Kweli " sometimes politics is unpredictable game " , January, Nape, Ridhiwani na Kigwangala hawako kwenye Baraza la Mawaziri towards 2025!!?

Fumadilu Kalimanzila

JF-Expert Member
Dec 10, 2016
1,651
5,126
January Makamba, Mwigulu Nchemba,Nape Nnauye, Ridhiwani Kikwete na Hamis Kigwangala ukitazama vizuri ni baadhi ya vijana wa CCM ambao ama walikuwa "wanaandaliwa" au "kujiandaa" kutoa uongozi mkubwa kwa Taifa letu katika siku zijazo .

Nasema hivi nikizingatia " generational succession plan" ya Nchi yetu.

Viongozi Wakuu wa Nchi yetu kuanzia 2025 - 2035 watakuwa ni watu ambao wamezaliwa kati ya mwaka 1961 hadi 1985.

Sasa nini kimetokea au wamekosea wapi hawa vijana maana sioni katika " rada" yangu "nafasi zao " katika uongozi mkuu wa Nchi yetu katika nyakati zijazo nilizozitaja.

Muda huu ndo walipaswa kuwa na majukumu makubwa ya kuwawezesha kuijua Nchi yetu vizuri, misingi ya uchumi wetu, kujua vizuri ndoto na matarajio ya watanzania, kuijua dunia vizuri na jinsi inavyo- operate !

Mwigulu Nchemba yeye naona yuko kwenye sheria na katiba sehemu ambako nadhani hajifunzi chochote kwa siku zijazo kwa manufaa ya Taifa zaidi ya kupata " ugali" wake wa kila siku tu!

Yeye ni mchumi na sidhani kama anajua hata a,b,c za sheria.Hajui hata "mens rea na actus reus" na huu kwa mtazamo wangu ni mzigo sana kwa watu kama Prof.Ibrahimu Juma (CJ), Aderladius Kilangi (AG) na Biswalo Mganga (DPP) ambao wote ni wanasheria.

Ugumu wa ufanyaji kazi wa Mwigulu Nchemba katika sheria ni sawa tu na kuendesha kesi na mtu anayejua lugha moja tu, mfano lugha ya kisukuma au kijaluo basi!

Watanzania lazima tufike mahali tukubali kuwa huu upatikanaji wa viongozi wakuu wa Taifa letu kwa "kushitukizana" una faida zake na hasara zake na unaweza kutugharimu sana kwa miaka dahari.

Athari mojawapo kubwa ya kupata viongozi wakuu wa Nchi ambao mawazo yao,ideology beliefs zao hazikujulikana mapema ni kubwa sana kwani viongozi wa namna hiyo akipata madaraka ni kama vile Nchi imepata Uhuru siku alipoingia yeye madarakani,hakuna continuity katika progress ya Nchi.

Hivyobasi mimi kama mwananchi naona tunapaswa kuyaangalia na kuyajadili haya mambo kwa Uhuru, staha na ueledi kwa mstakabali mwema wa Nchi yetu.
 
Kwahiyo unataka kusema Mzee Baba kavunja katiba ya Buza kutokuwateua kwenye kigoda?

Mbona wewe hujateuliwa na hatukusemi mkuu.

Mtu kama nape nae kweli anawaza urais?
Uongozi Mkuu sio Urais pekee nyie vijana wa shule za kata jaribuni kupanua vichwa vyenu wakati mnapobana suruali na makalio yenu!
 
Nimeyakumbuka maneno ya Mheshimiwa Palamagamba Kabudi. Yale maneno ni ya msingi sana kwa mtu yoyote anayeweka mategemeo yake kwenye vitu vilivyo nje ya uwezo na maamuzi yake.

"Prof Palamagamba Kabudi - ninaishi wosia watu wawili;
"1. Usiruhusu watu wakuandae kwa cheo chochote wala usijiandae kwa cheo chochote. Ukiwaruhusu watu wakuandae kwa cheo chochote na haswa kama hawana mamlaka ya uteuzi au hawaamui kwa kura zao, utafadhaika na kuishi maisha ya shida. Usijiandae kwa cheo chochote maana ukipata utakua na kiburi na fahari, na ukikosa utamchukia yule aliyepewa na kumfanya adui yako. Kumbe ndio kudra ya mwenyezi Mungu na ndio fungu lake - Baba mzazi rev Aidan Kabudi

"2. ..........Kwa kiongozi yoyote aliyeitwa kuwa msaidizi kama Haruni alivyoitwa kwa Musa JUA KIMO CHAKO, JUA UKOMO WAKO, HESHIMU MIPAKA YAKO".

