Kwenu Waandishi wa Habari na Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania...

Duuh!Nimalizie kiroba changu tu maana waandishi wa bongo walivyo na njaa kali,kesho sito shangaa wakisema "cdm wahusishwa na kifo"!


Hapo sasa ndipo utacheka ufe, na unakuta ni mmoja tu kapewa hela lakini anawageuza akili NewsRoom nzima
 
Kifo hiki cha kusikitisha kimeigusa Chanel Ten ambayo kwa mtazamo wangu huitizama CDM kama wafanya vurugu wa nchi hii. Sasa kwa hili mtakuwa mmepata akili na kuielewa CCM Police na maonevu yake. Sikuwahi kuona CDM wakifanya fujo hata siku moja, siku zote nashuhudia polisi wakifanya fujo kwa jina la kuzuia fujo ambazo wakati huo huwa hazipo.

Channel Ten sasa muache kujikomba kwa serikali, haya yanaweza kumkuta hata Fred Mwanjala na yule mjahidina mwenzake anayependa kujipendekeza kwa serikali.

Tupinge mauaji haya kwa kila hali. Polisi watulinde na si kutuua


Tusubirie "General On Monday"
 
Hata gazeti la Uhuru ni chombo cha habari. Usishangae likaibuka na kichwa cha habari "Mwandishi awafanyia vurugu askari" au "CHADEMA wamuua mwandishi wa habari" !!

Sijui kwa nini njaa ilichagua kukaa tumboni!

hawajagusia kabisa habari iyo leo
 
Juzi niliweka posti nikilaumu wanahabari kuwa kama nyumbu, hawajali mwenzao anaporaruriwa na simba. Nilikuwa naongelea MwanaHalisi. Siku hizi hakuna kelele kutoka wanahabari kuhusu gazeti hilo.

Sasa mwenzenu kauawa na bado utakuta kuna wanahabari watakaokuwa upande wa poliCCM.

Hakika mpaka muishe ndiyo mjue kuwa shida ya mtu yeyote inawahusu wanahabari pia.
 
I am really really sad for what is happening in my country Tanzania!! God please help this country! Remove this curse from us. Why are our brethren being killed? What have we done to offend you? Heal us Oh Lord!! Stop these killings of innocent people on the pretext of politics.
 
Usiku mzima nimeangalia picha ya mwandishi aliyeuliwa na police, nikakumbuka mlolongo wa mauji ya police maeneo mbalimbali ya nchi hii tena ya watu wasio na hatia. Jf tumekuwa mstari wa mbele kulaani maovu yote lakini bado sauti na hoja zetu zimeishia hapa jamvini. Hoja yangu wakati umefika sasa tujitokeze hadharani kulaani haya kwani mawazo hoja zetu zinahitajika sana kwa WTZ wenzetu hasa walio wasio na huduma ya internet, tufanye maandamano au tufanye mdaho huru ambao watu wengi zaidi wayasikia mawazo yetu. Mwisho wanauliwa ni ndugu na marafiki zetu kama tuendelea kujadili bila kuchukua hatua tutaendelea kuuliwa kama inavyotokea kule SYRIA
 
you are totally right on what you have just said kwa kweli kuna picha hapa inaosha mtutu umeelekezwa tumboni kwa marehemu Daudi View attachment 63613yaani ukizoom vizuri utaona marehemu mkono mmoja umemshika askari kuna askari amemuwekea mtutu tumboni
View attachment 63615 ona huyo askari anavyoshangaa baada ya tkio kutokea na hiyo ni gari ya rpc

asante sn mkuu kwa kuliweka wazi hili tukio kupitia picha, kwa sababu wameshaanza propaganda zao ooh marehem ameuawa kwa bom la machozi, ila safari hii ukweli lazima udhihirike na wahusika wachukuliwe hatua
 
Ndiyo wangoje kimbunga kutoka vyombo vya habari.

Bila shaka uysiku huu kuna harakati nyingi kati ya RPC Iringa, IGP Mwema, Dr Nchimbi, RC Iringa na DC Mufindi katika kupata msimamo mmoja kuhusu tungo zitakazotolewa na Polisi kesho kuhusu kuawa kwa mwandishi wa habari.

Nawaza tu sijui watakuja na maelezo gani yatakayoweza kukubalika na magazeti yakaandika positive headlines kwa polisi. Hata kama watashikilia lile lile la siku zote -- la 'hawakutii amri" maelezo ambayo yanaanza kuchosha masikioni, yatapinduliwa na wahariri. polisi wamechokoza nyuki kwa vyombo vya habari.

Aah wapi! Nyuki alikuwa ni Mwanahalisi na kwa mbali Raia Mwema. Hawa wengine ni nzi tu hawana lolote.
 
Ndiyo wangoje kimbunga kutoka vyombo vya habari.

