Kwenu kinaota/kinamea au kustawi kitu gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwenu kinaota/kinamea au kustawi kitu gani?

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Malila, Mar 6, 2012.

 1. M

  Malila JF-Expert Member

  #1
  Mar 6, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Kutokana na ushauri wa wadau wa jukwaa hili hasa upande wa kilimo, kumetolewa mawazo ya kuwa na data base ndogo ya taarifa muhimu za mazao,wanyama mbali mbali ambayo itakuwa hapa hapa jukwaani muda wote. Hapa tuwaombe wakuu wa jf waifanye iwe sticky ili new comers wasianzishe nyuzi nyingi nyingi juu ya suala lililokwisha ongelewa.

  Ninachokuomba mdau wa jukwaa hili la kilimo/busness ni kutoa taarifa sahihi za sehemu unayoijua kuhusiana na kilimo fulani, au wanyama fulani na viambatanisho vingine kama mawasiliano,manpower, hali ya hewa, nk nk.

  Mfano; Kwetu kunalimwa Pareto, ila ardhi hakuna.
  Katumba parachichi zinakubali sana, ila ardhi hakuna.
  Iringa ( Kilolo) kilimo cha nyanya kinawatoa watu na ardhi ipo, manpower ipo, mvua ipo, usafiri poa na vibaka
  hakuna.
  Ruaha Mbuyuni, vitunguu ndio kwake, ardhi ya kukodi ipo sana, usafiri upo, manpower ipo,na umeme upo.
  Mifugo; Misenyi kuna faa kwa ufugaji wa ng`ombe, lakini ardhi je ipo?
  Kitulo ng`ombe wa maziwa wanakubali, ila mashamba hakuna
  Ukifika Chunya, kuna nyuki wadogo,kilimo cha alizeti na wachimbaji wa madini wadogo wadogo.
  Tukichangia kidogo kidogo kila mtu kwa kadri ajuavyo, tunaweza tukapata majibu ya maswali yetu hapa hapa jamvini.
  Niwashukuru wote waliotoa wazo hili kupitia thread ya aridhi ya kitunguu. Vaveja sana.
   
 2. jino kwa jino

  jino kwa jino JF-Expert Member

  #2
  Mar 6, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kwa upande wa mavzao tuweke kabisa na msimu wa kupanda na kuvuna na mazao yanachukua muda gani hadi kuvunwa,

  huku kwetu pwani twalima mihogo inakubakui sana, mvua kidogo tu unauhakika wa kuvuna.
   
 3. L

  LAT JF-Expert Member

  #3
  Mar 6, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  Malila, yes, this is another great potential thread that can give way, more over may even attract prospecting farmers or investors in farming to think twice

  what i can say is that, this is a big "promo" to commercial farmers

  who guess what and run fast is always the winner,

  Malila, pamoja na mazao ya soko la nadani ningependekeza tujikite kudadavua maenneo ambayo yanapotential ya kilimo cha mazao yanayofaa kwa export ........ hii itawasaidia wanaochungulia humu kupata info na kuzifanyia kazi kwani bila kujikita na mazao ya export bado tutaendelea kulima mahindi ya kuchoma na viazi vitamu kwa ajili ya futari

  tuamke

  Location: Sanya Juu, West Kilimanjaro, Hai district,Kilimanjaro region

  Potential agro : Vanilla

  Export Market : Kenya, Europe and UAE

  Seasonal crop
   
 4. M

  Malila JF-Expert Member

  #4
  Mar 6, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Vizuri sana jkj,
  Huku Pwani ni kukubwa na kunafahamika sana. Ungesema moja kwa moja kwamba, mfano kule kimanzichana mhogo aina ya Kiroba unastawi sana, muda ni miezi kadhaa,mauzo nje nje. msimu mzuri ni kuanzia mwezi kadha. Ingependeza, angalia LAT alivyoeleza kwa ufupi hapo juu.
   
