Kwenda kwa mumeo na vitu vyote au kwenda na begi?

Smile, ngoja nikupa mfano wa kidunia zaidi labda utaelewa
Natataja nijaribu kutumia mfano wa ajira kukupa mantiki ya ndoa

Unapoajiriwa, mwajiri na mwajiriwa kila mmoja kuna kitu anatafuta kwa mwenzie.
Mwajiri anatafuta ujuzi wako ili aweze kuzalisha
Mwajiriwa anatafuta kipato, changamoto mpya, na labda kukua kikazi.

Lakini unapoajiriwa kuna vitu vinahitajika sambamba na ajira hiyo labda ofisi, usafiri, komputa, kalamu, simu n.k
Kulingana na makubaliano yenu mtaamua nani atoe vifaa hivyo nilivyoorodhesha, imezoeleka mwajiri kutoa ofisi na komputa lakini kuna makampuni kwa sasa machache yanakupa kazi, na hivyo vifaa utajiju ila yanakulipa kama kawaida.

Na kuna makampuni mengine yanakupa mengine wanatoa kila kitu.

Lakini yote hii inategemea na nini kila mmoja anataka toka kwa mwenzie.

Hali kadhalika ndoa, hizo nyumba, makochi, na masufuria yanasaidia tu ndoa kwenda smoothly, lakini siamini kama ndio sababu ya ndoa au ndio ndoa yenyewe.

Natumaini nimesaidia badala ya kukuchanganya zaidi.
 
Last edited by a moderator:
sio lazima ila kama unauwezo utatamani kumpa kila kitu hata wafanyakazi utatamani kumuwekea na mshahara ulipe wewe, ila je? jiulize utakuwa unamjengea binti yako huyo akili gani? ataweza kuchakarika in life na kutafuta in her own? au atakuwa ansema tu aah nikiishiwa mama atanipa na binti huyu utakuta hata kupika maandazi au chapati hajui.
Kama umemlea binti yako kisaikolojia na kimaadili vizuri na unauwezo mfungashie tuu kila kitu anachohitaji, ila kama huna uwezo usije ukakopa au ukaiba, uwezo wako ukoje? na huyu binti unataka akaishije kwa mume wake? anyenyekewe na mume na ndugu wote wa mume au...? reason behind ya kumfungashia mazagazaga yote haya ni nini?
bora unisaidie mdau ...dunia imeharibika kweli..ndo maana ndoa zina matatizo
 
Kikubwa jiulize, kwa nini unaolewa??

Unaolewa ili ukanunue vyombo??
Unaolewa ili ukamwonyeshe mmeo na wewe unaweza nunua chujio??
Unaolewa ili umma uoe na wewe ni mtu useful katika kuchangia pato la familia??

Yote haya yanategemea unatafsiri nini ndoa yako kwa wakati huo.

kongosho,sa ukute mwanaume ana mpaka chujio la nazi kweli?mimi sitakuwa comfortable,ningependa zaidi hivo vitu nivinunue mimi kwa kweli!
 
Mimi sifagilii kwenda na vitu kwa Mumeo you never know nini kitatokea baadae (Wengine tumedhulumiwa kila kitu)
 
Smile, ngoja nikupa mfano wa kidunia zaidi labda utaelewa
Natataja nijaribu kutumia mfano wa ajira kukupa mantiki ya ndoa

Unapoajiriwa, mwajiri na mwajiriwa kila mmoja kuna kitu anatafuta kwa mwenzie.
Mwajiri anatafuta ujuzi wako ili aweze kuzalisha
Mwajiriwa anatafuta kipato, changamoto mpya, na labda kukua kikazi.

Lakini unapoajiriwa kuna vitu vinahitajika sambamba na ajira hiyo labda ofisi, usafiri, komputa, kalamu, simu n.k
Kulingana na makubaliano yenu mtaamua nani atoe vifaa hivyo nilivyoorodhesha, imezoeleka mwajiri kutoa ofisi na komputa lakini kuna makampuni kwa sasa machache yanakupa kazi, na hivyo vifaa utajiju ila yanakulipa kama kawaida.

