mzeewaSHY
JF-Expert Member
- Aug 31, 2021
- 8,588
- 8,217
Kutokana na kufundishwa uzalendo wa kweli na wakawa wamefaulu kweli kweli ndio maana huwezi kumpata mchina ameiibia nchi pesa na Kwenda kuziweka nchi za ng'ambo !! Ukiiba pesa za Umma wanakunyonga! Ukijihusisha na madawa ya kulevya wanakunyonga ! Investment ya kutoka nchi za nje haikatazwi mradi ufuate sheria za nchi !!Unazungumzia kitu ambacho huna uelewa wa ndani. Uchumi wa China umeshikiliwa na mataifa ya Magharibi. Tafuta kwenye orodha ya makampuni makubwa kabisa 10 ya nchini China, niambie ni mangapi yanamilikiwa na wachina/China. Unaelewa kilichofanyika nchini China miaka 2000 kilichosababisha China yenye uchumi hohe hahe mpaka kufikia ukuaji wa 12% kwa mwaka?
Hivi unajua kuwa katika real development (human development), China ni nchi ya 89, ikizidiwa na nchi kama Botswana? Usione wachina wanazurura Duniani kote, ukadhani wanapenda. Hali zao za kimaisha na duni sana, japo Serikali ina pesa nyingi.
Huko Urusi kuna makampuni zaidi ya 1000 ya nchi za Magharibi. Unafuu wa uchumi wa Urusi, ulikuja baada ya kuachana na Leninism, na kuruhusu uwekezaji wa nje na uchumi huria lakini bado kuna pengo kubwa sana la maendeleo ukilinganisha na nchi kama US, UK, Belgium, Germany, Japan, Italy, Norway, n.k.
Hakuna nchi hata moja ya kidikteta ambayo wananchi wana maendeleo halisi. Urusi ni nchi ya 52 kwenye human development.