Kwenu wataalam wa lugha

Yusuph Salehe

Member
Nov 12, 2010
58
1
Kwa wataalam wa lugha naombeni msaada wenu. Katika sentensi kama hii HA-KU-CHEZ-A Je nini kazi ya "KU" zaidi ya kuonesha wakati uliopita?
 
Ku- inaweza kuwa na dhima kadhaa katika maneno lkn inategemea muktadha,
kutokana na mfano ulioutoa,kimofimu, dhima yake ni hiyo uloitaja tu.Ikitokea
katika muktadha tofauti ndo huweza kubeba dhima nyingine,
 
Je ikitokea katika muktadha mwingine hubeba dhima gani?
 
Kwa wataalam wa lugha naombeni msaada wenu. Katika sentensi kama hii HA-KU-CHEZ-A Je nini kazi ya "KU" zaidi ya kuonesha wakati uliopita?
Hainoyeshi wakati uliopita pekee maana pamoja na "HA" inaonyesha pia ya kwamba kazi haikutendeka maana ni kinyume cha "LI" inayoonesha pia wakati uliopita ("alicheza").
 
KU- HUWEZA KUWA NA DHIMA ZIFUATAZO:
1. Kudokeza wakati uliopita katika tendo linapokuwa katika ukanushi
mf: Hakucheza
2. Kudokeza mtendwa jambo (nafsi ya pili - wewe)
mf: amekupiga wewe
3. Kudokeza idadi (umoja)
mf: amekuona (umoja) wingi : wamuwaona
4. Huweza kuwa ni sehemu ya mzizi wa neno.
mf: kumbuka, kumbatia, kung'uta nk
5. Husaidia shina la kitenzi cha silabi moja
mf: i)kula, shina -kul-, mzizi -l- ; amekula,tutakula,amenilia,mlaji,sili,mlo,nk
ii)kufa, shina -kuf-, mzizi -f- ; amekufa,tutakufa,amenifia,hafi,kifo,nk
*vitenzi vingine vyenye mfumo huo ni kuja,kunya,kunywa,nk
*ktk mifano i na ii hapo juu tumeona -ku- imeweza kuonadoka kadiri
tulivyokuwa tunanyambua kwa vile husaidia shina -kul- na -kuf- na wala sio
sehemu ya mzizi wa maneno km ilivyo ktk 4 hapo juu.
6. Hudokeza upatanisho wa kisarufi.
mf i) Kuchakachua kumezidi
ii) Kule kuna kiza.
7. Huunda kitenzi jina
mf kusoma, kuimba, kulima
 
Nashukuru kwa orodha zuri. Ila tu maswali:
a) je na.2/3 si jambo lilelile (kutaja nafsi ya pili - umoja) ?
b) na. 4: je katika mifano hii si sehemu ya mzizi bali silabi ya kitenzi? (maana kama ingekuwa sehemu ya mzizi intaonekana pia katika mabadiliko ya kitenzi)?
 
Kwa wataalam wa lugha naombeni msaada wenu. Katika sentensi kama hii HA-KU-CHEZ-A Je nini kazi ya "KU" zaidi ya kuonesha wakati uliopita?
HA na KU ni neno moja HAKU, na linasimama kama kielezi cha kitendo ambacho kwenye sentensi hiyo ni CHEZA...!

Mf: Haku-Kimbia, Haku-imba, Haku-Kataza/zwa, Haku-muita, vile vile linaweza kutumika peke yake, kama vile umetoa shutuma fulani kwa mtoto naye akakujibu "Haku mimi sikuwepo"
 
Una hakika? "Siku - Kimbia" - kwa maana ile ile - ni silabi 2 pamoja lakini si neno?
 
Una hakika? "Siku - Kimbia" - kwa maana ile ile - ni silabi 2 pamoja lakini si neno?
Tunapoandika kwa kuanzia na Siku-*** na kumalizikia na kitendo, hapo inaonyesha umimi, yaani nafsi ya kwanza katika kupinga au kukataa jambo au kitendo...! Mf: Siku- iba, Siku- mkamata, Siku-mpiga, Siku-mdhurumu, Siku-muona, Siku-mtarajia n.k.
 
HA na KU ni neno moja HAKU, na linasimama kama kielezi cha kitendo ambacho kwenye sentensi hiyo ni CHEZA...!
Mf: Haku-Kimbia, Haku-imba, Haku-Kataza/zwa, Haku-muita, vile vile linaweza kutumika peke yake, kama vile umetoa shutuma fulani kwa mtoto naye akakujibu "Haku mimi sikuwepo"
Tunapoandika kwa kuanzia na Siku-*** na kumalizikia na kitendo, hapo inaonyesha umimi, yaani nafsi ya kwanza katika kupinga au kukataa jambo au kitendo...! Mf: Siku- iba, Siku- mkamata, Siku-mpiga, Siku-mdhurumu, Siku-muona, Siku-mtarajia n.k.
Hi yote sawa kabisa.
Ila tu ulisema ya kwamba unatazama "HAKU" kama neno. Hapo nimeuliza.

