Kweli Ujana maji ya moto, mtoto amtukana baba yake

Maguge Maguge

JF-Expert Member
Sep 1, 2016
2,734
1,774
Juzi tr 25/12 siku ya kusherehekea krismas kabisa, katika hali isiyokuwa ya kawaida, kijana mmoja wa kiume miaka 19 alifukuzwa na baba yake baada ya kumtukana baba yake eti ni mse..ge, kule tabata.

Tendo la mtoto kumtukana baba yake hivo kwa kuwa tu eti mtoto hapendi kazi za baba yake wakati kamtunza hadi umri huo, nilichukulia kama ni ujana.

Lakini nilibaki na swali.

Hivi baba yake kumfukuza alifanya sawa?

au alitakiwa kumsamehe kama mtoto wake?

naomba mchango wa mawazo yako katika hili
 
Uyo dogo alipaswa kupata kipigo cha mbwa mwiz ila ni ngumu kushaur sana sababu huwez jua mzee anamlea vipi mwanae
 
Kwanini usihoji uhalali wa kijana wa miaka 19, umri unaohesabika kuwa ni wa mtu mzima, kumtukana Baba yake tusi zito kama hilo? Kwanini asifukuzwe kwa kosa hilo? Anafanya nini hapo kwa wazazi wake wakati kwa umri alionao anapaswa kujitegemea?
 
Wengine wanawatukana wazazi wao waliowalea vizuri kwa taabu, wengine sisi hatujui hata sh. 10 ya Mzee toka tuzaliwe. Kweli dunia haiko fair.
Huyo Dogo ilitakiwa asogezww hapo mlimani city ya Segerea.
 
Back
Top Bottom