Skate Boy
JF-Expert Member
- Dec 15, 2016
- 312
- 204
[HASHTAG]#UNFORGOTTEN[/HASHTAG] TWINS.
Wakati Edward Moringe Sokoine akiwa Waziri mkuu Mwalimu Nyerere alipata ahueni na alinenepa..Huu ndio wakati pekee Mwalimu aliweza hata kupumzika na kunywa Juice huku akiamini anacho kichwa kingine kilichojaa Falsafa zake...Kichwa kinachodhibiti Wapiga dili, Wanyang'anyi,walanguzi na wahujumu wa Uchumi ipasavyo.
SOKOINE anachukuliwa kama Waziri Mkuu Bora wa Muda Wote, ...Kifo chake kilikuwa moja ya mapigo makuu aliyowahi kupata Mwalimu Nyerere akiwa rais,. kwani alimtegemea mno katika kusimamia serikali na Vita dhidi ya Walanguzi na Wahujumu wa Uchumi..Mwalimu Nyerere alilia Machozi hadharani.
Mwalimu alimwamini Sokoine na alimuona kama “pacha wake” kwani wote wawili walisimamia kile walichoamini na walichoishi,
Viongozi wa aina hii hawazaliwi kila mara na hata wanapozaliwa hupingwa na kupigwa Vita vikali.
Leo nimewakumbuka Mashujaa hawa kwa sababu ni vigumu kukumbuka mmoja bila kukumbuka mwingine. Bahati mbaya wote wameshatangulia mbele ya haki. Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi!.