Ndugu waheshimiwa Katambi na Kunambi kwa heshima kubwa naomba niwashauri jambo moja. Wengi wanaweza kuliona halina maana lakini naamini mkilitekeleza hili itakuwa ni heshima kubwa kwa mh. Rais wetu JPM.
USHAURI:Fanyeni maamuzi ya kufunga ndoa na kufanya harusi kwa wakati mmoja na sehemu moja.(yaani KWA PAMOJA).
Sababu za kuwashauri hili ni kama ifuatavyo
1: Heshima kwa mheshimiwa Rais wetu JPM. Heshima aliyowapa mh Rais ya kuwaomba hadharani muoe ni kubwa sana hivyo namna pekee ya kuonyesha heshima na utii kwa mh Rais ni kuoa tena kwa pamoja.
2: Sababu ya pili ni muhimu pia japo haina uhakika. Mkimualika mheshimiwa Rais kwenye harusi yenu naamini ataichukulia kwa uzito wake na naamini ataweza kuhudhulia harusi yenu. Itakuwa historia nzuri na kubwa sana kwenu na familia zenu kama harusi yenu itauzuliwa na Rais wa nchi. Ni mara chache sana hili hutokea.
3:Sababu ya tatu ni kuwa mtamthibitishia mh Rais kuwa mnafanya kazi ya kuleta maendeleo Dodoma kwa ushirikiano na upendo mkubwa. Ni juzi tu mh Rais katengua viongozi watatu wa jiji la Arusha kwa sababu zinazosemekana kuwa ni kutoshirikiana na kutoelewana katika utendaji kazi wao. Hivyo mtakuwa mmeonyesha mfano mzuri wa ushirikiano hata katika mambo yenu binafsi.
Mwisho kabisa naomba msisahau kunialika,itakuwa heshima kubwa sana kwangu.
Ahsanteni.