Kweli Tanzania kutumia shilingi trilioni 1.7 kununua ndege?

Wastaafu hawapati stahiki zao kutokana na 'watu hawa' kuhujumu fedha zao kununulia mindege isio na faida kwao.
Wanafunzi wanakosa madarasa na madawati kwa matumizi ya hovyo kabisa kama haya!
Cha kusikitisha tunapewa mkopo na WB shs 1.3 trilioni, tunafurahia na kushangilia bila aibu o_O
 
..tatizo shirika la ndege ni biashara kichaa?

..atcl ina mzigo mkubwa sana wa madeni.

..pia atcl imekuwa ikiingiza hasara mwaka hadi mwaka.

..kwanini hayo matrillion yasielekezwe kwenye sekta zinazogusa Watz wengi mfano kilimo, mifugo, badala yake tunaenda kununua midege toka kwa MABEBERU?
Mkuu hizo ndege zinachagiza ukuaji wa uchumi kwa njia ambayo mimi na wewe hatuioni. Ni rahisi kulalama humu jukwaani lakini kivitendo ndege zinahitajika sana haswa kwenye sekta nzima ya utalii.

Kuna mkataba wa kibiashara umetiwa saini kati ya Ubelgiji na Tanzania. Watalii watafuatwa moja kwa moja Brussels na kuletwa bongo. Kuna mikataba kama hiyo iliingiwa na Tanzania enzi zile za hayati JPM, muda sio mrefu itaanza kufanya kazi.

Ndege zinaifungua Tanzania kuliko aina nyingine ya usafiri. Kumbuka Mama anapigia debe uwekezaji uweze kukua, nchi inavyofunguka ndivyo mzunguko wa pesa unavyozidi kuimarika.
 
..nakuheshimu sana, but I disagree.

..you can not convince me ukizingatia HASARA ambayo Atcl inaliingizia taifa kila mwaka.

..pia hakukuwa na shida kwa watalii kufika Tz kiasi cha kulazimisha tununue ndege zetu wenyewe.

..kama ni suala la kuifungua nchi ningependelea sekta za kilimo na viwanda zipewe kipaumbele kupitia uwekezaji na uwezeshaji mkubwa wa serikali kama huu uliofanyika ktk ununuzi wa ndege.
 
Back
Top Bottom