Na kuna makampuni mengine yanakupa mengine wanatoa kila kitu.

Lakini yote hii inategemea na nini kila mmoja anataka toka kwa mwenzie.

Hali kadhalika ndoa, hizo nyumba, makochi, na masufuria yanasaidia tu ndoa kwenda smoothly, lakini siamini kama ndio sababu ya ndoa au ndio ndoa yenyewe.

Natumaini nimesaidia badala ya kukuchanganya zaidi.
mmmh sijawai kuona mwajiriwa akienda ofsini ni vifaa vyote vya kazi ..kwa kweli sijawai ona..
 
Kikubwa jiulize, kwa nini unaolewa??

Unaolewa ili ukanunue vyombo??
Unaolewa ili ukamwonyeshe mmeo na wewe unaweza nunua chujio??
Unaolewa ili umma uoe na wewe ni mtu useful katika kuchangia pato la familia?

Yote haya yanategemea unatafsiri nini ndoa yako kwa wakati huo.
tunaoana ili tukamilishane!
 
nzuri dear ,hebu sema kitu dear mi nipo kwenye mshangao hapa

Mi nataka kukuuliza Smile kwani mnapofanyiwa zile sherehe zenu za jikoni ile mizawadi mnayopewa na wageni waalikwa,vikundi vinavyotoa mizawadi hususan mama mzazi huwa mnavipeleka wapi, nyumbani kwa mama yako au huko kwa mumeo unakokwenda kuanza maisha mapya????!!!!
Nafikiri ukiwa na jibu la hili basi utakua umelijua jibu langu sawia.
 
Last edited by a moderator:
Vitu vidogo vidogo naweza kununua sio kwenda navyo nitanunua nikiwa navyo ndani ya nyumba.................
mi nitaenda navyo ila baadhi lakini siwezi mfano unalalia kitanda chako na mumeo eti hii ni sawa?...raha ya kuwa mwanamke ni nini hapo kama hadi tunalalia kitanda changu?
 
Mi nataka kukuuliza Smile kwani mnapofanyiwa zile sherehe zenu za jikoni ile mizawadi mnayopewa na wageni waalikwa,vikundi vinavyotoa mizawadi hususan mama mzazi huwa mnavipeleka wapi, nyumbani kwa mama yako au huko kwa mumeo unakokwenda kuanza maisha mapya????!!!!
Nafikiri ukiwa na jibu la hili basi utakua umelijua jibu langu sawia.
mi namaanisha zawadi ziwe za kawaida dear,,sipingi kwenda na masufuria na nini ila hadi kitanda cha kulalia mume na ndugu ..kila kitu...tuangalie bwana haya mambo mpenzi
 
Mie nikipewa nyumba hata Gaborone naenda ishi naye.
Kikubwa naamini huyo mme awe anaaamini katika kufanya kazi kwa bidii.

Tatizo huja unapokutana na mwenza mtoto wa mama, na yeye kuona hamadi kibindoni kaotoka almas badala ya mke sasa yeye anabaki kula shushu tu akitamba kwa mali ya wakwe, agrrrrrr!!

Ila kama anakituma, tunaishi na yeye na mimni tunajenga zingine kwa ajili ya mafao ya uzeeni.