Kiongozi mkuu hazoeleki na usimzoee, tii, mheshimu, mshauri kwa hekima na kiasi, na akiamua tofauti na ushauri wako usinune. Utekeleze kama vile hukuwahi kumshauri tofauti na alivyoamua. Na akitekeleza kama ulivyomshauri usitoke ukaringa na kutamba hata kwa mke wako au kwa mme wako maana yote ni maamuzi yake" - Cardinal Pengo "

Ukiyaelewa hayo inatosha
 
Nimeyakumbuka maneno ya Mheshimiwa Palamagamba Kabudi. Yale maneno ni ya msingi sana kwa mtu yoyote anayeweka mategemeo yake kwenye vitu vilivyo nje ya uwezo na maamuzi yake.

"Prof Palamagamba Kabudi - ninaishi wosia watu wawili;
"1. Usiruhusu watu wakuandae kwa cheo chochote wala usijiandae kwa cheo chochote. Ukiwaruhusu watu wakuandae kwa cheo chochote na haswa kama hawana mamlaka ya uteuzi au hawaamui kwa kura zao, utafadhaika na kuishi maisha ya shida. Usijiandae kwa cheo chochote maana ukipata utakua na kiburi na fahari, na ukikosa utamchukia yule aliyepewa na kumfanya adui yako. Kumbe ndio kudra ya mwenyezi Mungu na ndio fungu lake - Baba mzazi rev Aidan Kabudi

"2. ..........Kwa kiongozi yoyote aliyeitwa kuwa msaidizi kama Haruni alivyoitwa kwa Musa JUA KIMO CHAKO, JUA UKOMO WAKO, HESHIMU MIPAKA YAKO"

Budi naye ni mtu wa ku refer kauli zake kweli! Mtu aliyesema katolewa wapi vile...
 
January Makamba, Mwigulu Nchemba,Nape Nnauye, Ridhiwani Kikwete na Hamis Kigwangala ukitazama vizuri ni baadhi ya vijana wa CCM ambao ama walikuwa "wanaandaliwa" au "kujiandaa" kutoa uongozi mkubwa kwa Taifa letu katika siku zijazo .

Nasema hivi nikizingatia " generational succession plan" ya Nchi yetu.

Viongozi Wakuu wa Nchi yetu kuanzia 2025 - 2035 watakuwa ni watu ambao wamezaliwa kati ya mwaka 1961 hadi 1985.

Sasa nini kimetokea au wamekosea wapi hawa vijana maana sioni katika " rada" yangu "nafasi zao " katika uongozi mkuu wa Nchi yetu katika nyakati zijazo nilizozitaja.

Muda huu ndo walipaswa kuwa na majukumu makubwa ya kuwawezesha kuijua Nchi yetu vizuri, misingi ya uchumi wetu, kujua vizuri ndoto na matarajio ya watanzania, kuijua dunia vizuri na jinsi inavyo- operate !

Mwigulu Nchemba yeye naona yuko kwenye sheria na katiba sehemu ambako nadhani hajifunzi chochote kwa siku zijazo kwa manufaa ya Taifa zaidi ya kupata " ugali" wake wa kila siku tu!

Yeye ni mchumi na sidhani kama anajua hata a,b,c za sheria.Hajui hata "mens rea na actus reus" na huu kwa mtazamo wangu ni mzigo sana kwa watu kama Prof.Ibrahimu Juma (CJ), Aderladius Kilangi (AG) na Biswalo Mganga (DPP) ambao wote ni wanasheria.

Ugumu wa ufanyaji kazi wa Mwigulu Nchemba katika sheria ni sawa tu na kuendesha kesi na mtu anayejua lugha moja tu, mfano lugha ya kisukuma au kijaluo basi!

Watanzania lazima tufike mahali tukubali kuwa huu upatikanaji wa viongozi wakuu wa Taifa letu kwa "kushitukizana" una faida zake na hasara zake na unaweza kutugharimu sana kwa miaka dahari.

Athari mojawapo kubwa ya kupata viongozi wakuu wa Nchi ambao mawazo yao,ideology beliefs zao hazikujulikana mapema ni kubwa sana kwani viongozi wa namna hiyo akipata madaraka ni kama vile Nchi imepata Uhuru siku alipoingia yeye madarakani,hakuna continuity katika progress ya Nchi.

