Kwenu Waandishi wa Habari na Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwenu Waandishi wa Habari na Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Puppy, Sep 2, 2012.

 1. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,276
  Likes Received: 662
  Trophy Points: 280
  Kwanza kwa Masikitiko makubwa natoa salamu zangu za Rambirambi kwa familia ya Marehemu Bwanaa Daudi Mwangosi, Channel Ten, Waandishi Wa Habari na Wapenda maendeleo wote. Mungu aipumzishe roho ya marehem mahali pema peponi.

  Naanza kwa kuwaambia wanataaluma ya habari, Ni Heri umfadhili Punda atakubebea mizigo kuliko kufadhili fisadi.

  Ni katika matukio mengi tu toka napopata akili ya kujua jema na baya waandishi mmekuwa mkilalamikiwa kupindisha ukweli au kuuficha kabisa. Na hilo nimelidhihirisha mwenyewe katika baadhi ya matukio niliyoyashuhudia LIVE tukioni. Kama lile Tarehe 5 Januari 2011 Arusha. (Sitorudia maelezo yake, asante to JF ukweli ulifahamika).

  Hao mlokuwa mkiwasaidia either sababu

  1. Mnapewa rushwa
  2. Mnamlinda mwajiri wenu
  3. Mnajipendekeza kwa mwajiri
  Etc,
  sasa wameanza kuwafanyia nyie yale walotufanyia na mkawasaidia kuyaficha.

  "Bomu la Machozi", "kitu kizito" au "flying object" sasa limelenga na kumuua hapo hapo kipenzi chetu mwaandishi mwenzenu ndugu Daudi Mwangosi (R.I.P), kaa ukijua kwa ishara hiyo lolote lawezekana. Maana wanajua ninyi hamna guts za kufanya uchunguzi wala kuhoji, so wataweza ku-claim chochote kile apendacho kusema ndio kiliua au si ajabu hata ku-pin hii kesi kwa mmoja wenu.

  Nguvu mlio nayo ni kubwa mpaka mkaitwa the "4th Estate" nyuma ya Executive(1st Estate),
  Legislature (2nd estate) na Judiciary (3rd estate), mbele ya
  Organised Crime (5th Estate).
  Lakini ninyi kwa njaa au uoga mmekuwa wadogo mkawa dependants wa wadogo zenu the 5th Estate, mmeshindwa kujiamini na kujitegemea, hamuwezi kusema kweli. Ninyi wenyewe mnakatishana tamaa, msema kweli anatengwa.

  Gazeti la MwanaHalisi limefungiwa mmekaa tu kimya, Jerry kashikishwa kesi mmekaa tu. Na sasa mwenzenu, Mtanzania mwenzetu kauwawa tena on field, mtafanyaje?

  Je Mtakaa kimya upepo upite?

  Je Mtakubali pesa muudanganye Umma?

  Je Mtageuza kifo cha Daudi mtaji wa kupokea na kuomba rushwa a.k.a vibahasha?

  Je sasa mtaona kama wakati umefika na kusimamia kweli na haki??

  Sisi wananchi tunangoja kuona nini itakuwa reaction yenu, na je ina manufaa kwetu sisi na Taifa.

  Msiogope, Tunachopigania leo ni kwa ajili ya maisha yetu na watoto wetu kesho. Wengi tutaumia, tutalemaa, tutafungwa na wengine kuuwawa lakini tusitishike tusonge mbele. Hata wazazi wako walijinyima ndio mana leo angalau unaweza hata kusoma hii post.

  Watoto wanaozaliwa kwa siku ni zaidi ya mara mia ya risasi zinazotengenezwa kwa siku, Hatutaisha wote, kuna watakaobaki kuelezea Stori hizi za ukombozi.

  Rest In Peace Daudi Mwangosi.
   
 2. Root

  Root JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,217
  Likes Received: 12,928
  Trophy Points: 280
  you are totally right on what you have just said kwa kweli kuna picha hapa inaosha mtutu umeelekezwa tumboni kwa marehemu Daudi View attachment 63613 yaani ukizoom vizuri utaona marehemu mkono mmoja umemshika askari kuna askari amemuwekea mtutu tumboni
  View attachment 63615 ona huyo askari anavyoshangaa baada ya tkio kutokea na hiyo ni gari ya rpc
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,565
  Likes Received: 18,307
  Trophy Points: 280
  Speechless!

  RIP Daudi Mwangosi!.

  Pasco.
  (Mwana Habari wa JF).
   
 4. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #4
  Sep 2, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Well said,..you know sometimes i wonder matukio muhimu yanapotokea hasa yale yenye kuhusu uhai wa raia na Integrity ya Taifa na wanapuuzia..kwa kutotangaza/kuandika hivi hata familia zenu huwa zinadiriki kuangalia hizo Taarifa zenu au kusoma habari tofauti na matarajio yao?

  Waandishi wa habari badilikeni, watanzania wengi wanawategemea ninyi either kwa kuhalalisha au kupuuza mambo..and same message to Owners(Media Owners).
   
 5. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #5
  Sep 2, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 850
  Trophy Points: 280
  well said, daima ukweli utashinda.
   
