Kwenu Chuo Kikuu cha Dodoma na ofisi inayoshughulikia udahili wa wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2020/2021

P Accountant

JF-Expert Member
Sep 26, 2020
369
169
Habari za wakati huu wana JamiiForums.

Ujumbe huu wa wazi napenda uwafikie uongozi wa chuo kikuu cha Dodoma, pamoja na ofisi inayoshughulikia maombi ya wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2020/2021.

Kwanza kabisa nipende kuwapongeza kwa kazi nzuri ya utoaji wa elimu kwa Wanafunzi ndani na nje ya Tanzania.

Kwanza, nianze kuwashauri ofisi inayoshughulikia maombi na udahili wa wanafunzi UDOM, katika vipengele vifuatavyo:-

i, Mfumo wenu wa maombi ya kozi sio mzuri sana ukilinganisha na vyuo vingine, hususani katika uchaguzi wa kozi. Kwani hamna kipengele cha kubadilisha kozi kabla ya dirisha kufungwa, hii imekuwa kero kubwa sana kwa Wanafunzi.

Mfano mwanafunzi akianza na kozi ya Sheria kama chaguo la kwanza, hamna nafasi ya kubadilisha chaguo. Hii ni tofauti na UDSM ambayo ni ruhusa kubadilisha chaguo la kozi muda wowote kabla dirisha halijafungwa.

USHAURI, fanyeni mabadiliko katika mfumo huu ili kuepusha kero kubwa sana kwa Wanafunzi.

ii, Utaratibu wa kuthibitisha chuo nao ni kero kubwa sana tena sana kwa Wanafunzi. Kwani mfumo wenu hauna kipengele cha kubatilisha maombi. Tofauti na vyuo vingine.

USHAURI, wekeni kipengele cha kubatilisha(UNCONFIRM) maombi ya kujiunga na taasisi yenu.

Kwani si Wanafunzi wote wanapata uwezekano wa kutumia internet, hasa waishio vijijini hivyo hupelekea kuwapa maagizo ya kuthibitisha vyuo watu wengine, Ambayo madhara yake ni kwenda chuo wasichokitaka hasa kama hakuna mfumo wa kubatilisha maombi. INAUMIZA SANA.

iii, Mtandao upo chini sana kwa wanaothibitisha na kuomba vyuo.

OMBI LANGU KWENU
Wekeni kipengele cha kubadilisha kozi kwa wanaoomba chuo. Pia wekeni kipengele cha kubatilisha(UNCONFIRM) maombi ya kujiunga chuo chenu. Kabla ya tarehe ya mwisho 17/10/2020 kama ilivyo agizwa na TCU.

UDOM ni taasisi kubwa nchini, lakini kwa mambo hayo juu yanaleta walakini.

Natanguliza shukrani hasa pale mtafanyia kazi maombi haya na ushauri huu.

Wenu,

Triple Entente.
 
Back
Top Bottom