Kweli Tanzania hakuna Pesa?: Huyu ndiye Mtanzania anaemiliki Gari la Tsh Bilioni Moja

Achana nae mzushi tu huyo nyumbani kwake hapo
cbk

hizo ni councel flat ambazo zipo moja ya deprived areas in london (mitaa ya dagenham hiyo ndio mitaa wabongo weengi wapo huko).

By the way chilisosi toa post code yako.
tatizo unatoa mapovu mno kaka, mie sijakataa kuwa huyu mtu ana hela ila sikubaliani na thamani ya gari alilotaja, gari lake ni la 2004 na unaweza kupata hata kwa £25,000 kumbuka mie sijasema nina hela kama mosha. nimepinga thamani, narudia tena jamaa ana hela ila thamani ya gario kadanganya mafala kama wewe, hebu nenda autotrader uone bei
 
Hivi hizo bei zenu za magari huwa mna-quote kutoka wapi mbona zinakuwa kubwa mno kutokana na uhalisia wenyewe angalia hapo bei za lambo Used LAMBORGHINI GALLARDO Car for Sale - Auto Trader UK (na hiyo tena kama unasafirisha unadai vat yako kwa maana hiyo ni cheaper zaidi).

Hivi huyo mwandishi anajua hata mshahara wa Rooney kwa wiki? hadi Lambo imsumbue kichwa au hata lowest wage ya mchezaji wa Man Utd, hivi mbona vitu vidogo sana kwao wao.

tatizo unatoa mapovu mno kaka, mie sijakataa kuwa huyu mtu ana hela ila sikubaliani na thamani ya gari alilotaja, gari lake ni la 2004 na unaweza kupata hata kwa £25,000 kumbuka mie sijasema nina hela kama mosha. nimepinga thamani, narudia tena jamaa ana hela ila thamani ya gario kadanganya mafala kama wewe, hebu nenda autotrader uone bei
tazama ulivyokuwa mwerevu ungepitia thread yote ungeona kwenye first page watu walishapinga hiloooo loooongi. Halafu sijui matusi yanini.
 
Hakuna biashara halali aliyoifanya huyo ya kupata fedha za kuchezea namna hiyo, AS HIS NAME IMPLIES, Mosha, MUSHI, MASAWE, TEMU,.....,.....,...?! Chezea watu hawa wewe? I'm in doubt!

Mie kwa kifupi nawafagilia sana wachaga hasa hayo majina uliyotaja,
Tanzania kuna makabila ambayo kwa kifupi upende usipende hawa jamaa wanaamini lazima wawe matajiri at any cost na most of them wanafanikiwa
WAKINGA,
WACHAGA
 
tazama ulivyokuwa mwerevu ungepitia thread yote ungeona kwenye first page watu walishapinga hiloooo loooongi. Halafu sijui matusi yanini.

Hapo nimekusoma kaka,
Mie jamaa namfahamu vizuri na tumekutana naye mara kadhaa, na kama mapedeshee wote naye anapenda sana kusifiwa, hiyo gari anayoendesha mie mwenyewe naipenda na nadhani ni my next car, nimekubali makosa sikusoma thread za mwanzo.
AM SORI MA BLADA
 
Mi nafikiri ni ushamba tu na tamaa za kijinga kuwa na gari kama hilo Tanzania.
 
Wana Jamiiforums huwa tunapenda kusaili kila taarifa au data zinazobandikwa humu na wana-Jamiiforums wenzetu. Katika kudadafu na kusaili intaneti nimepata kijimwanga kuwa Lamborghini bei ya juu kabisa used ni £ 155,000 hivi, sawa na kama Tshs. 300 millioni ya ki-Tanzania kwa bei za modeli zote gonga hapo chini ktk linki:

lamborghini_gallardo_1_m.jpg

Bei £ 85,000.

Modeli zingine bei zake gonga hapa chini:

Used Lamborghini Gallardo Price Guide - Lamborghini Gallardo Average Car Prices by Year
http://www.buyyourcar.co.uk/used-car/lamborghini/page/3
 
Hapo ndipo penye tatizo Tanzania, hata ukiweza watasema umebebwa, ukikosa pia watakutafutia jina, ni lipi jema kwa Tanzania? Bw. Mosha siyo mwasiasa ana biashara zake, anunua gari anayoipenda, tunashangaa na kuanza kuuliza kapata wapi hiyo hela.

Mitazamo hii ndiyo inayoturudisha nyuma siku zote ndugu zangu tubadilike. Hapo hakuna aliyelalamika kaibiwa na Mosha, kwa hiyo ni jasho lake hilo, tumpongeze na sisi tujifunze ili tuwe na nyumba nzuri, watoto wasome vizuri, tununuwe usafiri wa size yetu n.k siyo lazima vifanane na vya Mosha maana haujui aliko anzia.
 
