Kweli Zitto Kabwe wa Buzwagi akikutana na Zitto Kabwe huyu itakuwa ni vita ya 3 ya dunia

Maramla

JF-Expert Member
Jan 8, 2014
572
1,000
Na Nathaniel Ndilito, DSM.

Nimesoma andiko linalodaiwa kuandikwa na Zitto Kabwe akihoji kama Rais Magufuli amemtumbua Kangi Lugora kwa kusaini Mkataba ambao "haujapita Bungeni," mbona kuna mikataba mingi "haijapota Bungeni" na watu hawajachukuliwa hatua?

Kama kawaida yake Zitto akataja mifano ya yale yale makubwa ya JPM yanayomuumiza kichwa; SGR, ununuzi wa ndege na mengineyo. Anataka tuamini nayo "hayakupitia Bungeni."

Nianze kwa kusema Zitto ameshajenga dhana ya kupinga kila kinachofanywa na Serikali. Hivyo ni kazi yake kupinga lakini asitufanye sisi raia ni wajinga. Tunaielewa dhamira ya Rais na tunafuatilia.

Kiufupi katika hili Zitto hakumsikiliza wala hakutaka kumwelewa JPM. Ametoka kuwa mjenga hoja hadi pingapinga tu. Sasa asome hapa:

Mosi, Kwa nini naamini hakumsikiliza Rais kuhusu issue ya Kangi Lugola. Rais amelaumu mambo 2 kuingiwa mkataba wa mkopo ambao kwa mujibu wa Sheria ya Bunge ya Madeni na Misaada, mkataba huo ulitakiwa ushughulikiwe na Kamati ya Madeni iliyopo Wizara ya Fedha. Kosa la kwanza na Rais alitaja wazi. Zitto anafanya propaganda kwenye facts!

Pili, Rais akazungumzia kosa la "Hata Bungeni" mkopo huo haukupelekwa. Zitto tena hakutaka kusikiliza.

Muktadha wa Rais hapa kwa Sheria ya Bajeti ni kuwa mkopo unapokuwa umepitia hatua zote za Wizara ya fedha (sio kupelekwa mkataba) bali Bunge linahusika kwa maana ya kupitisha mkopo huo kama chanzo rasmi cha mapato katika Bajeti ya wizara na taasisi husika.

Kama ni mradi utaelezwa kuwa utaketewa USD au Euro kadhaa, source inatajwa. Huu ni mfumo wa kawaida wa Bajeti ambao Rais ndio anahoji chanzo cha kina Lugola mbona hakimo hata ktk vilivyoidhinishwa na Bunge? Kosa nini hapo?

Zitto yuko nyuma ya wakati sana, Serikali ya Tanzania ilishaachana na ubabaishaji huu wa kila Wizara au Tasisi kukopa kivyake kwanza inaweza kuleta shida kwenye uchumi maana mikopo hata ya sekta binafsi na taasisi za umma inasomeka kwenye uwiano wa deni la Taifa.

Sasa cha ajabu Zitto huyu huyu anayelalamikaga deni la Taifa linakua na kutaka udhibiti, leo hapa anadhihirisha unafiki wake kwa kumtetea Lugola kuwa kaonewa? Alitaka mkopo ukopwe hivyo kihohela halafu aje apate kete ya kisiasa kuwa deni la Taifa liongezeke aibuke kuponda!!! Kweli Magu Chuma. Watu wanakosa hoja hadi sasa wanakula ubuyu tu

Nimegundua Zitto anapitia wakati mgumu katika utawala huu, hakuna pa kufanya unafiki, kila mahali watu wanasimamia principles. Anataabika.

Lakini licha ya kutomwelewa Rais, pia bado hajaelewa hata muktadha wa hoja. Suala la kina Lugola linahusu mkopo.

Zitto anatoa mfano wa SGR kuwa nayo "haikupita Bungeni," wapi na wapi kwani SGR kuna mtu kakopa? Kakopa wapi? Au ndege? Zimekopwa wapi???Ili hata kama mkataba wake ungetakiwa kupita Bungeni tuseme haukupita???