Bila shaka uysiku huu kuna harakati nyingi kati ya RPC Iringa, IGP Mwema, Dr Nchimbi, RC Iringa na DC Mufindi katika kupata msimamo mmoja kuhusu tungo zitakazotolewa na Polisi kesho kuhusu kuawa kwa mwandishi wa habari.

Nawaza tu sijui watakuja na maelezo gani yatakayoweza kukubalika na magazeti yakaandika positive headlines kwa polisi. Hata kama watashikilia lile lile la siku zote -- la 'hawakutii amri" maelezo ambayo yanaanza kuchosha masikioni, yatapinduliwa na wahariri. polisi wamechokoza nyuki kwa vyombo vya habari.

tayar wameshasema mwangosi hajauliwa na polisi,nimesikia kwenye uchambuz wa magazet ya leo asbuhi MAGIC Fm,,,,kauli hiyo imetolewa na msemaji wa polisi
 
Mpaka 2015 kwa spidi hii watakua washatuua wote sasa. Tumekwisha.
ndugu ! Huku jamvini kuna watu wenye ujuzi mbali mbali tujaribu kujilinda kabla hatumaliza na kudai tumendondokewa na kitu kizito
 
Waandishi wa habari ZINDUKENI, KUMBUKENI UKWELI, ANDIKENI UKWELI. Marehemu Mwangosi alikuwa ni jasiri sana, alikuwa mkweli na alisimamia ukweli.
 
Waandishi nakumbuka mlipogomea habari za wizara ya mbambo ya ndani enzi za OMARI MAPURI je leo bado mnazo nguvu zile kama ni kweli basi fanyeni.kwani waandishi wengine duniani tayari hii habari wanayo mkononi, msitufanye baadae tusome habari kupitia the citizen la UK, au CNN, au mengineyo_ONYESHENI UBAVU WENU KAMA M4C wanavyofanya.
 
Tunahitaji wasomi jeshi la polisi, watu watakaofanya maamuzi kwa busara na kwa kuzingatia sheria na haki za msingi za watu.
Sio maroboti ambayo yanaendeshwa kwa rimoti. Ni ajabu sana wanawakandamiza wananchi ambao wanazinduka, na kimsingi ambao wanataka mageuzi kwa njia ya amani, tena mageuzi kwenye mfumo ambao utawaneemesha kwanza askari na wafanyakazi wengine kabla hata ya hao wanayoyapigania.
Mnamuua mtu ambaye yuko pale kuufahamisha umma kinachojiri, tena kwa nia njema kabisa...

Nyie askari wa levo ya chini, ndo maana maisha yenu ni magumu na ya aibu, kwa sababu mnapuuzika Labda kuliko kada nyingine yeyote. Watu wanaowapa order hata hawana habari na kilichoko field, wao nia yao ni kukandamiza mabadiliko yoyote, maana wanajua yatawanyima usingizi, Hasa pale ambapo yatawazindua hata nyinyi.

Hiyo ni kazi kama zilivyo nyingine, busara ina nafasi yake pia. Sio kutumia maguvu tu, akili ndio silaha muhimu kuliko zote.

Mtahukumiwa na kizazi hiki hiki. Manachokitengeneza, hamta kimudu, mtaishia kujiunga.

Unatoa roho ya mwananchi mwenzio, halafu unaenda kulala kwenye mabati. Sio ushujaa hata kidogo.

Mnaudhi mamilioni ya watanzania, na mnazidi kupuuzika.
 
Wana jamvi nimesikitishwa na kitendo ambacho kimefanywa na ITV jana katika taarifa ya habari ya saa mbili usiku! inasikitisha pale ambapo mass media kama hiyo inapofungwa mdomo kwa masilahi ya watu fulani. kwa aliyefuatilia vipindi vya chombo hicho siku ya jana, ITV katikta habari zao za saa majira ya saa kumi na moja walirusha habari kwa mhutasari kuhusu tukio la 'mwandishi Mwangosi' kuuwawa, tulitegemea ktk taarifa yao ya saa mbili usiku wangetuleta habari japo kwa ufafanuzi zaidi, cha ajabu hata kugusia tu hawakuthubutu! licha ya kuonyesha police wakiwarushia mabomu na kuwapiga virungu wafuasi wa chadema.
Kichekesho zaidi ni pale ambapo msomaji wa taarifa wa jana alionyesha uso wa kupigwa mkwara na kukubali kuficha hiyo habari, hali ambayo ilipelekea mpaka akasahau jina lake wakati anajitambulisha! hata kipindi alichokuwa ana preasant alisahau.

My take. kuuwawa kwa mwandishi wa habari(TV preasanter) na ITV kuchakachua hiyo habari ni weledi wa vyombo hivi? maoni yako ni mhimu sana ktkt hili.
 
lets be fair .... je TV nyingi ziliripoti vipi hili tukio .... mfano TBC, STAR TV, CLOUDS, MLIMANI,?
 
Back
Top Bottom