Hivyobasi mimi kama mwananchi naona tunapaswa kuyaangalia na kuyajadili haya mambo kwa Uhuru, staha na ueledi kwa mstakabali mwema wa Nchi yetu.
Hawafai wote kuwa huko
 
Kuna sababu nyingi, na kwa kulinda utu wake, mtu kama Kigwangala ondoa kabisa. Tulikuwa tunamshangaa Magufuli kumpa hata ile nafasi. Ana mengi ya aibu.

Mwigulu hafai na hastahili kabisa. Hata mahali alipo, hakustahili. Huyu anafaa zaidi kuwa guerrilla leader kuliko kuwa kiongozi wa Serikali.

Mtu pekee hapo ambaye unaweza kumfikiria kupewa nafasi kubwa zaidi ni January.

Ridhiwani, hapana. Ameinuliwa na baba yake kuwa Rais. Bila hiyo, huenda asingeweza kuwa hata mbunge.
 
Mwenyez Mungu humpa ufalme amtakaye wa tudhwiluu ma ntashau.na humshusha amtakae.kusema kwamba lazima waandaliwe au sijui wawekwe wap sio sawa.

Nchi ina watu milion 65 waoo weng tu wanaweza kutoa uongozi mzuri.

kudura ya mwenyezi Mungu ndio itakuwa juu yako. Akipenda unakuwa kiongozi usiutafute hautaupata.fanya kazi mahali ulipo na jamii itajua tu.sio lazima uwe laisi
 
Kwa kuangalia baraza la mawaziri ni vigumu sana kutambua nani anaandaliwa ila JPM ni very unpredictable, unaweza kuta bado wanamuangalia Makamba kama amejifunza au lah, kibaya saivi ni hakuna anayeweza tumia nguvu ya pesa kutafuta ushawishi maana ataishia kupata money laundering charge, hadi sasa ni kama nyota ya Mwinyi tu ndio inang’aa bila kuwa na mpinzani.
 
Kuwa pahala ni kusudi la uumbaji, kama hukuumbiwa kua hapo utasubiri sana kama LOWASA.
 
January Makamba, Mwigulu Nchemba,Nape Nnauye, Ridhiwani Kikwete na Hamis Kigwangala ukitazama vizuri ni baadhi ya vijana wa CCM ambao ama walikuwa "wanaandaliwa" au "kujiandaa" kutoa uongozi mkubwa kwa Taifa letu katika siku zijazo .
Magufuli ana gubu sana, yaani Mwigulu ashukuru pamoja na kwambwa kafichwa. Magufuli anajua wazi kumpa Mwigulu na hao wengine ni kuwapa nafasi ya wapate umaarufu dhidi ya mtu wake anaetaka amrithi
 
Nimeyakumbuka maneno ya Mheshimiwa Palamagamba Kabudi. Yale maneno ni ya msingi sana kwa mtu yoyote anayeweka mategemeo yake kwenye vitu vilivyo nje ya uwezo na maamuzi yake.

"Prof Palamagamba Kabudi - ninaishi wosia watu wawili;
"1. Usiruhusu watu wakuandae kwa cheo chochote wala usijiandae kwa cheo chochote. Ukiwaruhusu watu wakuandae kwa cheo chochote na haswa kama hawana mamlaka ya uteuzi au hawaamui kwa kura zao, utafadhaika na kuishi maisha ya shida. Usijiandae kwa cheo chochote maana ukipata utakua na kiburi na fahari, na ukikosa utamchukia yule aliyepewa na kumfanya adui yako. Kumbe ndio kudra ya mwenyezi Mungu na ndio fungu lake - Baba mzazi rev Aidan Kabudi

"2. ..........Kwa kiongozi yoyote aliyeitwa kuwa msaidizi kama Haruni alivyoitwa kwa Musa JUA KIMO CHAKO, JUA UKOMO WAKO, HESHIMU MIPAKA YAKO"
Kiongozi mkuu hazoeleki na usimzoee, tii, mheshimu, mshauri kwa hekima na kiasi, na akiamua tofauti na ushauri wako usinune. Utekeleze kama vile hukuwahi kumshauri tofauti na alivyoamua. Na akitekeleza kama ulivyomshauri usitoke ukaringa na kutamba hata kwa mke wako au kwa mme wako maana yote ni maamuzi yake" - Cardinal Pengo "

Ukiyaelewa hayo inatosha
Kabudi aliongea kwa busara sana hapa japo aliwachongea wenzake wakati yeye ameisha ukwaa uwaziri ha ha hah ha ha
 
Back
Top Bottom