Kama kuna baadhi ya viongozi wa Yanga wa ngazi zingine walikuwa wanalalamika kutokulipwa pesa zao.......yeye ndo aibuke na faranga kwenye hiyo nyanja, tena kihalali?? Hapana NO!!

Hapo in red,
Sikatai kuwa kuna watu wenye pesa na wengine wanaweza kuwa wamezipata kiuhalali.
But, why wengi wali 'lay low' baada ya maneno ya EPA.....as per your say?
Ama kweli Tanzania ni shamba la mwendawazimu na hakuna anayeuliza kilichovunwa! Laiti ingekuwa katika nchi makini, angefuatiliwa hata amezipataje fedha hizo na analipa kodi kiasi gani? Lakini si katika hii Tanzania ya CCM ambapo Usalama wa Taifa, Polisi na Takukuru wako bize kuwawinda, kuwapeleleza, kuwakaba wanaoikosoa serikali, kuwateka nyara, kuwatesa kuwasumbua na hata kuwaua ili "chama chetu" kidumu milele. Mimi ni mmoja wa wasioamini kwamba fedha ya kijana huyu imepatikana kihalali, sawa na ya kina RA, Chenge, EL na Manji, Riz1 na mamia kadhaa wanaojificha nyuma ya pazia la u-CCM.
 
Wana Jamiiforums huwa tunapenda kusaili kila taarifa au data zinazobandikwa humu na wana-Jamiiforums wenzetu. Katika kudadafu na kusaili intaneti nimepata kijimwanga kuwa Lamborghini bei ya juu kabisa used ni £ 155,000 hivi, sawa na kama Tshs. 300 millioni ya ki-Tanzania kwa bei za modeli zote gonga hapo chini ktk linki:

lamborghini_gallardo_1_m.jpg

Bei £ 85,000.

Modeli zingine bei zake gonga hapa chini:

Used Lamborghini Gallardo Price Guide - Lamborghini Gallardo Average Car Prices by Year
Used Lamborghini Cars For Sale
Asante sana mkuu, kumbe jamaa kaingizwa mkenge! kumbe Lombarghini iliyotumika inapatikana as low as 60,000 British Pounds!
 
Tatizo bongo stori za kujiandikia nyingi sana,
Huyu jamaa namfahamu vizuri, hela anazo na kajikita sana kwenye transport na kikubwa kilichomuinua ni mikopo mikubwa ya benki, ana akili na conection za kucheza ambazo hata wewe ukiipata chance tumia.
Lakini hili gari lake sio la bilioni moja kama anavyodai, hii ni kujitakia maujiko yasiyo ya lazima, sikatai anazo lakini gari lake kwa thamani ya sasa uk ni £30,000 sawa na shs 100,000,000 nusu ya bei ya shangingi la mbunge
soma link hii hapa chini uone bei za ma lambo
Used LAMBORGHINI Car for Sale - Auto Trader UK

halafu soma hili tangazo chini
2 Doors, Manual, Coupe, Petrol, Metallic White. LAMBORGHINI Murcielago LP 640, 2 Doors, 56,000 miles, White. Lamborghini Murcielago Replica based on Toyota MR2,. IM NOT LOOKING FOR ANY OFFERSSS, WHITE WITH RED LEATHER SEATS, SO PLEASE DONT WASTE MY TIME, SAT/NAV, TELEVISION, CD/MP3 PLAYER, ONLY THE NUMBER PLATE WORTH 25000 POUNDS, ALOT TO MENTION BETTER TO COME N SEE URSELF. 10 MONTHS MOT, 6 MONTHS TAX, PART EXCHANGE WELCOME, TAVISTOCK STREET, DUNSTABLE, LU6 1NE. £29,999 call +44(01582) 639916
siyo mnakuwa mnadanganywa halafu mnakubali kwa sababu mwenzake kaisha litumia hivyo atakuwa kamuuzia kama milioni sitini tu
Tuko wengi tunaoendesha magari ya kifahari hivyo tunazijua bei zake
Acha kujisifia na kuleta ujuaji humu, 60mil 4 lambo-jini c hata juma nature na masharo baro wote wanaopenda mitumba kama ya karume wangemiliki!!?
 

Ha ha ha ha ha ha! Sio mawaziri tu Mkuu. Hata waheshimiwa wabunge wetu wakopeshwe. Litawasaidia sana kuwahi vikao mbali mbali majimboni kwao pamoja na kukutana na wapiga kura wao na wakati huo huo kuwahi vikao vya kamati na bodi mbali mbali jijini Dar es Salaam ambako pia ni wajumbe. Pia litawasaidia sana kutoa misaada kwa wajazito hasa wakati wa kujifungua majimboni kwao. Kwa kweli lina hadhi ya 'uheshimiwa'. V8 wapewe madiwani.

