Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Wakati wananchi wake hapo juu wanahangaika pa kula, kulala na afya zao!...
(Picha zote toka kwa Michuzi)
Hoja imejengwa humu na watetezi wa "majanga ya kitaifa hayazuii Rais kwenda kuburudika" na kuwa tukiwa na matatizo makubwa haina maana Rais hafanyi shughuli muhimu 'za' kitaifa. Watetezi hawa wametetea kwa nguvu mno kuwa ilimlazimu Rais Kikwete kwenda mpirani ili kuonesha uongozi na kuwa ilikuwa ni sehemu ya kazi yake!
Katika hili ninawaita hawa ni watetezi wa uzembe na mazingaombwe ya siasa na ulaghai wa uongozi kwa sababu ningewaita vingine ingekuwa ni heshima wasiyostahili!
Nilikuwa mtu wa kwanza kutoa taarifa ya mafuriko makubwa siku ya Krismasi na kusema wazi kuwa "maafa yahofiwa". Nililiamsha tena taifa langu na kuliasa kujiandaa kama nilivyofanya zaidi ya mwaka mmoja uliopita katika makala ya "taifa lisiliojiandaa kwa majanga limejiandaa kwa maafa". Nilitegemea labda wangeamka!
Wakati watu wetu wanakosa pa kula na kulala, wakati watu wamekufa, wakati reli ya kati imechomolewa na usafiri kwenda bara kwa njia hiyo unakomeshwa kwa kiasi kikubwa hadi Aprili, watawala wetu wamekaa na kupiga picha na kina Ivory Coast katika kampeni ya "kulitangaza taifa".
Zaidi ya wiki mbili zinapita sasa Rais Kikwete hata kwenda kuwajulia hali wananchi wake huko Kilosa, Kongwa, Ruvuma n.k hajafanya hivyo kwa sababu yuko katika shughuli muhimu ya kitaifa!
Cha kushangaza (kama ilivyokuwa wakati akifunga 200 kwenye hotuba yake ya kuuaga mwaka 2009 hakuzungumzia lolote juu ya mafuriko na hali ya ndugu zetu hawa. Leo hii Msalaba Mwekundu wanahitaji karibu miliooni 300 kupeleka msaada; Leo hii Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa serikali imeionyoshea kidole Idara ya Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuwa wazembe kila maafa yanapotokea!
Niiteni mlalamishi lakini sababu za yeye kutokugombea tena zinazidi kuongezeka.
Yaani wiki mbili zinapita...na anamuda wa kwenda mpirani, kuandaa dina, na bila ya shaka kufanya mambo mengine "muhimu".. it reminds me of another president in another country during a hurricane named Katrina!
Mwenyewe anaridhika baada ya kutoa statement hii kupitia kina Salva;
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,ametuma salamu za pole kwa wakuu wa mikoa minne ambayo imekumbwa na maafa yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini.
Aidha, Rais Kikwete amepongeza jitihada zinazofanywa na uongozi katika mikoa hiyo kukabiliana na maafa yanayosababishwa na mvua hizo.
Rais Kikwete ametuma salamu hizo za pole leo (jana) Jumanne, Desemba 29, 2009, kwa wakuu wa Mikoa ya Dodoma, Morogoro, Ruvuma na Rukwa.
Katika mikoa hiyo, baadhi ya watu wamepoteza maisha kutokana na mafuriko, wengine wamejeruhiwa kutokana na radi, na kumekuwepo na upotevu wa mali, na mamia ya watu kukosa mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kuezuliwa na upepo ulioambatana na mvua kubwa.
Katika salamu hizo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhandisi Dkt. James Alex Msekela, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Luteni Kanali (mst) Issa Saleh Machibya, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mheshimiwa Christine G Ishengoma, na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mheshimiwa Daniel Ole Njoolay, Rais Kikwete amesema kuwa amesikitishwa na upotevu wa maisha, upotevu wa mali na hasara ya watu kuezuliwa nyumba zao.
Nimesikitishwa na kuhuzunishwa na maafa ambayo yameambatana na mvua zinazoendelea kunyesha katika Mkoa wako. Nakupa salamu za pole wewe binafsi Mkuu wa Mkoa, na kupitia kwako, natoa mkono wa pole kwa watu wote waliopatwa na maafa kutokana na mvua hizo, amesema Rais Kikwete katika sehemu ya salamu zake kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Kanali Machibya.
Rais ametuma salamu zenye ujumbe kama huo kwa Mhandisi Dkt. Msekela, Mheshimiwa Ishengoma na Mheshimiwa Njoolay.
Katika Wilaya ya Kongwa ya Mkoa wa Dodoma watu 220 hawana mahali pa kuishi wakati idadi ya wasiokuwa na mahali pa kuishi katika Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro imefikia 2, 152 kufuatia nyumba zao kuezuliwa ama kuharibiwa na upepo ama mafuriko. Katika wilaya hiyo hiyo ya Kilosa, nyumba 922 zimefurika maji.
Katika Mkoa wa Rukwa, watu 27 wamelazwa katika Kituo cha Afya cha Kakese baada ya kuwa wamepigwa na radi katika tukio ambako mtu mmoja amepoteza maisha.
Katika salamu zake, Rais Kikwete amewaelekeza wakuu hao wa mikoa kuendelea kuchukua hatua za dharura kukabiliana na maafa yanayotokana na mvua hizo na kuahidi kuwa Serikali yake iko pamoja na wananchi waliopatwa na maafa katika mikoa hiyo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
29 Desemba, 2009