Ununuzi wa ndege na bajeti za SGR zinapitishwa Bungeni kupitia vifungu vya Bajeti za kila mwaka, Zitto haoni hapo?Au yeye anajua kukataa tu Bajeti hasomi ndani!

Lakini pia Akasome the Government Loans Guarantees and Grants Act (as ammended) na kisha akasome the Budget Act ataziona hoja mbili za Magufuli dhidi ya upuuzi wake.

Hapa ndio naamini yule Zitto mjenga hoja wa enzi za Buzwagi akikutana na huyu Zitto mjenga vihoja wa zama hizi, vita yake itakuwa sawa na vita ya III ya dunia.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
375
1,000
Itakuwa ni hatari kwani Zitto Zuberi Kabwe wa leo amejaa vioja, vitimbi, vituko na muumini wa siasa nyepesi zitokanazo na matukio ili avume tu mitandaoni. Yule Zitto wa Buzwagi na Escrow kumbe naye alifariki na Deo Filikunjombe kwenye ajali ya helikopta huyu sijui katoka wapi
 
mhuri25

JF-Expert Member
Sep 3, 2016
1,876
2,000
Zitto Kabwe ni wakupuuzwa tu!! Yeye kila hoja huwa anachukulia negative tu nakujifanya ana akili sana kuliko WaTZ karibia 40M!!

Typed Using KIDOLE
 
Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
4,327
2,000
Huu uchafu wa Kangi na jinsi Mh Rais alivyousema kwenye hadhira naamini kwa mwendo huu upinzani unaendelea kukosa hoja! Ingekuwa kipindi cha JK hela ingepigwa alafu baadae wakina Zitto ndo wangekuja kuibuka kama vyanzo vya habari.
Mh Rais kamaliza mwenyewe, kaibua na kachukua hatua papo hapo wakati JK angelazimishwa na Bunge.
 
TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
2,000
Nimesoma andiko linalodaiwa kuandikwa na Zitto Kabwe akihoji kama Rais Magufuli amemtumbua Kangi Lugora kwa kusaini Mkataba ambao "haujapita Bungeni," mbona kuna mikataba mingi "haijapota Bungeni" na watu hawajachukuliwa hatua???

Kama kawaida yake Zitto akataja mifano ya yale yale makubwa ya JPM yanayomuumiza kichwa; SGR, ununuzi wa ndege na mengineyo. Anataka tuamini nayo "hayakupitia Bungeni."

Nianze kwa kusema Zitto ameshajenga dhana ya kupinga kila kinachofanywa na Serikali. Hivyo ni kazi yake kupinga lakini asitufanye sisi raia ni wajinga. Tunaielewa dhamira ya Rais na tunafuatilia.

Kiufupi katika hili Zitto hakumsikiliza wala hakutaka kumwelewa JPM. Ametoka kuwa mjenga hoja hadi pingapinga tu. Sasa asome hapa:

Mosi, Kwa nini naamini hakumsikiliza Rais kuhusu issue ya Kangi Lugola. Rais amelaumu mambo 2 kuingiwa mkataba wa mkopo ambao kwa mujibu wa Sheria ya Bunge ya Madeni na Misaada, mkataba huo ulitakiwa ushughulikiwe na Kamati ya Madeni iliyopo Wizara ya Fedha. Kosa la kwanza na Rais alitaja wazi. Zitto anafanya propaganda kwenye facts!

Pili, Rais akazungumzia kosa la "Hata Bungeni" mkopo huo haukupelekwa. Zitto tena hakutaka kusikiliza.

Muktadha wa Rais hapa kwa Sheria ya Bajeti ni kuwa mkopo unapokuwa umepitia hatua zote za Wizara ya fedha (sio kupelekwa mkataba) bali Bunge linahusika kwa maana ya kupitisha mkopo huo kama chanzo rasmi cha mapato katika Bajeti ya wizara na taasisi husika.

