Kwenu wanaJF: Saint Anne ninawashukuru mno

Pole sana St.Anne.Mungu ni mwema aendelee kukutia nguvu kipindi hiki unachopitia.Mshukuru Mungu baba amewafikisha hapo walau mnajitambua.Mmeuonja upendo wake.Wengine wazazi wanafariki watoto wakiwa wadogo imagine unakuja kuoneshwa picha tu.Yote kwa yote amani ya Mungu itawale moyoni mwako.
 
Natumaini mnaendelea vizuri.

Nikiri msiba unauma jamani.
Yaani maumivu niliyonayo nashindwa namna ya kuyaelezea..
Nimempoteza mzazi wangu wakati ambao bado nilikuwa namuhitaji ,umri wangu bado ni mdogo kuweza kusimama bila baba.

Tumempumzisha tayari mzee wetu na amani ya moyo inaniambia amepumzika salama.
Ameondoka usiku wa kuamkia tar29/5/2021.
Taarifa ilinipa mshtuko mkali,hadi sasa mapigo yangu ya moyo hayaendi sawa.

Mwendo ameumaliza,nina imani kabisa kwamba nitakutana naye Mbinguni.

Baba alipoanza kuugua,nilipokuwa nikiingia katika maombi,kila nikiomba uponyaji,nafsi ilinisukuma sana kuomba naye toba na pumziko Zuri.
Nilikosa raha sana lakini Roho wa Mungu alikuwa ananisihi sana kulipokea hilo.

Amepumzika,

Baba yangu alikuwa baba mzuri na mtu wa watu,licha ya mapungufu madogo ambayo kila mtu ana yake.
Mwezi mmoja kabla hajaugua,alifanya usafi sana nyumbani(Nikiri mzee alikuwa smart sana hasa katika kuweka sawa mazingira ya nyumbani),akaacha ametengeneza bustani nzuri,akatuaga akatuambia anaenda kuhangaikia usafi wa mashamba..akiondoka atakaa muda mrefu bila kurudi.
Kumbe alikuwa anatuaga.

Aliwahi kusema kwamba mwanangu nitakuhudumia hadi pale utakapomaliza mambo yako ya shule.
Kweli, alilitimiza hilo, hadi alipokamilisha,akasema sasa mwanangu nimemaliza kazi yangu.

•Shukurani kwa Mungu kwa ajili ya baba:
Namshukuru Mungu kwa ajili yake, kwa neema aliyompa Miaka yote 64 akiwa duniani,
Alikuwa mtu wa kujishughulisha mno hasa kutafuta chakula shambani kwa ajili ya familia.
Sijui maisha yatakuwaje ila naamini Mungu atafanya njia.

Inaniwia ngumu kuamini kama kweli mzee hayupo ila ni kweli ameondoka.

Jambo hili ni zito sana kwangu.
Nipo Kwenye depression nzito,sielewi nitatoka vipi.
Anayeweza kunisaidia namna ya kuondokana na hili wimbi la mawazo naomba anisaidie.
Kiufupi akili yangu nahisi haipo sawa kabisa.

Mziwanda wa baba Mimi
Nyumbani ni pazito mno, usingizi hauji kabisa.

SHUKURANI ZANGU KWENU:
Kiukweli upendo mliouonyesha kwangu ndugu zangu ni upendo wa ajabu mno hadi nashangaa.
Natokwa na machozi ya huzuni lakini pia natokwa na machozi ya furaha kwa jinsi mlivyonionyesha upendo wa ajabu.

Namshukuru MUNGU sana kwa kunipa marafiki /ndugu wazuri sana namna hii ambao ni nyie.
Kuna watu mmekuwa wazazi wangu, dada zangu, kaka zangu..yaani nawaona ni zaidi ya ndugu kwangu.
Baba yangu hayupo ila ninaamini humu nitapata baba,nitapata wazazi,ninaamini mimi si yatima.

Baba yangu hayupo tena ila natiwa nguvu sana maana yupo Mungu ambaye ni baba yangu.
Amesema yeye ni baba wa yatima.

•Mungu awabariki wote ambao kwa namna moja ama nyingine,mmekuwa karibu na mimi kwa hali zote kunitia nguvu,kuniombea,kunifariji,kuniliwaza na kutoa michango yenu ya mali(rambirambi) kwangu.

Yaani sina namna nzuri ya kushukuru zaidi ya kusema Asante.

•Napeleka shukrani zangu kwa dada yangu Heaven Sent.
Mungu akubariki sana dada yangu Heaven Sent.
Umefanyika kuwa faraja kwangu.
Nilipopata msiba,mtu kwa kwanza kumuambia alikuwa ni huyu dada.
Amani ya moyo ilinituma nimwambie yeye.
Ni dada ambaye kwa kweli nikimuona namtukuza Mungu maana ananitia moyo mno.
Sina namna nzuri ya kumuelezea vile ninavyomuona ila itoshe kusema ni dada ambaye Mungu amenipa.

