta unatoboa 30 hapo bado ramani hazisomeki,
Ukipata ajira ni heri usipopata pia uwe na plan B,
Being a Man means a lot of things, Pambana usikate tamaa. Anzisha hata biashara itakayokupa shilingi elfu 5 kwa Siku, hii itakupa relief ya Maisha.
All the best.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom