white wizard
JF-Expert Member
- May 18, 2011
- 8,314
- 13,277
Yaani nimeamini kama una ugomvi wa kibiashara na mfanyabiashara mwenzako ,mbinu ambayo itakurahisishia mkakati huo ni kusema kuwa bidhaa hiyo ina punguza nguvu za kiume! na watu wakaamini hivyo utakuwa umemumaliza mshindani wako.
Hili suala kipindi cha nyuma lilishawahi kutokea kwenye ile juice ya super dip kwa wale wanayoikumbuka paketi moja unachanganya na maji ndoo moja. Ilitokea kupendwa sana miaka hiyo, pale waliposema kuwa inapunguza nguvu za kiume tu ndio ikawa mwisho wake!
Mfano mwingine ni hivi vyandarua vinavyogawiwa na serikali, watu wanavichukua na kuviweka ndani tu, na wengine wanatumia kuvulia samaki! kisa vinapunguza nguvu za kiume, na hata watoto wa kiume wameshakatazwa na wazazi wao kuvitumia.
Kuna sehemu moja nimekwenda wameshahamia kwenye hizi AZAM COLA, wanasema nazo zinapunguza nguvu za kiume! eti kutokana na gesi iliyomo, kwani soda gani kila uifunguapo gesi haiishi! Mpaka wiki bado inafuka gesi!
KWELI WA AFRIKA TUNAJARI SANA ILE "KAZAENI MUONGEZEKE".NA KIBAYA ZAIDI WATU WAKISHA JAZWA FIKRA HIYO KUWA BADILISHA TENA UFANYE KAZI TENA YA ZIADA