Ni umasikini kung'ang'ania mali za mke/mme
wasiojitambua na walafi ndo huwa na tabia hizo
Ni umasikini kung'ang'ania mali za mke/mme
ofkozi,ikiwezekana wape,,,,,,wenyewe watajipanga watanunua tu kiwanja watajenga,,,,,,,
mmmh wanaume wa sasa hivi kumbe ndo maana sipati mpenzi ..ngoja nianze kusema nina nyumba namalizia mbezi beach
mimi nisie na hata na kijiko na mama yangu yupo hoi kitandani .. nitapata mtu kweli maana naona wakaka hapa ??????????????
aya maaaa..i wish ungekuwa mamamkwe wangu
Kumpa nyumba mkweo ya kuishi na bintiyo ni ishara ya ukomavu wa makuzi na malezi ukiwa mzazi
thax mdau@Sakapal but sio lazima kumpa vitu vyote eti au unasemaje?Dah! ulimwengu umebadilika sana na mambo yanaenda kutoka stage moja kwenda nyingine ni kama vile kutoka homo sapians to homo erectus etc... na kuendelea...
Kwa mtazamo wangu tangu nimeanza kupata ufahamu kwenye akili yangu zamani ili mwanaume aoe au apewe mke alikuwa anatakiwa awe na uwezo wa kulisha familia yaani mke na watoto watakao zaliwa. Awe na mahali pa kuishi either amejenga au amepanga ila sio nyumba ya familia au wanayokaa wazazi wa mume. Pia mume huyo alitakiwa awe na vitu kadhaa vya ndani ya nyumba ambavyo ni godoro, kitanda, angalau stuli au kigoda kwa wageni na mwanamke ili aweze kuolewa alikuwa anaangaliwa kwanza anauwezo wa kuzaa?, kulea watoto?, anajua kupika kwa njia zote yaani kuni, mkaa, jiko la mchina, anajua kufua, kuhudumia wagonjwa na usafi kwa ujumla. Na suala la mwanamke kuwa na kitu au kwenda na kitu kwa mume halikuwepo. Mtaji wa mwanamke kwenye ndoa ilikuwa ni uchapa kazi, usafi, kulea familia n.k. na mwanaume mtaji wake kwenye ndoa ilikuwa ni ujasiri, mtafutaji wa chakula na vitu vya familia.
Matatizo yanayotokea kwenye ndoa mengine yanafikia wenye ndoa kuachana na hapo kwenye kuachana baada ya miaka kadhaa ya kuishi kwenye ndoa ndipo ikaonekana mwanamke anafukuzwa na kirago cha nguo zake tu kama alivokuja wakati anaolewa. Hii imeipa shida jamii na kuifanya jamii ijihami au itengeneza njia za kumnusuru mwanamke ili ikitokea wanaachana au anafukuzwa basi mwanamke huyo awe na kitu cha kutoka nacho kwenye ndoa na si kufukuzwa na kirago cha nguo. Isingekuwa shida na matatizo yaliyowahi kutokea kwenye ndoa ambazo nimeshuhidia au wewe umezisikia basi hadi leo mwanamke angekuwa anatoka kwao na nguo tuu na khanga kibao na jukumu la nyumba na vitu vyake na kula likabaki kwa mwanaume. Ila kwa sababu ya matatizo hayo hata pale mume anapofariki ndugu wa mume kumnyanyasa mwanamke na kumfukuza mwanamke na nguo zake tuu wakati mali walizochuma mwamamke aliwekeza nguvu zake za uchapakazi, usafi, kulea n.k
Mabadiliko haya ndo yameleta leo wamama au wazazi kwa ujumla kuwafungasha mabinti zao wanapoenda kwa waume zao na vitu vyote vya ndani japo hapa uwezo unazingatiwa. Kwasababu wale ambao wanatoka kwenye familia duni bado wanaenda kwa waume zao na nguo tuu. Tatizo ni pale binti anapojishebedua kabla hata hajateswa na mume au ndugu wa mume, utasikia, ''eeeh usinibabaishe kama umenichoka naita fuso sasa hivi na ninasepa na kilakitu changu cha kichen party''. Hapo mwanaume akisikia hivi na akiangalia nyumba ibaki wazi anaona bora soo liishe na binti hapa anakuwa anakosea kwani unamfanya mwanaume kuwa mdogo na kutojiamini.
