Kwenu AIRTEL, wizi huu mliouanza hauvumiliki!

REAGAN C.MABOGO

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
1,269
1,007
Juzi tarehe 3 bando yangu ya wiki (mitandao yote) iliexpire kabla ya muda. Nikachukulia poa. Nikaamua kujiunga tena kupitia AIRTEL MONEY, na bando nyingine ya wiki, hiyo ikiwa ni tarehe 3 yaani juzi Jumatano.

Leo saa nane hii napiga mtu anapokea tu na simu inakata. Napokea ujumbe ukisema salio langu limekwisha. Nikaangalia salio kwenye hiyo yatosha (mitandao yote) nakuta nina dakika 0, 0 bytes , na 0 sms. Nikapiga simu AIRTEL huduma kwa wateja najibiwa kuwa wameona sijawahi kuweka vocha wala kununua salio ama bando yoyote kwa AIRTEL MONEY tangu JULY.

Nimeshituka sana.! Na kama hivyo ndivyo ilivyo mitambo ya AIRTEL, basi wenye pesa zenu kwenye account za AIRTEL MONEY anzeni kutafakari upya kabla mambo hayajaharibika. Muda wowote utaenda kutoa pesa na utapata ujumbe kuwa huna salio la kutosha kwenye account yako.
 
Pole sana mkuu, kama ulinunua kwa airtel money c unatumiwa namba ya muamala wa kununua ? Kwa nn usitumie hyo kulalamika kwao..
 
Hoja yako ni sahihi kabisa hata mimi yamenikuta na leo hii nimeachana kabisa na Internet ya Airtel na nimejiunga rasmi na Halotel. Kasi ya mtandao ni nzuri sana ukifungua ni mara moja haina kusitasita kama mitandao mingine. Najuta kuchelewa kujiunga na Halotel !!
 
Back
Top Bottom