 5. M

  Malila JF-Expert Member

  #5
  Mar 6, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Location; Bonde la Mbingu - Ifakara
  Crop ; Organic cocoa - is a perenial ( harvesting starts at 3yrs age)
  Export; USA

  Kiongozi wa kilimo hiki ni Parokia ya Mbingu kwa msaada wa jamaa wa USA,(MOCOA- Mbingu Organic cocoa association), ni kilimo cha Cocoa bila matumizi ya madawa. Unaweza kujiunga na MOCOA, mpaka nilipokuwa naondoka pale kituoni Mbingu, kulikuwa na wanachama zaidi ya 70 wa kutoka miko mbalimbali Tanzania.
   
 6. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #6
  Mar 6, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  MOCOA ni chama cha wakulima wa cocoa, chama hiki kinaenda vizuri sana, wamepata ufadhili wa serikali ya Marekani kwa ajili ya kilimo hai cha zao la cocoa ukiwa chini ya uongozi wa Bw. Lwiga

  Idadi kubwa ya ndizi zinazoliwa jijini Dar es Salaam aina ya mzuzu zinatoka Mbingu. Eneo hili nadhani lilipendelewa na Mwenyenzi Mungu, ukiweka aina yoyote ya mbegu chini ya ardhi itaota vizuri sana, maji ya mito yapo mengi sana, yanayotiririka kutoka milima ya Udzungwa. Serikali inatakiwa isaidie wananchi wa maeneo haya kuchimba mifereji ya kuchota maji kutoka kwenye mito na kuyapeleka kwenye mashamba.

  Ni eneo lenye chakula kingi na ndiyo eneo lenye barabara mbaya sana hasa kipindi cha mvua, barabara zinafungika na wenyeji hutumia treni ya Zambia kutoka na kuingia eneo hilo.
   
 7. T

  Topical JF-Expert Member

  #7
  Mar 7, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kwetu dodoma: karanga na mtama
   
 8. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #8
  Mar 7, 2012
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Wilaya ya Chamwino

  Alizeti
  Ufuta
  Mibono

  Ardhi ipo ya kutosha ila manpower si ya uhakika sana! na miundo mbinu si mibaya sana wakati wa mvua.........magari madogo na trekta bado yanaweza kupita

  Wilaya ya Tunduru

  Mpunga unastawi ardhi ipo ya kutosha
   
 9. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #9
  Mar 7, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Mbinga, Ruvuma

  Kahawa inastawi vizuri sana, sasa hivi wilaya imechukuwa nafasi ya kwanza, Kilimanjaro, Kagera, Arusha, Mbeya zinafuatia

  Mashamba yanapatikana
   
 10. d

  dav22 JF-Expert Member

  #10
  Mar 7, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 1,902
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Idea nzuri hii naona .......
   
 11. M

  Malila JF-Expert Member

  #11
  Mar 7, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Mkuu ukifafanua kabisa itapendeza sana, yaani ukisema milima ya Matengo soft arabica inamea vizuri au robusta. Halafu tukija kwenye ardhi inabidi utusaidie kidogo, je ni ardhi ya kijiji au mashamba ya watu, au ni mapori ya kujikatia? Na bei ni friendly au ni pasua kichwa?
   
 12. Kitope

  Kitope JF-Expert Member

  #12
  Mar 7, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Neno La siku! Export kwa mtindo flani tunaweza kukuta mkulima anafaidika kwa mengi, wacha utajiri bali kuwa na uwezo wa kujikabili na vikwazo vidogo vidgo hasa katika nyenzo za ukulima na mahitaji yake mengine.
   
 13. M

  Malila JF-Expert Member

  #13
  Mar 7, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Kuna huyu chura anayeliwa na anapatikana Mtwara, watu wa Mtwara kama mnajua hii rasilimali tujulisheni nini kijiji kipi ambako mbegu yake inapatikana. Kuna jamaa aliwahi kuwafuga maeneo ya Kibaha, wanaweza kufikia 0.25Kg, na mauzo ni nje ya nchi huko Ufaransa na far east. Mavuno huanza baada ya miaka miwili. Jamii yao kama sijakosea ni Bullfrog.
   
