Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kitu kinachokushindwa kuelewa ni kuwa magari hayo yanapokuwa ya mtumba yanakuwa ni rahisi sana, kama unabisha "google" halifiki kabisa bei hiyo usitake kuchakachuwa.
Hivi kwanini mnapenda kusema uongo?
maneno ya kikafiri haya!Kuna watu wanaishi bwana apa bongo, sie wengine tunaigiza tu
Mkuu yeye ritz1 anamiliki lakeSi tuliambiawa humu JF kuwa hicho kituo cha mafuta cha Ridhiwan.
Si tuliambiawa humu JF kuwa hicho kituo cha mafuta cha Ridhiwan.
Kiukweli hiyo ni gari nzuri na ni gari ya gharama, ila sio kweli kuwa hiyo ndio most expensive hapa bongo!,
Nimeona kuna mtu ana Bugati, kuna mtu ana Ferrari, kuna mtu ana Carrera, kuna mtu ana Mc Laren!. Bongo nasi tupo tupo, umasikini uliotopea ni kwa wengi wetu na utajiri uliotukuka ni kwa wachache wetu.
HII sasa ni kufuru! Hivi ndivyo utakavyoweza kusema kwa Davies Mosha ambaye ni makamu mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Yanga, ambaye nafasi yake kwa sasa klabuni hapo inashikiliwa na Clement Sanga.
Kwa tafsiri ya haraka, yawezekana Mosha anaweza kuwa ndiye kiongozi pekee wa soka nchini kumiliki gari la kifahari na lenye gharama kubwa aina ya Lamborghini kama ambalo linamilikiwa na mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney.
Gari analomiliki Mosha ambalo lina rangi ya njano, linaaminika kuwa miongoni mwa magari yenye thamani kubwa siyo tu Tanzania na Afrika, bali duniani kote, kwani hata siku Rooney alipolinunua wenzake wengi hawakutegemea, siyo kwa sababu hana fedha, ila kwa kuwa hakuwa mtu wa matumizi ya magari yenye thamani kubwa kama hilo.
Mosha ameliambia Championi Ijumaa kuwa anamiliki magari kadhaa ya kifahari kwa matumizi yake binafsi na familia yake.
Yafuatayo ni maelezo kuhusiana na gari hilo la kifahari kwa kuanzia kiwango cha mafuta na usumbufu anaoupata akiwa katika mizunguko yake.
Ameinunua kwa bei gani?
Kutokana na ubora wa gari hili, nililazimika kutoa shilingi bilioni moja kwa ajili ya kulinunua, kama unavyojua ni fedha nyingi, nimenunua kwa mapenzi yangu.
Alipolinunua
Hili gari kaniuzia mtoto wa Bakhresa (Yusuph), baada ya kufikia makubaliano kati yake na mimi, aliniuzia Julai 2011.
Spidi ya gari
Hili gari kasi yake ya mwisho ni 360, ni kasi kali na inatosha kwa matumizi yangu binafsi.
Matumizi ya mafuta
Matumizi ni ya kawaida wala siyo ya kuogopesha sana, inategemea na umbali utakaotembea.
Usumbufu anaoupata
Usumbufu mkubwa ninaoupata kiukweli, nikiwa naendesha barabarani, madereva wengine wanalishangaa sana, hali inayosababisha kutokea ajali au msuguano mara kadhaa.
Hivi karibuni dereva mmoja aliigonga sehemu ya tairi la nyuma kushoto kutokana na kuishangaa, ilikuwa maeneo ya Masaki hapahapa Dar es Salaam.
Matengenezo yake yaligharimu pauni 20,000 (zaidi ya shilingi milioni 50), hali iliyosababisha niwe makini nikiwa naendesha, anasema Mosha.
Matengenezo yake yaligharimu pauni 20,000 (zaidi ya shilingi milioni 50), hali iliyosababisha niwe makini nikiwa naendesha, anasema Mosha.
chanzo:http://www.globalpublishers.inf
Which club, Young Africans?!?Uki-Google Davies Mosha, utapata habari kumhusu huyo jamaa Mjasiriamali. Anamiliki hii kampuni www.delinagroup.com Profile yake hio hapo: Davis Mosha lives a fulfilling life by doing what he loves best: business, rallying and football. He is an entrepreneur, a rally driver and owns a football club in Tanzania, his motherland.
Mama mdogo,
Bei ya Bugatti Veyron ni kubwa zaidi ya hiyo. Wengine wanasema ni zaidi ya Milioni kumi US $.
Kiwanda cha VolksWagen (People's Car) huwa wanatengeza ili kuonyesha UBABE kuwa wakitaka, wanaweza.
Hupunguza bei kwa makusudi ili watu wanunue kirahisi ikiwa na maana wanauza kwa hasara.
Hii hupelekea KAMPUNI na MASHIRIKA yote duniani KUGOMA kutoa BIMA ya aina yoyote kwa hili gari. Wanagoma kwa sababu ukitaka kuweka bima, utasema umenunua kwa hiyo bei wakati likiharibika, wanaenda pambana na Spare parts ghali mara tano ya bei hiyo.
Ndiyo maana wananunua watu ambao pesa kwao si tatizo. Pia ulaji mafuta wa hii Veyron si mzuri kabisa kwani linafikisha hadi zaidi ya 500 Horse Power, nguvu inayotosha kuzalisha umeme wa kutumika hapa Sikonge pote.
Kama humjui huyu jamaa ndio operation manager wa Riz KKT anasimamia na hoteli anayoijenga hapa kibaha mbele ya mail moja pia kuna kituo cha mafuta na figure ya twiga na nyati so bado ni ufisadi uleule wa JK+Riz=moshaHawa ndo wanaochanganya mafuta na maji ili wamaximize profit!
Wabongo wee waache tuu, kuna mtu namfamu hapa hapa bongo, anamiliki cruise ship, anamiliki jet, na yuko very low profile ndugu zake ndio matanuzi na kujitapa kutwa kucha!. Huyo mwenye Bugati sio hiyo Veylon bali ni Mama mmoja wa Kiarabu, mwenye Ferrari ni yule mhindi wa rada, Mwenye McLaren ni mswahili mwenzetu!. Bongo tuna tajiri wetu mmoja anayependwa kujatwa tajwa sana kwenye nyimbo, huku amejisheheneza kwa micheni kibao na mipete ya almasi, ile Hummer zimetoka tuu akanunua, walipotoa latest version, akanunua tena na walipotoa hii version ya sasa, kanunua tena, anazo 3 ili kuonyesha jeuri ya utajiri!. Wakati hao wakionyeshea, wako matajiri wa ukweli, wanamiliki mpaka visiwa!, wamejinyamazia kimya kabisa na account zao ziko Credit Sussie zimejituliza tuli!.Ngosha, unamaanisha kama hilo juu Bugatti Veyron?! Mtu analo bongo?! Kama ndiyo, wabongo ni 'balaa'.
Mh! Maana unyamwezini hata kina Diddy et al. wengi wanayafanyia shooting tu ngosha!!
Ngosha hizo gari toka zianze kutengenezwa mwaka 2005 hadi mwaka jana, zilikuwa zimeuzwa 300 tu dunia nzima!