•Mungu akubariki kaka Mshana Jr kwa moyo wako wa upendo na kujali.

•Mungu akubariki rafiki yangu Karma ..nimefurahi kukuona na ninaona sipo mwenyewe,,nina rafiki anayejali.

•Mungu awabariki wote walionitia moyo kwa namna mbalimbali.
Kuna walionitafuta PM,kuna walionitafuta kwa namba yangu ya simu,Kuna walionitia moyo hapa jukwaani..Kila nikisoma comments zenu natiwa moyo mno kwa faraja ninayopata.
Natamani nitaje mmojammoja ila naona nitakesha ninataja.

•Nakosa namna nzuri ya kuwashukuru,itoshe kusema Mungu na awabariki mno.

Ninaleta shukrani zangu hizi kwenu..ninaomba mzipokee.

Pia soma: TANZIA - MwanaJF Saint Anne, amefiwa na baba yake mzazi leo
Pole sana Saint Anne Mungu akutie nguvu

Ruhusu nafsi yako iamini kwamba Baba haupo nae tena, iruhusu pia nafsi yako iamini kwamba maisha lazima yaendelee baada ya msiba, iruhusu pia nafsi yako iamini kwamba Sote tupo njia moja, baba ametutangulia na tutafuata, ukiweza kujinasua kwenye hayo basi hiyo depression itaondoka automatically, jipe muda najua sio rahisi lakini this too shall pass

Naamini wewe ni Mkristo, sisi wakristo tunaamini kuishi ni kristo na Kufa ni faida, hili neno hata kwenye Biblia linaandikwa, endelea kumuombea baba na kuyaenzi mema aliyokuachia ili aendelee kupumzika kwa amani

Mshukuru Mungu na usonge mbele, Mungu akuponye majeraha na maumivu yote uliyoyapitia kwa kumpoteza baba, you still have 10000 reasons to live.
 
Natumaini mnaendelea vizuri.

Nikiri msiba unauma jamani.
Yaani maumivu niliyonayo nashindwa namna ya kuyaelezea..
Nimempoteza mzazi wangu wakati ambao bado nilikuwa namuhitaji ,umri wangu bado ni mdogo kuweza kusimama bila baba.

Tumempumzisha tayari mzee wetu na amani ya moyo inaniambia amepumzika salama.
Ameondoka usiku wa kuamkia tar29/5/2021.
Taarifa ilinipa mshtuko mkali,hadi sasa mapigo yangu ya moyo hayaendi sawa.

Mwendo ameumaliza,nina imani kabisa kwamba nitakutana naye Mbinguni.

Baba alipoanza kuugua,nilipokuwa nikiingia katika maombi,kila nikiomba uponyaji,nafsi ilinisukuma sana kuomba naye toba na pumziko Zuri.
Nilikosa raha sana lakini Roho wa Mungu alikuwa ananisihi sana kulipokea hilo.

Amepumzika,

Baba yangu alikuwa baba mzuri na mtu wa watu,licha ya mapungufu madogo ambayo kila mtu ana yake.
Mwezi mmoja kabla hajaugua,alifanya usafi sana nyumbani(Nikiri mzee alikuwa smart sana hasa katika kuweka sawa mazingira ya nyumbani),akaacha ametengeneza bustani nzuri,akatuaga akatuambia anaenda kuhangaikia usafi wa mashamba..akiondoka atakaa muda mrefu bila kurudi.
Kumbe alikuwa anatuaga.

Aliwahi kusema kwamba mwanangu nitakuhudumia hadi pale utakapomaliza mambo yako ya shule.
Kweli, alilitimiza hilo, hadi alipokamilisha,akasema sasa mwanangu nimemaliza kazi yangu.

•Shukurani kwa Mungu kwa ajili ya baba:
Namshukuru Mungu kwa ajili yake, kwa neema aliyompa Miaka yote 64 akiwa duniani,
Alikuwa mtu wa kujishughulisha mno hasa kutafuta chakula shambani kwa ajili ya familia.
Sijui maisha yatakuwaje ila naamini Mungu atafanya njia.

Inaniwia ngumu kuamini kama kweli mzee hayupo ila ni kweli ameondoka.

Jambo hili ni zito sana kwangu.
Nipo Kwenye depression nzito,sielewi nitatoka vipi.
Anayeweza kunisaidia namna ya kuondokana na hili wimbi la mawazo naomba anisaidie.
Kiufupi akili yangu nahisi haipo sawa kabisa.

Mziwanda wa baba Mimi
Nyumbani ni pazito mno, usingizi hauji kabisa.

SHUKURANI ZANGU KWENU:
Kiukweli upendo mliouonyesha kwangu ndugu zangu ni upendo wa ajabu mno hadi nashangaa.
Natokwa na machozi ya huzuni lakini pia natokwa na machozi ya furaha kwa jinsi mlivyonionyesha upendo wa ajabu.