Kama ni mradi utaelezwa kuwa utaketewa USD au Euro kadhaa, source inatajwa. Huu ni mfumo wa kawaida wa Bajeti ambao Rais ndio anahoji chanzo cha kina Lugola mbona hakimo hata ktk vilivyoidhinishwa na Bunge? Kosa nini hapo?

Zitto yuko nyuma ya wakati sana, Serikali ya Tanzania ilishaachana na ubabaishaji huu wa kila Wizara au Tasisi kukopa kivyake kwanza inaweza kuleta shida kwenye uchumi maana mikopo hata ya sekta binafsi na taasisi za umma inasomeka kwenye uwiano wa deni la Taifa.

Sasa cha ajabu Zitto huyu huyu anayelalamikaga deni la Taifa linakua na kutaka udhibiti, leo hapa anadhihirisha unafiki wake kwa kumtetea Lugola kuwa kaonewa? Alitaka mkopo ukopwe hivyo kihohela halafu aje apate kete ya kisiasa kuwa deni la Taifa liongezeke aibuke kuponda!!! Kweli Magu Chuma. Watu wanakosa hoja hadi sasa wanakula ubuyu tu😀

Nimegundua Zitto anapitia wakati mgumu katika utawala huu, hakuna pa kufanya unafiki, kila mahali watu wanasimamia principles. Anataabika.

Lakini licha ya kutomwelewa Rais, pia bado hajaelewa hata muktadha wa hoja. Suala la kina Lugola linahusu mkopo.

Zitto anatoa mfano wa SGR kuwa nayo "haikupita Bungeni," wapi na wapi kwani SGR kuna mtu kakopa? Kakopa wapi? Au ndege? Zimekopwa wapi???Ili hata kama mkataba wake ungetakiwa kupita Bungeni tuseme haukupita???

Ununuzi wa ndege na bajeti za SGR zinapitishwa Bungeni kupitia vifungu vya Bajeti za kila mwaka, Zitto haoni hapo?Au yeye anajua kukataa tu Bajeti hasomi ndani!

Lakini pia Akasome the Government Loans Guarantees and Grants Act (as ammended) na kisha akasome the Budget Act ataziona hoja mbili za Magufuli dhidi ya upuuzi wake.

Hapa ndio naamini yule Zitto mjenga hoja wa enzi za Buzwagi akikutana na huyu Zitto mjenga vihoja wa zama hizi, vita yake itakuwa sawa na vita ya III ya dunia. 😀

*MAGUFULI CHAGUO LETU* *#T2020JPM*
 
Fursa Pesa

JF-Expert Member
May 30, 2012
4,122
2,000
Kuna wakati alisema mkimfutilia sana,ataangamiza ukoo mzima hata panya,mende na kunguni......
Siasa zina visa na vihoja,wakati anasema hivyo kumbe kuna mahala watu wanafanya yao.......
Ila Magufuri ni kamanda wa kweli,siku hizi sisikii wanasiasa wakiwatishia watu maisha.
 
ERoni

JF-Expert Member
Jan 9, 2013
30,792
2,000
Hii ndio mnaita "sayansi jamii" ama political science? Neno sayansi hapo lina maana gani? Naona mwingi ni uongo katika hiyo sayansi. Political science is full of lies....
 
Betterhalf

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
2,830
2,000
Na Nathaniel Ndilito, DSM.

Nimesoma andiko linalodaiwa kuandikwa na Zitto Kabwe akihoji kama Rais Magufuli amemtumbua Kangi Lugora kwa kusaini Mkataba ambao "haujapita Bungeni," mbona kuna mikataba mingi "haijapota Bungeni" na watu hawajachukuliwa hatua?

Kama kawaida yake Zitto akataja mifano ya yale yale makubwa ya JPM yanayomuumiza kichwa; SGR, ununuzi wa ndege na mengineyo. Anataka tuamini nayo "hayakupitia Bungeni."

