Kweli zantel !!

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,578
8,600
Kumbe laptop tunazotangaziwa nikanyabwoya!!unatakiwa ukafungue akaunti katika benk ya ABC Bank then upeleke mshahara wako uwe unapita pale ili wakukate makato ya kompyuta utakayokuwa umenunua!!unanunua computer kwa bei zaidi ya ilinayouzwa kwenye soko!!Wizi mtupu!!
 
Kumbe laptop tunazotangaziwa nikanyabwoya!!unatakiwa ukafungue akaunti katika benk ya ABC Bank then upeleke mshahara wako uwe unapita pale ili wakukate makato ya kompyuta utakayokuwa umenunua!!unanunua computer kwa bei zaidi ya ilinayouzwa kwenye soko!!Wizi mtupu!!
Ufafanuzi tafadhali, umeniacha hewani.....
 
Ufafanuzi tafadhali, umeniacha hewani.....

Kuna mikopo ya laptop zantel lakini wanakwambia ukafungue account abc Bank then mshahara wako uwe unapita kule kama wewe ni mwajiriwa!kwa maelezo zaidi nenda kwenye kituo cha zantel.
 
Hukumu Yaitikisa Zantel
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 15th December 2010 @ 07:45 Imesomwa na watu: 254; Jumla ya maoni: 0
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Zanzibar Telecom Limited (Zantel), imetikiswa na pigo la kisheria baada ya kukumbana na hukumu ya kutakiwa kumlipa mfanyabiashara wa Dar es Salaam mamilioni ya shilingi.

Katika kesi Namba ya 305 ya mwaka 2007, Zantel ilishitakiwa na mfanyabiashara Haidari Y. Rashidi wa Kampuni ya Nararisa Enterprises ikitakiwa kulipa fidia ya Sh milioni 53.4 kutokana na kusitisha mkataba wake wa kuiuzia viyoyozi kampuni hiyo ya simu.

Hata hivyo, baada ya mvutano wa kisheria katika mahakama nchini, iliamriwa kuwa Zantel inapaswa kumlipa Haidari zaidi ya Sh milioni 800, badala ya maombi ya mshitaki ya Sh milioni 53.

Gazeti hili limefanikiwa kupata nyaraka za mwenendo wa kesi hiyo ambayo hukumu yake inaelezwa kuwa imeuchanganya uongozi wa Zantel na mawakili wake kutokana na kile kinachoonekana ‘kupaishwa’ kwa malipo hayo kwa zaidi ya mara 15 ya fidia iliyokuwa imeombwa na mdai.

Hukumu iliyompa ushindi Haidari ilitolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Waliarwande Lema.

Uamuzi huo unaelezwa kuunyima usingizi uongozi wa Zantel ambayo hata hivyo iliamua kulipa deni kwa kile kinachotajwa kuwa ni kuheshimu uamuzi wa mahakama, ingawa kuanzia hapo uongozi wa kampuni hiyo ya simu umeelezwa kuwa unahaha kutaka kutenguliwa kwa hukumu husika.


SOURCE: habari Leo.
 
Back
Top Bottom