Namshukuru MUNGU sana kwa kunipa marafiki /ndugu wazuri sana namna hii ambao ni nyie.
Kuna watu mmekuwa wazazi wangu, dada zangu, kaka zangu..yaani nawaona ni zaidi ya ndugu kwangu.
Baba yangu hayupo ila ninaamini humu nitapata baba,nitapata wazazi,ninaamini mimi si yatima.

Baba yangu hayupo tena ila natiwa nguvu sana maana yupo Mungu ambaye ni baba yangu.
Amesema yeye ni baba wa yatima.

•Mungu awabariki wote ambao kwa namna moja ama nyingine,mmekuwa karibu na mimi kwa hali zote kunitia nguvu,kuniombea,kunifariji,kuniliwaza na kutoa michango yenu ya mali(rambirambi) kwangu.

Yaani sina namna nzuri ya kushukuru zaidi ya kusema Asante.

•Napeleka shukrani zangu kwa dada yangu Heaven Sent.
Mungu akubariki sana dada yangu Heaven Sent.
Umefanyika kuwa faraja kwangu.
Nilipopata msiba,mtu kwa kwanza kumuambia alikuwa ni huyu dada.
Amani ya moyo ilinituma nimwambie yeye.
Ni dada ambaye kwa kweli nikimuona namtukuza Mungu maana ananitia moyo mno.
Sina namna nzuri ya kumuelezea vile ninavyomuona ila itoshe kusema ni dada ambaye Mungu amenipa.

•Mungu akubariki kaka Mshana Jr kwa moyo wako wa upendo na kujali.

•Mungu akubariki rafiki yangu Karma ..nimefurahi kukuona na ninaona sipo mwenyewe,,nina rafiki anayejali.

•Mungu awabariki wote walionitia moyo kwa namna mbalimbali.
Kuna walionitafuta PM,kuna walionitafuta kwa namba yangu ya simu,Kuna walionitia moyo hapa jukwaani..Kila nikisoma comments zenu natiwa moyo mno kwa faraja ninayopata.
Natamani nitaje mmojammoja ila naona nitakesha ninataja.

•Nakosa namna nzuri ya kuwashukuru,itoshe kusema Mungu na awabariki mno.

Ninaleta shukrani zangu hizi kwenu..ninaomba mzipokee.

Pia soma: TANZIA - MwanaJF Saint Anne, amefiwa na baba yake mzazi leo
MUNGU aendelee kukutia nguvu Sis na familia nzima, May his Gentle Soul keep resting in Eternal peace
 
Pole sana saint Anne

Baba amepumzika, Mungu akupe moyo wa kukubali na amani

Nimesoma hii post nikaona una mengi mazuri yanayokuumiza kwa kumkosa, ila una mengi zaidi ya kumshukuru Mungu kwaajili ya uhai wake kwani amekua baba bora sana

Ametenda mema, ametenda yaliyompasa, amemaliza kazi na ameenda kupumzika kwa Mungu wetu

Lala salama baba saint Anne 🙏
 
Nilikaa siku nzima,
Japo nimuone baba,basi hata aseme neno,ila haikuwezekana.
Bado nahisi ni ndoto,nilimwita lakini hakunisikia tena
Jamani acheni kabisa

Sijawahi kulia maishani kama ninavyolia SasaView attachment 1811738
Dada ukiendelea hivyo utajitesa na mwisho utamkufuru Mwenyezi MUNGU shida uliyo nayo ni ya akili kukubali baba hayupo tena chakufanya endelea mbele yawezekana una deni hukutimiza ila you still have time,mweke baba katika sala Fanya yote mazuri aliyokufundisha ndio njia sahihi yakuendelea kuishi nae katika maisha mazuri yake yapo endelea kuyaenzi utamwona baba yupo kila wakati,biblia unasema kila jambo na wakati wake kuna wakati wakulia na wakucheka.....ruhusu akili yako kukubali kazi ya MUNGU kama una jambo unaweza kwenda katika mahali alipopumzika na ukanena nae kwa imani na ukapata suluhu,mwache baba apumzike kwa amani usijifunge na manung'uniko,amani iwe juu yako na familia nzima
 
Kwakweli hiki ni kipindi kigumu sana kwako, tuliopitia huko tunaweza elewa ni namna gani unahisi my dear, nikupe pole kwa mara nyingine

Lakini pamoja na yote tunakuombea Mungu akushike mkono uvuke salama katika pito hili gumu kwako

Na zaidi ya yote muda ni uponyaji mwingine Mungu aliyoweka kwajili ya kutufuta machozi na kutusaidia kusonga mbele

Hivyo my dear kua imara huku ukimtegemea Mungu nae atakuimarisha zaidi na zaidi. Baba ameumaliza mwendo kazi kwetu tuliobakia tujipange tujue nasi tutaumalizaje huu mwendo kila mmoja kwa wakati wake
 
Back
Top Bottom