Kwenu mawifi, wake wa kaka zetu

mchakavumlasana

JF-Expert Member
Mar 9, 2011
389
212
Nineitoa mahali....

Kwa group husika mtanisamehe tu kaujumbe kamenigusa

Kama ilishaletwa humu pia mnisamehe bure


Kwenu mawifi wake za kaka zetu....


Salaam nyingi ziwafikie hapo mlipo ni matumaini yetu mu wazima sisi pia wazima hofu kwenu mlio mbali nasi..

Dhumuni ya hii barua nikuwaambia kuwa sisi tunawapenda wala hatuna vinyongo nanyi kuna matatizo mnayaleta wenyewe kwa sababu ya kuingia ktk ndoa kwa kujihami kutokana na historia fulani. ..

wifi zetu mbona mnakuwa hivyo kwa nini hamtaki kaka zetu watusaidie??mbona kwenu wanasaidia..je hamjui kuwa waume zenu wana ndugu pia wanaoweza hitaji msaada? ?wifi zetu kwa nini mnatudharau tukija majumbani mwenu??wengine mnathubutu hadi kuwaambia wadada wa kazi tusiwatume hata kununua vocha magengeni??

wifi zetu mnawafanya nini kaka zetu mbona mnakuwa wakali hadi wanaogopa kukaa na sisi tukija kutembea..wifi zetu kwa nini hamuwapendi mama zetu??mbona mnasahau kuwa ndio waliowazalia waume zenu..mbona mnasahau kuwa hizo kazi za waume zenu bila wazazi wasingepata mbona mnasahau jinsi mlivyowahi simuliwa kuwa mama zetu wengine walipika hadi gongo ili wasomeshe waume zenu..
kwa nini mnawatenga hawa kina mama hata kitenge hamuwapi..mbona kwenu mnapeleka?


Wifi zetu mbona mkija likizo kusalimia mnakuja nakucha ndefu ka kwale mbona mnalala ukweni hadi saa 4 kwa nini mnafanya hivyo??wifi zetu kama hamuwezi kutumia kuni kwa nini.msiwe mnawashauri kina kaka wawe wanakuja na gesi kijijini kama mulizowanunulia kwenu??wifi zetu kwa nini mmekuwa wanyimi..tukiwatembelea sie mnaona ni mzigo mbona mmejaza hadi binamu zenu kwenye nyumba za kaka zetu.


.wifi zetu ni mengi ya kuongea lkn karatasi linaishia hapa tunaomba sana mtuthamini na muwathamini wazazi wa waume zenu..wengine kutwa mnashinda vijijini kwenu na kaka zetu lkn kwetu hamji..wifi zetu badilikeni mkipata familia nzuri msitake kujionyesha usupa star hakuna mwenye kutaka kuingilia ndoa za kaka zetu tatizo mnaingia kwenye ndoa kwa kujihami ndio maana hamuoni uzuri wa ndugu wa kiumeni badilikeni.

Mwisho wasalimie watoto ingawa hamtaki waje vijijini eti hakuna video lkn milimani kwenu tumesikia wanaenda hongera kwa kufanikisha zoezi la kumwambia kaka ajenge kwenu na kusomesha ndugu zenu..nakutunyima ada sisi wa kiumeni....


Ni sisi watiifu
Mawifi kiumeni
 
Mawifi wengi ( ndugu upande wa wanaume) wanaboa.
Unakuta wifi anataka anyenyekewe kama vile yeye ndiyo Mume.
Pia kumridhisha binadamu ni kazi sana maana mazuri 1000 hufutwa na baya moja.
Nyie hamjui kaka yenu akishaoa majukumu yanaongezeka? Mnataka mchote tuu hela tusiwe na maendeleo ? Mwishowe mseme mwanamke nuksi?
Binafsi mawifi huwa nawachukulia watu wa kawaida sana.
 
Kakako akio jua Wifi wewe ni mtu wa kupita tu maana nawe ujiandae kua na mji wako badala ya kukaa na kubinyana mapaja na kakako kwenye kochi kwa mbanano, mawifi mtulie muache meno ya Mbele kung'ata ng'ata ndoa za kaka zenu maana ufanyalo nawe utafanyiwa muda wako ukifika!! Ninachoshukuru wifi yangu ni kigego
 
Kakako akio jua Wifi wewe ni mtu wa kupita tu maana nawe ujiandae kua na mji wako badala ya kukaa na kubinanyana mapaja na kakako kwenye kochi kwa mbanano, mawifi mtulie muache meno ya Mbele kung'ata ng'ata ndoa za kaka zenu maana ufanyalo nawe utafanyiwa muda wako ukifika!! Ninachoshukuru wifi yangu ni kigego
Leo......
 
Mawifi na nyie si muolewe tu,msituonee wivu bwana,kumbukeni hata sisi tuna ma wifi wake za kaka zetu,ila kwa vile tupo busy na kulea ndoa na wanetu hatuna time.Ushauri oleweni ili msiwe na time ya kufuatilia wake za kaka zenu.
 
Wifi deal na ndoa yako yangu haikuhusu, ma mkwe nampenda sana tu make bila yeye nisingepata mume.....
Kuishi kwa kuigiza siwezi wifi kwa hilo nisamehe bure kwangu naamka saa mbili kwanini nije ukweni niigize kuamka sa kumi alfajiri, nipigwe baridi weee mwisho nipate ngiri hapana asee!
 
Hahaha
Kila mwanamke mwenye kaka lazima awe wifi ake mtu...

Tuanze kujiangalia sisi kwanza maana hata sie tuna mawifi!!!!

Kwangu mie mawifi wananipenda hasa Emmyta, sijui ndo karibu mgeni.... Ila mke wa Kakangu nampenda ingawa twakutana mara chache sana hasa siku za siku Kuu tu nafikiri hili nalo huwa lasaidia pia
 
Mawifi wengi ( ndugu upande wa wanaume) wanaboa.
Unakuta wifi anataka anyenyekewe kama vile yeye ndiyo Mume.
Pia kumridhisha binadamu ni kazi sana maana mazuri 1000 hufutwa na baya moja.
Nyie hamjui kaka yenu akishaoa majukumu yanaongezeka? Mnataka mchote tuu hela tusiwe na maendeleo ? Mwishowe mseme mwanamke nuksi?
Binafsi mawifi huwa nawachukulia watu wa kawaida sana.
Una kaka aliyeowa?
 
Mawifi na nyie si muolewe tu,msituonee wivu bwana,kumbukeni hata sisi tuna ma wifi wake za kaka zetu,ila kwa vile tupo busy na kulea ndoa na wanetu hatuna time.Ushauri oleweni ili msiwe na time ya kufuatilia wake za kaka zenu.
Halafu unaachaje kutafuta maisha yako,ukitegemea mtu mmoja awatoe umasikini au akusaidie na weww umekaa tu,anaetafuta anangalia watoto wake na uzee wake.
Hatulogwi ila tunaangalia utaokuwa uzee wetu.
Jukumu lipo kwa wazazi wasiojipanga tu,kwakuwa hawana nguvu.
Akina dada na wao wakachague wanaume wanaowafaa,siyo mizoga halafu shida tupate kina KAKA.
 
Back
Top Bottom