 6. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #6
  Sep 2, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,276
  Likes Received: 662
  Trophy Points: 280

  Pasco kipindi hiki mnao ushahidi wa picha video. Piganieni haki zenu hata Mahakamani, hata mkishindwa mjue mlijaribu.
  Kwa Heshima ya Daudi Mwangosi
   
 7. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #7
  Sep 2, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ndiyo wangoje kimbunga kutoka vyombo vya habari.

  Bila shaka uysiku huu kuna harakati nyingi kati ya RPC Iringa, IGP Mwema, Dr Nchimbi, RC Iringa na DC Mufindi katika kupata msimamo mmoja kuhusu tungo zitakazotolewa na Polisi kesho kuhusu kuawa kwa mwandishi wa habari.

  Nawaza tu sijui watakuja na maelezo gani yatakayoweza kukubalika na magazeti yakaandika positive headlines kwa polisi. Hata kama watashikilia lile lile la siku zote -- la 'hawakutii amri" maelezo ambayo yanaanza kuchosha masikioni, yatapinduliwa na wahariri. polisi wamechokoza nyuki kwa vyombo vya habari.
   
 8. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #8
  Sep 2, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,276
  Likes Received: 662
  Trophy Points: 280

  Kama moto unachoma kwa jirani na wewe unasema sio moto, watu hawatauzima wakijua sio moto. Lakini upepo ukija kidogo Moto huo utaunguza hata kwako.

  Ukweli hutuweka huru.
   
 9. Kingcobra

  Kingcobra JF-Expert Member

  #9
  Sep 2, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Frankly speaking, nimesikitishwa sana na kifo cha mwanahabari na kiongozi wa chama cha waandishi wa habari mkoani Iringa Daudi Mwangosi. Hakika ningekuwa mwandishi wa habari, ningesitisha mara moja kuandika au kutangaza habari yoyote inayohusu serikali mpaka jamii nzima ya wanahabari iombwe radhi na kiongozi wa serikali.
   
 10. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #10
  Sep 2, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,276
  Likes Received: 662
  Trophy Points: 280


  Hizi picha zimeniliza.
   
 11. K

  Kimweli JF-Expert Member

  #11
  Sep 2, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 865
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Tanzania ni zaidi ya hatari
   
 12. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #12
  Sep 2, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Mwanadamu hawezi fanyiwa unyama namna hii na mwanadamu mwenzie, please ccm ondokeni tu kabla hatujawafukuza kwa nguvu
   
 13. Head teacher

  Head teacher JF-Expert Member

  #13
  Sep 2, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,811
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  watakuja na bomu la machozi lilirushwa na slaa
   
 14. K

  Kimweli JF-Expert Member

  #14
  Sep 2, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 865
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  R.I.P Daud, police wetu ni kwa ajiri ya kuua watu. Damu yako hataenda bure. Mungu akupokee kwa moyo mmoja
   
 15. Root

  Root JF-Expert Member

  #15
  Sep 2, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,217
  Likes Received: 12,928
  Trophy Points: 280
  bado hapo pia watasema CHADEMA Ndio wahusika wakati ukiimaximize na kuangalia vizuri utaona huyo polisi amemuwekea mbele yake kuna police sijui ndio RPC mwenye blue ameshika bastola wabaona tu


  ukija hiyo ya chini kuna huyo askari anashangaa kuona yaliyotokea

  kuna picha nyingine zinaonesha wakimchukua mtu wao na kumuacha marehemu chini surely hii serikali imeoza
   
 16. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #16
  Sep 2, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,276
  Likes Received: 662
  Trophy Points: 280
  Nimeangalia hizo picha, na kufikiria majibu mepesi tutakayopewa kesho nimepata hasira sana.
   
 17. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #17
  Sep 2, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Waandishi kwa nini msianzishe move ya kuigomea serikali mpaka iwaombe radhi? Mkiendelea kuandika habari za serikali nitajua kweli nchi hii haina waandishi wa bahari.
   
 18. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #18
  Sep 2, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  Baada ya ajali za barabarani,polisi tanzania inaongoza kwa kuua na rushwa!maradhi hayaui kama polisi
   
 19. n

  ndomyana JF-Expert Member

  #19
  Sep 2, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 4,731
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Inauma sana polisi kufanya hivi nani alikutuma
   
 20. SOLOMO

  SOLOMO JF-Expert Member

  #20
  Sep 2, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Waandishi wa Habari, ni vyema sasa mufahamu kuwa hakuna tena haja ya kupuliza! Unapoandika ukweli kuhusu uozo wa CCM na Serikali yake, usijaribu tena kuficha ukweli kwa namna yoyote ile. Ninyi pia mnaonekana sawa na CDM kwani wamekuwa wakisema siku zote kuwa ninyi ni MHIMILI WA NNE hivyo mnatishia Mhimili wa Serikali yao.

  Jiulizeni jamani! hivi kuna uhusiano gani kati ya sensa na ujenzi wa chama cha siasa!!!? Polisi bila aibu mnatumwa kwenda kuwapiga watanzania wenzenu hadi kusababisha vifo ili tu kulinda maslahi ya wachache! Haya tuone kama mtakapoongezwa vyeo vya 'V' mtarejesha imani ya wananchi kwenu. Kweli kuwa polisi ni sawa na kurejeshwa Chekechea. Tumeumia sana kutokana na kitendo cha kusitisha maisha ya Comred Mwangosi!
   
Loading...