Nisipokosei Kiswahili kinatumia muundo wa silabu maalumu kuonyesha wakati wa tendo na nafsi ya mtendaji. Silabi maalumu zinaonyesha ukanusho na hizi ziko kwa silabi za wakati na pia za nafsi.

MFANO: ............ UKANUSHO
ni - li - fanya ......si - ku - fanya
u - li - fanya .......hu -ku - fanya
a - li - fanya .......ha - ku - fanya

ni-me-fanya .......si - ja - fanya
u-me-fanya ....... hu -ku - fanya
a-me-fanya ........ha - ku - fanya

Kwa hiyo nisingesema ile HAKU ni neno. Ni zile silabi mbili za ukanusho kwa nafsi ya pili (umoja) wakati uliopita.
 
Nashukuru kwa maoni
Naomba nichangie tena:
1. KIPALA
a) Maoni yako unaposema 2/3 zinataja jambo lile lile "kutaja nafsi ya pili -umoja" tayari umeshataja dhima mbili:
i) Nafsi ya pili
ii) Umoja (idadi)
Ndio maana nikazitenganisha hapo awali 2/3 katika maelezo yangu.

2. X-PASTER

" HA na KU ni neno moja HAKU" HAPANA

Swali alilouliza ndugu yetu kwa taaluma ya kisarufi ni la mofimu.
Ambapo mofimu ni neno au sehemu ndogo kabisa katika neno ambayo haiwezi kugawanyika tena yenye maana ya kisarufi,

HAKU katika neno KAKUCHEZA sio neno bali ni sehemu ya neno HAKUCHEZA
Pia HAKU inaweza kugawanyika tena kisarufi na kupata HA- na -KU- ambazo zote zina dhima zake. HA- Hudokeza ukanushi na KU- wakati uliopita.
 
HAKU linakuwa ni neno lenye kujitegemea pale mtu anapo tuumiwa kufanya jambo fulani na yeye hakakanusha kwa kutamka neno "HAKU sikuwa mimi"
 
Nashukuru sana X-Raster kwa mfano wako hapo juu ingawa unathibitisha maelezo yangu kuwa "HAKU" kutokana na muktadha wa neno la muuliza swali SIO NENO KAMILI bali ni mofimu mbili katka neno HA-KU-CHEZ-A ambazo hazipaswi kuwekwa pamoja na kuwa "HAKU" kama ulivyoeleza hapo awali pamoja na maelezo ya KIPALA!

Kwa muuliza swali naona uko kimya umeanzisha mada kisha umekaa pembeni hatujui kuwa umetosheka,umechoshwa,umekatishwa tamaa au vipi,naomba nikusikie!
 
HAKU linakuwa ni neno lenye kujitegemea pale mtu anapo tuumiwa kufanya jambo fulani na yeye hakakanusha kwa kutamka neno "HAKU sikuwa mimi"
Nashukuru kwa ujumbe huu lakini najitahidi sana kukumbuka kama nimemsikia mtu kusema vile. Sikumbuki.

Je kuna uwezekano ya kwamba ni neno lililo kawaida kieneo tu? Labda athira ya lugha jirani ya kikabila?
Maana yake ni nini?
Kuna uwezekano ni lahaja kwa "hakika"? Au ni kuongeza ukanusho?
 
Ku- kiambishi awali, cha mtenda, nafsi ya tatu umoja!!!! hakuna njeo hapo!!!
 
Nashukuru kwa ujumbe huu lakini najitahidi sana kukumbuka kama nimemsikia mtu kusema vile. Sikumbuki.

Je kuna uwezekano ya kwamba ni neno lililo kawaida kieneo tu? Labda athira ya lugha jirani ya kikabila?
Maana yake ni nini?
Kuna uwezekano ni lahaja kwa "hakika"? Au ni kuongeza ukanusho?
Huwa linatumika sana hasa na wasichana!
 
Nashukuruni sana jamani kwa majibu yenu mmenipa mwanga mzuri na nimeridhika na majibu yenu mliyoyatoa ahsanteni sanaaa
 
X-PASTER, naomba ufafanuzi wa maana ya hii sentensi "HAKU sikuwa mimi", hii HAKU ni jina la mtu au...? , kwa mimi ninayejua kiswahili cha mtaani na sio cha shuleni ningesema, "huyo sikuwa mimi" au "sio mimi", naomba unifahamishe hapa, sijawahi kusikia/kuona matumizi ya namna hii.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom