Kweli wabongo washachoka na matatizo!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kweli wabongo washachoka na matatizo!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Babu Lao, Feb 4, 2011.

 1. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #1
  Feb 4, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Wananchi waharibu magari Dar


  WANANCHI wenye hasira kali jana walizingira Barabara ya Sam Nujoma eneo la Mwenge Vinyago kisha kuanza kuvunja vioo vya magari na kusababisha uharibifu wa mali za wapita njia.Kutokana na tukio hilo Jeshi la Polisi lililazimika kurusha risasi hewani ili kuwatawanya wananchi hao.

  Tukio hilo limetokea jana saa 5 usiku, Barabara ya Sam Nujoma eneo la Mwenge.

  Shuhuda wetu amedai kuwa tukio hilo lilitokea baada ya wakazi hao kudai kuchoshwa na ajali zinazotokea mara kwa mara ambapo jana mtembea kwa miguu aliyefahamika kwa jina la Mangushi (45), ambaye ni mchonga vinyago, kugongwa na gari katika eneo hilo na kufa papo hapo.

  Imedaiwa kuwa ajali hiyo ilisababishwa na dereva wa gari dogo aina ya Suzuki Escudo ambaye alitoweka baada ya tukio hilo.
   
 2. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #2
  Feb 4, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  ni habari ya kusikitisha lakini tuangalie ni nini chanzo cha ajali mara kwa mara maana sio high way kubwa sana kama nimepafahamu vzuri pana keepleft hapo au pana hitaji tuta au zebra inakasirisha sana panapotokea ajali sehemu moja mara kwa mara
   
 3. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #3
  Feb 4, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Poleni wafiwa, Serikali ifanye ukaguzi maeneo ambayo ni makazi ya watu iweke matuta.
   
Loading...