mtotowamjini
JF-Expert Member
- Apr 23, 2012
- 4,526
- 1,169
Helo my dears
kwanza nianze na story hii
juzi nilienda kwenye kitchen party ya rafiki .wakati wa zawadi mamayake kumbe alienda china kafungasha contena lina kila kitu cha ndani kilazagazaga
vitanda,magodoro ,sofa ,majiko ,friji ,radio ,matv, taulo yaaanikila kitu ambacho kinatakiwa kiwe ndani ya nyumba ya mtu hadi kijiko
kijana aliemuoa huyo dada ni mtu wa kawaida tu kwa kweli ,hata kujenga bado
sasa najiuliza hili limekaaje wadau
hivi ni sawa kwa mwanamke ukiolewa kwenda na kila kitu kwamume au ni vizuri kwenda na begi lako la nguo tu?
tatizo la hapo ni kwamba ninavyowajua wanawake..siku mwanaume akimuudhi anaweza kumwambia alale chini akisema kitanda ni changu hakuna kulala leo hapa..mmh hapana na siku mama mkwe anaingia ndani anaanza kufungua fridge ataanza kutumia vitu vyenu na kulalamika hamuwezi maana vitu ni vyake na alitumia hela yake..we kama mwanaume hapo utamwambia nini mama mkwe wakati vitu vyote ni vya kwake yeye?