Hata wao wenyewe CHADEMA walishangazwa na idadi ndogo ya watu waliojitokeza. Amini usiamini, watu walidhani Mwanza pangechimbika na biashara kufungwa.....hakuna lolote magari yalipita kama kawaida, watu waliendelea na biashara na kazi kama kawaida. Maoni ya wengi waliona ni kupoteza muda tu, mtu aache kutafuta riziki yake na watoto aandamane akapigwe jua!
Wengine walisema mbona hao viongozi wa CHADEMA hatujawasikia wakitoa posho au mishahara yao kwa wananchi kama kweli wana uchungu huo? Mbona hawajakataa ile mikopo ya millioni 200, na milioni 90 za magari? Lema anaongea tu, mbona mkopo kavuta?
Watu wamekuwa wajanja, wameona wanatolewa kama chambo, viongozi wakitoka hapo wanakutana Tilapia au TAI FIVE WANAGONGANISHA GLASI ZA MVINYO,,, WALALAHOI WANARUDI MILIMANI AMBAPO HATA UMEME HAKUNA!
Acheni kuwapotezea muda watanzania. Amani iliyopo tuilinde wote.
we ongea kwa kuwa domo lako ni la kifisadi ila tuliokuwepo tuliona hali halisi na idadi ya watu kuzidi wewe unaeongea kwa hisia na mahaba ya kifisadi.