Kweli tabia ya mtu ni kama ngozi yake, ni vigumu kuibadili. Bashiru na Polepole ni mfano hai

Major

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2007
Messages
1,867
Points
2,000

Major

JF-Expert Member
Joined Dec 20, 2007
1,867 2,000
Umaarufu wa Pole pole ulikuja kutokana na umahiri wake kifikra na namna ya ujengaji hoja wake ulivyokuwa makini na ukweli ambao watu wengi sana duniani hupenda kusikia. Hili lilidhihirika wakati wa mchakato wa kuunda katiba mpya na kuanzia hapo ndipo Pole pole alianza kujulikana. Kabla ya hapo hakuna aliyekuwa anamjua Pole Pole. Kwa hiyo sifa kuu ya Pole pole wa Enzi za katiba Mpya ilikuwa ni Ukweli.

Pole pole wa Leo Amebadilika kabisa. Ameamua kuwa mfuasi wa uongo, lakini cha Ajabu ukimtizama ktk hotuba zake, ile body language, unamuona kabisa ni Kama mtu asiye na raha moyoni. Hata akiongea ni Kama anapayuka payuka tu. Anaonekana Kama mtu aliyepoteza vitamini fulani ktk mwili wake. Hata ukiona anavyowahutubia watu ni Kama watu wanamshangaa badala ya kumshangilia.

Ndugu Bashiru Katibu mkuu ndiyo kabisa. Huyu ni mtu Mcha Mungu wa Kweli. Na anajua kabisa uongo ni dhambi na Chukizo Kwa Mungu. Huyu mpaka sasa bado hatabiriki, labda kwa sababu bado ni mgeni au bado hajaamua kudanganya wazi wazi, lakini kwa Mimi ninavyoona na kwa namna ninavyomjua huyu Bwana ktk Misimamo yake, huwa siyo mtu wa kubadilika kabisa.

Hata ukiangalia body language ya huyu Bashiru ni Kama hata hicho cheo alichopewa ni kama amelazimishwa tu kwa Sababu anajua Mwisho wa Siku lazima Ageuke na kuwa Mfuasi wa Shetani wakati sasa hivi ni Mfuasi wa Mungu.nilimuona Jinsi alivyomshukia Makonda kule Kilimanjaro wakati wa mazishi ikanipa picha kubwa sana.kwa sababu Kwa ninavyojua ktk Nchi hakuna Mwenye uwezo wa kumkemea Makonda. Hata JPM mwenyewe Hana uwezo wa kumkemea. Lakini ni Dhahiri Makonda anamuogopa Bashiru kuliko JPM .

Haya mambo madogo madogo yanayotokea Kati ya Kachero Membe na Bashiru, Nina Imani ni ya muda tu, na hata ukiangalia kwa makini utaona kabisa hakuna popote Bashiru aliwahi kumtaja Membe moja kwa moja zaidi ya mafumbo tu. Na ni dhahiri Bashiru anajua kwamba Membe Hana kosa lolote kikatiba ya chama iwapo ataamua kugombea 2020. Tabia ya mtu ni Kama ngozi ya mwili mwili wake. Kuibadili ni kazi kubwa sana. Ukilazimisha, ndiyo unapata matokeo kama ya Polepole, kutoka kuheshimiwa hadi kuwa Kama kituko ktk jamii.
 

BEHOLD

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2013
Messages
5,036
Points
2,000

BEHOLD

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2013
5,036 2,000
NJAA HAIJAWAHI KUMUACHA MTU SALAMA
Mbele ya njaa na ukosefu wa hekima dhabiti, utu na nafsi ya MTU hupoteza thamani. Tupo hapa tulipo kwa sababu ya NJAA.
 

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Messages
1,292
Points
2,000

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2019
1,292 2,000
wote wanasema kweli juu ya CCM kwamba CCM itashinda miaka mingi ijayo. Wote ni waumini wa Ujamaa ambao CCM inauamini.

personal life yao hao siijui hivyo sijui lolote kutoka kwao zaidi ya hayo mawili wanayoamini
 

kinje ketile

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2015
Messages
454
Points
1,000

kinje ketile

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2015
454 1,000
Badala ya kuwawaza watu...! Inatubidi tuwe serious kidogo,Embu tuwe tunakuja na idea nzito jinsi ya kushika dola uchaguzi ujao ..! La sivyo tutakua tunaishia Kushinda vitongoji na kwa uchache ubunge..C'mon PipoozzziiiiPawaaa..!
 

Major

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2007
Messages
1,867
Points
2,000

Major

JF-Expert Member
Joined Dec 20, 2007
1,867 2,000
NJAA HAIJAWAHI KUMUACHA MTU SALAMA
Mbele ya njaa na ukosefu wa hekima dhabiti, utu na nafsi ya MTU hupoteza thamani. Tupo hapa tulipo kwa sababu ya NJAA.
Uzuri wa Bashiru ni kwamba Hana njaa na siyo mtu wa Tamaa, taaluma yake inamtosha sana kuishi maisha mazuri daima
 

Rweye

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2011
Messages
16,387
Points
2,000

Rweye

JF-Expert Member
Joined Mar 16, 2011
16,387 2,000
Organization behavior inakjhusu na CCM si UDSM. Moja ni political based na nyingine academic ...alafu ujue kuna contextual analysis
 

Forum statistics

Threads 1,392,173
Members 528,565
Posts 34,100,610
Top