Nianze kwa kusema Zitto ameshajenga dhana ya kupinga kila kinachofanywa na Serikali. Hivyo ni kazi yake kupinga lakini asitufanye sisi raia ni wajinga. Tunaielewa dhamira ya Rais na tunafuatilia.

Kiufupi katika hili Zitto hakumsikiliza wala hakutaka kumwelewa JPM. Ametoka kuwa mjenga hoja hadi pingapinga tu. Sasa asome hapa:

Mosi, Kwa nini naamini hakumsikiliza Rais kuhusu issue ya Kangi Lugola. Rais amelaumu mambo 2 kuingiwa mkataba wa mkopo ambao kwa mujibu wa Sheria ya Bunge ya Madeni na Misaada, mkataba huo ulitakiwa ushughulikiwe na Kamati ya Madeni iliyopo Wizara ya Fedha. Kosa la kwanza na Rais alitaja wazi. Zitto anafanya propaganda kwenye facts!

Pili, Rais akazungumzia kosa la "Hata Bungeni" mkopo huo haukupelekwa. Zitto tena hakutaka kusikiliza.

Muktadha wa Rais hapa kwa Sheria ya Bajeti ni kuwa mkopo unapokuwa umepitia hatua zote za Wizara ya fedha (sio kupelekwa mkataba) bali Bunge linahusika kwa maana ya kupitisha mkopo huo kama chanzo rasmi cha mapato katika Bajeti ya wizara na taasisi husika.

Kama ni mradi utaelezwa kuwa utaketewa USD au Euro kadhaa, source inatajwa. Huu ni mfumo wa kawaida wa Bajeti ambao Rais ndio anahoji chanzo cha kina Lugola mbona hakimo hata ktk vilivyoidhinishwa na Bunge? Kosa nini hapo?

Zitto yuko nyuma ya wakati sana, Serikali ya Tanzania ilishaachana na ubabaishaji huu wa kila Wizara au Tasisi kukopa kivyake kwanza inaweza kuleta shida kwenye uchumi maana mikopo hata ya sekta binafsi na taasisi za umma inasomeka kwenye uwiano wa deni la Taifa.

Sasa cha ajabu Zitto huyu huyu anayelalamikaga deni la Taifa linakua na kutaka udhibiti, leo hapa anadhihirisha unafiki wake kwa kumtetea Lugola kuwa kaonewa? Alitaka mkopo ukopwe hivyo kihohela halafu aje apate kete ya kisiasa kuwa deni la Taifa liongezeke aibuke kuponda!!! Kweli Magu Chuma. Watu wanakosa hoja hadi sasa wanakula ubuyu tu

Nimegundua Zitto anapitia wakati mgumu katika utawala huu, hakuna pa kufanya unafiki, kila mahali watu wanasimamia principles. Anataabika.

Lakini licha ya kutomwelewa Rais, pia bado hajaelewa hata muktadha wa hoja. Suala la kina Lugola linahusu mkopo.

Zitto anatoa mfano wa SGR kuwa nayo "haikupita Bungeni," wapi na wapi kwani SGR kuna mtu kakopa? Kakopa wapi? Au ndege? Zimekopwa wapi???Ili hata kama mkataba wake ungetakiwa kupita Bungeni tuseme haukupita???

Ununuzi wa ndege na bajeti za SGR zinapitishwa Bungeni kupitia vifungu vya Bajeti za kila mwaka, Zitto haoni hapo?Au yeye anajua kukataa tu Bajeti hasomi ndani!

Lakini pia Akasome the Government Loans Guarantees and Grants Act (as ammended) na kisha akasome the Budget Act ataziona hoja mbili za Magufuli dhidi ya upuuzi wake.

Hapa ndio naamini yule Zitto mjenga hoja wa enzi za Buzwagi akikutana na huyu Zitto mjenga vihoja wa zama hizi, vita yake itakuwa sawa na vita ya III ya dunia.

Sent from my iPhone using JamiiForums
Well said mleta hoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom