Kweli Ujana maji ya moto, mtoto amtukana baba yake

Muda mwingine malezi nayo yanachangia kuharibu watoto na sifikirii kuwa huyo kijana ameanza leo huenda ikawa alianza kidogo kidogo mwisho wake ameshazoea.

Kumfukuza huenda ikasaidia kumbadilisha na pia kwa upande mwingine inaweza ikazidi kumuharibu kabisa.

Pia hilo ni funzo kwa wazazi kwamba mtoto anatakiwa alelewe katika njia zilizo sahihu na zenye faida mbele ya jamii mana kama baba yake kamtukana je kwa mtu baki itakuwaje?
 
Tatzo ukipiga mtoto unashtakiwa na UMMA ukisema HaYa nimwache Unatukanwa kama Hvi unalaumiwa kwa Malezi MabaYa .....usimnYime mtoto mapigo 19 Yrs unamkunja vizur tu
 
Kitendo cha dogo kumtukana mzee wake, tendo la kuvunja heshima sana.

Sasa ngoja aingie mtaani akapambane na life, akizubaaa yeye ndio atakuwa msnge kweli.

Mimi nisinge ishia hapo, ninge waambia wana ndugu, ambaye ata msapoti huyu dogo ,maana yake wameungana kunitukana.
 
Huku ni kuonyesha kuwa ndani ya familia Kuna kasoro kubwa kimaadili, huyo baba ni tatizo na mtoto ndo zaidi wanahitaji msaada na unasihi wa kutosha
 
Huku ni kuonyesha kuwa ndani ya familia Kuna kasoro kubwa kimaadili, huyo baba ni tatizo na mtoto ndo zaidi wanahitaji msaada na unasihi wa kutosha
Kweli hapo utakuta mama anamdharau baba na anampenda litoto hilo. Usishangae ukikuta kesho yake yupo hapo nyumbani. Kwa kawaida mama ni dira ya watoto hasa wa kiume, mama akikudharau jua hata watoto wanakudharau mara mbili. Mama akikuheshimu mbele za watu, piga ua watoto watakuheshimu.
 
Sema tunatofautiana Mimi nimetoka kwetu kwa amani tu nilipotimiza miaka 17 baada Ya kumaliza kidato cha nne elimu nyingine Ya juu nimejisomesha Mimi mwenyewe.
Inasikitisha kuona mtu Anamiaka 20+ Bado anakaa kwao Kama mtoto wa kike ni sawa kabisa...!!
 
Juzi tr 25/12 siku ya kusherehekea krismas kabisa, katika hali isiyokuwa ya kawaida, kijana mmoja wa kiume miaka 19 alifukuzwa na baba yake baada ya kumtukana baba yake eti ni mse..ge, kule tabata.

Tendo la mtoto kumtukana baba yake hivo kwa kuwa tu eti mtoto hapendi kazi za baba yake wakati kamtunza hadi umri huo, nilichukulia kama ni ujana.

Lakini nilibaki na swali.

Hivi baba yake kumfukuza alifanya sawa?

au alitakiwa kumsamehe kama mtoto wake?

naomba mchango wa mawazo yako katika hili
Huyo mtoto akili yake ni sawa na ya yule mbunge wa upande ule ambaye Yuki kule kwa sasa
 
Nashukuru kwa michango yenu, mliyotoa na mnayoendelea kutoa, lile swali kwangu lilikuwa tata sana.

Kwa upande mwingine

Hongera Founder wa JF MR MAX na washirika wako, kwa kumiliki chombo cha namna yake, chenye uwezo na nguvu ktk kuimarisha mijadara yenye maudhui tofauti tofauti katika jamii ya ki Tanzania.

Hata ukikatishwa tamaa Tumia mbinu zote kukifanya chombo chetu kibaki salama, penye neema hapakosi wawanga!
 
Kuna kitu kimoja napenda sana kujifunza kupitia kwa watoto wadogo ,kabla ya kumuhukumu huyo dogo hebu tupe ukweli ,huwezi kuitwa mssenge kwa kazi unayofanya kuna kitu kipo nyuma ya pazia
Mwisho kunapotokea tatizo jaribu kujiuliza what's wrong with me kabla ya kubebesha wengine mizigo yako
 
Kuna kitu kimoja napenda sana kujifunza kupitia kwa watoto wadogo ,kabla ya kumuhukumu huyo dogo hebu tupe ukweli ,huwezi kuitwa mssenge kwa kazi unayofanya kuna kitu kipo nyuma ya pazia
Mwisho kunapotokea tatizo jaribu kujiuliza what's wrong with me kabla ya kubebesha wengine mizigo yako
Mkuu,
kuna mambo hayafai kuwekwa kwenye mijadala, hasa yale yenye maslahi binafsi.
kama kungekuwa na kitu nyuma ya pazia jambo hili lingekuwa na maslahi binafsi.

ila kwa hili kila mtu anaweza kujifunza kitu.

jambo hili lipo kama lilivyoelezwa, wala halina kitu unachoita kuwa nyuma ya pazia.
hizo ni dondoo za uhakika kutoka kwenye tukio
 
Siku zote kabla ya kutatua tatizo ni vizuri kujua chanzo cha tatizo, nadhani baba mzazi anatakiwa ajiulize chanzo cha hilo tatizo ni nini?

Mtoto kumtukana mzazi aliyemuhangaikia toka akiwa mdogo mpaka mkubwa ni kitendo kinachomchukiza sana mwenyezi Mungu,

Siwezi kushangaa huenda mama kamwambia mwanae kua "huyu sio baba yako mzazi" japo hiyo kauli haijustfy kumtukana mtu aliyekulea kwa miaka 19,

Mtoto aombe msamaha kwa baba yake,baba nae hana budi kusamehe na maisha yaendelee.
 
Back
Top Bottom