Magari hayo yanawafaa zaidi polisi kukimbiza majambazi, fuso za mchanga, waendesha magari kwa kasi n.k.

Pia wapatiwe walimu hasa wa shule za kata kama incentive ili waongeze kiwango cha ufaulu mashuleni
 



HII sasa ni kufuru! Hivi ndivyo utakavyoweza kusema kwa Davies Mosha ambaye ni makamu mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Yanga, ambaye nafasi yake kwa sasa klabuni hapo inashikiliwa na Clement Sanga.


Kwa tafsiri ya haraka, yawezekana Mosha anaweza kuwa ndiye kiongozi pekee wa soka nchini kumiliki gari la kifahari na lenye gharama kubwa aina ya Lamborghini kama ambalo linamilikiwa na mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney.​


Gari analomiliki Mosha ambalo lina rangi ya njano, linaaminika kuwa miongoni mwa magari yenye thamani kubwa siyo tu Tanzania na Afrika, bali duniani kote, kwani hata siku Rooney alipolinunua wenzake wengi hawakutegemea, siyo kwa sababu hana fedha, ila kwa kuwa hakuwa mtu wa matumizi ya magari yenye thamani kubwa kama hilo.​


Mosha ameliambia Championi Ijumaa kuwa anamiliki magari kadhaa ya kifahari kwa matumizi yake binafsi na familia yake.​



Yafuatayo ni maelezo kuhusiana na gari hilo la kifahari kwa kuanzia kiwango cha mafuta na usumbufu anaoupata akiwa katika mizunguko yake.


Ameinunua kwa bei gani?



Kutokana na ubora wa gari hili, nililazimika kutoa shilingi bilioni moja kwa ajili ya kulinunua, kama unavyojua ni fedha nyingi, nimenunua kwa mapenzi yangu.



Alipolinunua



Hili gari kaniuzia mtoto wa Bakhresa (Yusuph), baada ya kufikia makubaliano kati yake na mimi, aliniuzia Julai 2011.


Spidi ya gari



Hili gari kasi yake ya mwisho ni 360, ni kasi kali na inatosha kwa matumizi yangu binafsi.



Matumizi ya mafuta



Matumizi ni ya kawaida wala siyo ya kuogopesha sana, inategemea na umbali utakaotembea.

Usumbufu anaoupata


Usumbufu mkubwa ninaoupata kiukweli, nikiwa naendesha barabarani, madereva wengine wanalishangaa sana, hali inayosababisha kutokea ajali au msuguano mara kadhaa.

Hivi karibuni dereva mmoja aliigonga sehemu ya tairi la nyuma kushoto kutokana na kuishangaa, ilikuwa maeneo ya Masaki hapahapa Dar es Salaam.


Matengenezo yake yaligharimu pauni 20,000 (zaidi ya shilingi milioni 50), hali iliyosababisha niwe makini nikiwa naendesha, anasema Mosha.



Matengenezo yake yaligharimu pauni 20,000 (zaidi ya shilingi milioni 50), hali iliyosababisha niwe makini nikiwa naendesha, anasema Mosha.












Jee na hicho kiti alichokalia hapo kina thamani gani?
Maana kuna mtu kaniambia kwamba hicho kiti bei yake ni 150ml!
 
napingana na wote, bongo hakuna bugati, mie niko UK na zimeuzwa 25 tu hapa zikionekana kila mtu anapigania apige nayo picha

Mkuu JF sio sehemu ya porojo ebu weka evidence ya hayo maneno yako.
 
barabara pekee anaweza endesha speed angalau 220 ni kutoka chalinze kwenda moro tena kibande kidogo tu. huko kwingine atapasuliwa na akina air msae sijui simba mtoto n.k
 
jitume utaipata tu mkuu, hakuna uchawi..ni jitihada binafsi na kutumia nafasi vizuri
 
Wanasema alikuwa kiongozi wa "Young Africans" AKA "kandambili"Nthen kwamba gari kalinunuwa kutoka kwa mtoto wa Bakhressa,so wote sijui kama wana uhusiano na chukua chako mapema AKA. Gamba?That's another topic,navyojuwa kuna watu wana pesa bongo,however wengi wali "lay low" mara baada ya ile maneno ya epa na ingine.
..Haishangazi sana jamani lazima itakuwa used hiyo gari.Hiyo bi ya 1Bilion ni bei kutoka kiwandani so si rahisi huyo mtoto wa bakhresa ainunue 1b na yeye auze kwa bei hiyo. Sema huyo Davis Mosha naye bado limbukeni anataka kujifagilia tu....ametokea kwenye uchakachuaji wa mafuta huyo na kampuni ya TIOT na ni fundi bomba pia..!!!
 
Back
Top Bottom