 14. L

  LAT JF-Expert Member

  #14
  Mar 7, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu malila

  je una ufahamu wa zao la zabibu inakubali vizuri maeneo gani ukiondoa maeneo ya Dodoma kama vile makutupora, veyula na mzakwe? zabibu nyeupe (white grapes) ni deal kama almasi,

  je hakuna uwezekano wa maeneo ya coast kama fukayosa au kiwangwa ambayo nahisi ni semi arid kuweza kustawi zao hili la zabibu
   
 15. Kitope

  Kitope JF-Expert Member

  #15
  Mar 7, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Huyo chura nimemsikia, kwenye delicate menu in France. chura pia hutumika. na bei yake mkuu ukiisikia utakimbia. ama furaha itakujaa kama wewe ni msambazaji wa chura hao. Ila process zake zinahitaji mtu kuwa verry serious na hio biashara vinginevyo unaweza kukata tamaa njiani. kwa mujibu wa wanakijiji wenzangu, wafaransa kwa sasa wana import hao wadudu sana kutoka Asia. Je kuna mtanzania that dares to do so! I would call this not far from being a Niche Market ( take that in consideration and think of what it takes)
  kwa mtwara sina taarifa sana. waliopo huko mtufungue macho
   
 16. Kitope

  Kitope JF-Expert Member

  #16
  Mar 7, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Watanzania tuna Mali nyingi sana, tatizo wote huwa tukishavuna tunajazana dar-es-salaam kutafuta soko. hatuwezi kulaumiana kwa hili kwa sababu where else and how!!! is out of our knowledge/ability. ila mkulima wa dot com haya yote ni verry possible. ukitembea nje utakuta mazao mengi tuliyonayo kwetu yana soko kubwa tu. na kwa mifumo kama hii ya watu kupeana mawazo, mkulima anaweza kufika mbali sana (without 10%) kama atachukulia shughuli yake serious. consultancy can never be a problem for those who can consult and have the knowledge of a specific market and its customers behaviour.
   
 17. M

  Malila JF-Expert Member

  #17
  Mar 7, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Hii ni homework kubwa, hata mimi nilikuwa najua Dom tu, lakini siku moja niliona mizabibu Iringa mitaani ktk kijiji cha Ndiwili mtu kapanda kama mapambo,ngoja nifanyie kazi nitatoka na jibu. Fukayosa nimefika january 2012, wasiwasi wangu uko ktk soil PH and capillarity. Ila ukiniambia Mvomero kule ndani ndani Mbigiri/Mabana inawezekana.
   
 18. L

  LAT JF-Expert Member

  #18
  Mar 7, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  malila, kuna wakenya huwa wanasign mikataba na wakulima wa zabibu nyeupe (contract farming) maeneo ya dodoma, wakati wa mavuno wanakuja na refrigirated truck yao, wanavuna wao wenyewe, wanapakia na kusafirisha kwenda Nairobi, wakifika huko wana repack nakupeleka spain

  ukifanikiwa hii homework, utakuwa na hazina kubwa sana

  hili zao ni rahisi sna pale utakapopata the right place na mavuno yake ni sustainable for a period of time
   
 19. M

  Malila JF-Expert Member

  #19
  Mar 7, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Tayari nimetuma ujumbe kwa dogo yuko Mipango dom ili afanyie kazi suala hili.
   
 20. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #20
  Mar 7, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  ardhi ya kongwa ni nzuri sana kwa karanga, maharagwe na njugu iwapo mvua itakuwepo kwa wingi mwaka utakaolima (kongwa kidogo mvua ni nyingi ukilinganisha na wilaya nyingine za dodoma). Mashamba ya kukodi yapo na bei ni maelewano c'se wenye ardhi huwa hawaitumii. Usafiri ni 4WD au pikipiki
   
Loading...