Kwenu Kikosi cha Usalama Barabarani na TARURA

Lubengera

JF-Expert Member
Jun 21, 2019
810
1,292
Yah! Barabara ya External-Maji Chumvi-Kwa Mkuwa-Korogwe

Kichwa cha habari cha husika. Kwa masikitiko makubwa sana, naleta kwenu ombi la kuweka vibao vya spidi ya vyimbo vya moto.

Barabara hii imekuwa na Ajali nyingi zinazotokana hasa na spidi, ingawa kutoka Korogwe-kwa Mkuwa- Maji chumvi-External hakuna sehemu iliyoruhusu ku Over take.

Kikosi, sisi wakazi wa huku tuko hatarini, ajali zimezidi saaana!

Natumaini ombi langu mtalifanyia kazi, basi hata kwa namna nyingine kama alama za barabarani na hasa speed zimeshindikana kuwekwa.

Binafsi siafiki mtu akisema eti ni kama barabara za mtaani! hiinsio sahihi! barabara hii inakona nyingi, lakini pia magari yamekiwa mengi sana.

Nitafurahi endapo ombi langu litashughurikiwa

Mwananchi wa kawaida.
 
Huwa ninakereka sana na mwendo kasi.

Hiyo barabara Kama ile ya Marangu-Mwika hadi Mamsera.

Kuna siku tulikuwa na msiba huko.

Mimi nilikuwa naendesha moja ya gari zilizokuwa kwenye msafara wa msiba.

Barabara ile speed limit ni 30 kwa sehemu kubwa ila cha kushangaza Kuna dereva wa kosta ambaye naye alikodiwa na alibeba waombolezaji akaniovateki kwenye kona kwa mbele alinusurika kugongana na gari ndogo nikamsevu kwa kupunguza mwendo.

Nilimshangaa sana.

Kwanza njia ina kona, then tuko msibani, na tupo pamoja sasa alikuwa na haja gani kwenda kasi?

Tukiwa hospital mzee mmoja ananiambia wakati wa kurud niongeze mwendo.

Nilimjibu kuwa tuko msibani isitoshe barabara ina kona sana.

Yaani hata hiyo ya maji chumvi huhitaji kuwekewa vibao Wala nn.

Dereva mzuri anajua njia inahitaji speed limit ngapi.

Tatizo lingine mtu akiendesha rafu anaonekana anajua sana kumbe ni ujinga
 
Back
Top Bottom