Huko ni kumfuga. Mwanaume anatakiwa ajenge nyumba na mkewe, sio ya kupewa. Mie na Paw wangu hata tupewe nyumba masaki na mzee Mtambuzi staki ng'oo, tutapanga mbagala, tukizichanga tuhamie sinza afu tujenge mbezi. Ila nikipewa nyumba ya kazini hapo tutaenda kuishi na l'aziz wangu kipenzi. Nitahakikisha namsaidia mume wangu na kum-push tufikie level niliyozoea na sio kwa kubebwa. Aibu gani, hata apewe na mamake nyumba staki hadi mamake afe ndo tuirithi. Aweke mpangaji ale penshion yake!
 
kwa nini uende na begi la nguo?
ndoa ni ya watu wawili...
mnaishi wawili....
kwenye shida na raha, karaha na furaha....mmoja akianguka mwingine amuinue...

unapoenda na begi lako la nguo vitu vyako atumie nani? mende?
halafu waanze kujipiga piga kununua vitu ambavyo umeviacha home? isee...
yaani huyo binti mama yake kambusti sana, hapo wajipige wanunue kiwanja wajenge....hawana shida ya kununa sofa wala friji kazi ni kwao....

ooopphs kwa kukujibu ukiolewa unaenda na vitu vyako my dear, ndo maana wengine wanaulizwa kwako hakuna nini tukununulie, maana yake aangalie alivyonavyo bi harui, then alivyonavyo bwana harusi kilichomiss ndo anunue....

Nakuaminia...
 
Mimi sifagilii kwenda na vitu kwa Mumeo you never know nini kitatokea baadae (Wengine tumedhulumiwa kila kitu)

Mmmhhh mke mwenzangu hapo mabanoni yametukuta wengi kumbe.....lol. Ila tusiwakatishe tamaa hawa ndugu zetu maana hizo ni zawadi inabidi wazibebemo hahahaaaaaa. Mie nilikosea nikabeba vyangu nilivyoanza navyo maisha(yani niliamua kuvihamisha kutoka nyumba hii kuingia nyumba hiyo niliyoenda kujumuika na taahira wangu) nikaona nikachanganya na vyake itasaidia kumbe loooh borea ningempa mama yangu hata kama angevitupia stoo viliwe na panya ni heri......lol
 
Mwanao ameolewa kwa kapuku hana hata uwezo wa kujenga kibanda umiza si umpige tafu tu jamani.

Huyo mwanangu nimemlea kupambana na maisha! Na kupata kila atakacho kwa jasho, sio kwa kupewa. Kama kaambukizwa uvivu na handsome wake watajibeba. Si auze mchicha! Akija nitamkopesha mtaji wa biashara na mumewe namkodisha shamba (najua kudai kuliko bank aliyokopa Bishanga).
watu wameuza maji mjini wamejenga maghorofa, ebooo
 
Last edited by a moderator:
Hujawahi ona mtu anaajiriwa anachopelekwa ofisini ni report tu tena kwa email??
Na wakimhitaji wanampigia simu anaenda pale.

mmmh sijawai kuona mwajiriwa akienda ofsini ni vifaa vyote vya kazi ..kwa kweli sijawai ona..
 
Mi nataka kukuuliza Smile kwani mnapofanyiwa zile sherehe zenu za jikoni ile mizawadi mnayopewa na wageni waalikwa,vikundi vinavyotoa mizawadi hususan mama mzazi huwa mnavipeleka wapi, nyumbani kwa mama yako au huko kwa mumeo unakokwenda kuanza maisha mapya????!!!!
Nafikiri ukiwa na jibu la hili basi utakua umelijua jibu langu sawia.
Kwa mtazamo huu wa Smile napata picha kuwa ile mijizawadi ni ujasiriamali..huwa wanauza ,then anaenda kwa mumewe na nguo zake tu..
 
Last edited by a moderator:
Mie nikipewa nyumba hata Gaborone naenda ishi naye.
Kikubwa naamini huyo mme awe anaaamini katika kufanya kazi kwa bidii.

Tatizo huja unapokutana na mwenza mtoto wa mama, na yeye kuona hamadi kibindoni kaotoka almas badala ya mke sasa yeye anabaki kula shushu tu akitamba kwa mali ya wakwe, agrrrrrr!!

Ila kama anakituma, tunaishi na yeye na mimni tunajenga zingine kwa ajili ya mafao ya uzeeni.

Hahahaaaaaaaaaa Kongosho bana
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom