Kweli siasa haina urafiki, licha ya kujikomba kote kule Kikwete amsambaratisha Mrema. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kweli siasa haina urafiki, licha ya kujikomba kote kule Kikwete amsambaratisha Mrema.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Deodat, Sep 16, 2010.

 1. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Kwa hisani ya Tanzania Daima:


  Kikwete amsambaratisha Mrema
  • Avunja ngome yake, azoa wanachama


  na Tamali Vullu, Moshi
  MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, amevunja ngome cha Chama cha Tanzania Labour (TLP) kwa kuvuna wanachama 750 wa chama hicho katika jimbo la Vunjo.
  Wanachama hao, walijiunga na CCM jana katika mkutano wa kampeni za mgombea huyo uliofanyika katika uwanja wa Polisi, Kata ya Himo, Wilaya ya Moshi Vijijini ambako pia aliwanadi mgombea ubunge na wagombea udiwani.

  Mbali na wanachama hao, wanachama wengine wa vyama vya upinzani walihamia CCM kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na wengine nane wa kutoka NCCR Mageuzi.

  Akizungumza baada ya kumkabidhi kadi za wanachama wa TLP, mmoja wa wanachama hao alisema wameamua kujiunga na CCM baada ya kukaa kambi ya upinzani kwa muda wa miaka 18 bila kuona mafanikio yoyote.

  “Tumeamua kurudi kwa baba na mama, kwani tumebaini kuwa huwezi kuvaa koti jeupe na suruali nyeusi na ukasema umevaa suti. Urais ameshindwa na sasa anawania ubunge... sasa anapiga watu na kutoa maneno machafu ya kila aina,” alisema mwanachama huyo bila kufafanua.

  Rasi Kikwete, akizungumza baada ya kupokea wanachama hao, aliwashukuru kwa kuchagua ukweli na kumtahadharisha mgombea ubunge wa jimbo la Vunjo kwa tiketi ya CCM, Crispin Meela, kuwa katika uwanja wa siasa kuna uongo mwingi na kusingiziwa kwingi.

  “Meele umeamua kuingia katika uwanja huu wa siasa kuna uongo mwingi na kusingiziwa sana, unaweza ukasingiziwa kuwa ukilala asubuhi kitanda huwa na maji, hilo usijali, wewe simamia kwenye ukweli na kuendelea kuomba kura kwa wananchi,” alisema.

  Awali akizungumzia ahadi kwa wananchi, mgomgea huyo wa urais kwa tiketi ya CCM, alisema serikali yake ijayo itaendelea kuboresha mambo mbalimbali mkoani Kilimanjaro kwa lengo la kuboresha sekta ya utalii na kuongeza kuwa serikali yake pia itajenga barabara kuzunguka Mlima Kilimanjaro.

  Pamoja na hayo, alisema kwa upande wa elimu serikali yake ijayo itahakikisha kila shule ya sekondari ya kata inajengewa maabara za kisasa pamoja na shule zote kupatiwa walimu wasiopungua watano kuanzia mwakani.

  Alisema atamaliza tatizo la upatikanaji maji katika Wilaya ya Moshi Vijijini ambapo kwa sasa maji yanapatikana kwa zaidi ya asilimia 70 ya lengo lililokusudiwa.

  Akiwa katika jimbo la Rombo, alisema mbali na mafanikio waliyoyapata, changamoto ambazo bado wanakabiliana nazo watazimaliza katika serikali ya CCM ya miaka mitano ijayo ambazo ni ya upungufu wa walimu, nyumba za walilmu pamoja na maabara.

  “Hizo changamoto tutaweza kuzimaliza ndani ya miaka mitano ijayo ...sisi hatutoi ahadi kwa ajili ya kuomba kura, tunatoa ahadi ambazo tutazitekeleza na tumeshafanya hivyo katika miaka mitano iliyopita,” alisema.

  Mbali ya changamoto hizo, alisema tatizo la ajira kwa Watanzania bado lipo kwani pamoja na kuahidi kutoa zaidi ya ajira milioni moja, tatizo bado ni kubwa, hivyo katika serikali ijayo wataongeza ajira mara tatu ya za awali.

  Pia alimsifia mgombea ubunge katika jimbo hilo, Basil Mramba, kuwa ni mtu makini na katika kipindi cha miaka mitano iliyopita amefanya maendeleo makubwa katika jimbo hilo.

  Naye mgombea ubunge katika jimbo hilo, Basil Mramba, aliwaomba wamchague kwa kuwa ametimiza ahadi alizotoa na kujifananisha na panga la zamani, lakini makali ni yaleyale.

  “Mimi ni panga la zamani lakini makali ni yaleyale, ahadi nilizotoa nimetimiza, sasa hatuna tatizo la umeme vijijini bali tutashughulikia tatizo la umeme katika vitongoji,” alisema Mramba.

  Kwa upande wake Mrema naye alizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana. Mrema alisema huo ni uzushi usiokuwa na mipaka kwani hakuna mwanachama yeyote aliyerudisha kadi ya TLP, zaidi ya kupigwa changa la macho.

  “Huu ni uzushi ndugu yangu, amepewa taarifa mbovu za viongozi wa mkoa, Mrema ni roho ya wana Vunjo kokote unakozunguka hapa jimboni. JK pale amedanganywa naendelea kukaza uzi kwenye kambi zangu mpaka kitaeleweka,
  …amefurahishwa na watu wake, ni mtu ambaye tunamuelewa aliyepanda pale jukwaani…. hizi ni mbimu za kisiasa tu; njia zote tumekwishazipita,” alisema Mrema.
   
 2. JOYCE PAUL

  JOYCE PAUL JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2010
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 1,007
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  mrema ANALISHWA hana shida kivileeeeeee
   
 3. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  haya ub anaweza pewa, maana hata debe la JK alikuwa kubwa kivileeeeeeeeee
   
 4. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #4
  Sep 17, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Hizi ni siasa tu! Kwani nani aliwaambia kwamba Mrema ni MWANASIASA? Ameshatamka mara kadhaa kwamba yeye ni mtu wa usalama wa taifa. Kazi yake ni moja tu! Kuhakikisha hakuna upinzani unaosimama. Ndio maana alikataliwa kurudi NCCR-Mageuzi ilipoonekana (kiasi) chama kinasimama licha ya kazi "nzuri" aliyoifanya kukisambaratisha. CHADEMA ndio wala hataingiza mguu. Mrema ni sawa na mchwa; unamkaribisha nyumbani, anaanza kutafuna viti, meza, makochi, milango hadi madirisha. Ukishashtuka, nyumba imebomoka.

  Aliyoyafanya Kikwete ni MAKUBALIANO yao. Lazima ionekane kwamba Mrema naye yuko yuko, hata kama analizwa na JK! Hili haliitaji akili nyingi kulitambua!
   
 5. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mwanahaki umenena. Kwa kazi yake hiyo ya ushushu wa kusambalatisha upinzani nchini, mrema ametaketza kazi, biashara na
  ujira wa watu wengi waliokuwa wakimuunga mkono wakizani ni mpinzani kumbe anawachoma. Mungu anamlipa kwa kadili ya
  matendo yake, dhambi ya usaliti inamwandama.
   
 6. W

  WildCard JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Pia hakuna adui wa kudumu kwenye siasa. Mramba ana kesi mbaya ya jinai ambayo ilishinikizwa vilivyo na JK lakini juzi amekwenda kumpigia kampeni! Hao ndio viongozi wetu Nchi hii. Ni UNAFIKI, FITNA, MAJUNGU kwa sana tu.
   
 7. J

  Jafar JF-Expert Member

  #7
  Sep 17, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ina maana hata hizo kadi na wanachama wa upinzani kurudi CCM inaweza pia ikawa UONGO.
   
 8. P

  Paul S.S Verified User

  #8
  Sep 17, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Huu ni moja ya unafiki mkubwa wa wapinzani hasa chadema kupenda kushabikia vyama vingine vya upinza vikienda kombo.
  ninadra sana kukuta gazeti mama la chadema linaisifu CCM, lakini kwakuwa limetokea kwa chama kingine cha upinzani basi gazeti lao limeiweka ukurasa wa mbele kabisa
   
Loading...