Ni vizuri kuwafungasha mabinti na vyombo vya ndani kwani jiko linaaminika ni sehemu ya mama na si baba ndo maana wanaume wachache sana hata waliojenga wanakuwa na vyombo vingi vya ndani. Utakuta hata kama anajipikia atakuwa na sahani moja au kikombe kimoja na sufuria moja. Kumpa binti sofa, dining table, coffe table, makabati ya ndani, godoro vitanda n.k vya ndani ili kuwasaidia wanandoa hawa kujikwamua kimaisha na si kwenda kunyanyasana.
Nimeongea kwa kireeefu but hope nimeeleweka, wanaume msiwanyanyase wake zenu waliokuja na nguo tuu na kuwakuta nyie wanaume na kilakitu ndani. Na nyie mabinti mnaoolewa na mmefungashiwa kila kitu na wazazi wenu yaani mmejaza fuso kwenda kwa waume zenu msijishebedue kwa kujiona nyumba nzima umeijaza wewe.
ZINGATIA: mwanaume na ampende mke wake, mwanamke na amtii mume wake, for sure ukiweza kuitimiza hii rule in all ur marriage life hutapata shida. Kila mtu atimize wajibu wake na kufanya yanayompasa. Play ur part in ur marriage and enjoy....!
Ni mtazamo wangu tuu.
Ever remaining,
Sakapal.
Huko ni kumfuga. Mwanaume anatakiwa ajenge nyumba na mkewe, sio ya kupewa.
hiyo poa ,kuliko aolewe akute huyo mwanaume ana kila kitu mpka tambala la deki!
aisee! hata wewe mamamdogo?Kabla ya kujibu hili swali, kitu cha kujiuliza ni 'kwa nini unaolewa'?
Ukipata jibu hapa, ndilo litakuwa vission ya ndoa yako
Haya mengine makelele tu.
Kama vission ya ndoa kwako ni mume kukutunza kwa kila kitu, basi usiende hata na nduo maana atakununulia zingine.
Kama vission yako ni kutafuta mwenza wa kufurahi pamoja na kuijaza dunia wakati unasubiri kuingia makao yako ya milele, nenda hata na Ubungo Plaza zako 5 achia mbali masufuria.
Ni sawa kwenda na vyombo au si sawa kutegemea na dira ya ndoa yenu.
mi nauliza ni sawa kwenda na kila kitu ? yaani kila kitu ndani kinakuwa ni chako ni sawa?
kweli angempa hata hela za biasharaKwa maisha ya sasa yasivotabirika especially kiuchumi mi naona kama haikuwa muimu kusomba hayo mavitu kuwapa na watu wanaenda kuishi nyumba ya kupanga.ngemuona uyo mama ana busara kama angempa hizo fedha binti yake na kumshauri azifanyie biashara ili ziwasaidie katika ujenzi na maendeleo kwa ujumla.kitu cha muimu kuingia nacho kwenye ndoa ni kazi/biashara yako,hayo mengine matokeo.
Labda mama alifanya ivo kuepusha wale wanaoleta vitu vibaya kwenye zawadi,mfano mtu anaweka lichupi la period ndani yaboksi la zawadi,au makonokono etc.
thax mdau@Sakapal but sio lazima kumpa vitu vyote eti au unasemaje?
Sio vibaya kukuta kila kitu pia,
sasa kama mwanamme anavyo avitupe??
Yote inategemea kwa nini mwaoana.