Kweli si kweli - Vituko vya Uchaguzi Mkuu 2005 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kweli si kweli - Vituko vya Uchaguzi Mkuu 2005

Discussion in 'Celebrities Forum' started by jmushi1, Jul 22, 2008.

 1. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,543
  Likes Received: 1,892
  Trophy Points: 280
  Hivi na huyo Gogo ni nani?
  Ni usalama wa Taifa ama mtoto wa Kigogo?

  Hayo mambo ya ajabu aliyofanyiwa mama yetu Killango kama ni kubakwa...Basi NCHI ITAMWAGA DAMU!
  KAMA MAMA KILLANGO ALIBAKWA SERIKALI IJIUZULU MARA MOJA LA SIVYO VITA NA IANZE!
  Huu NI UHUNI ULIOKUBUHU NA UMAFIOSO!
  Watanfanyiaje mama wa atu matendo maovu jamani!
  Hivi kweli Mungu yupo?
   
 2. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Mkuu kama kweli una ushahidi wa haya maneno ni-pm, otherwise wewe ni muongo na mzandiki mkubwa sana, kilichotokea hasa ni kwamba:-

  1. Majambazi waliweka misumari, gari la mama Kilango likapata flat, ndani ya gari kulikuwa na dreva wa Mzee Malecela, anayeitwa Mzee Habibu ambaye amekuwa akimuendesha Mzee for the last 30 years, pia alikuwemo mtoto wa Mama Kilango anayeitwa Edwin Nyange.

  2. Majambazi walikuwa karibu 7, ndani ya gari kulikuwa na masanduku mazito sana yenye bidhaa za biashara ya Mama Kilango, kule Dodoma majambazi wakayajaribu wakashindwa hata kuyasogeza toka ndani ya gari, wakaamua kuyaacha.

  3. Wakadai hela toka kwa Mama Kilango, akawapa pochi yake iliyokuwa na shillingi laki tatu tu, wakachukua simu yake ya mkono, na simu ya mtoto wake ya mkononi baada ya kumpiga kwanza na kumvunja mkono kwa sababu alikataa kutoa simu, pia walimpiga sana Dreva Mzee Habibu ambaye naye aligoma kuwapa simu na hela.

  4. Wakiwa wanampiga Dreva Mzee Habibu, likatokea Lori kubwa sana likiwa linakuja kwa kasi, majambazi wakakimbia porini na kujificha wakisubiri lipite, lakini Mama Kilango akapungia mikono na lile lori likasimama mbali kidogo na watu wenye silaha ktuoka kwenye lile lori wakaja pale, ndipo majambazi walipokimbia kabisaa, na ndani ya lile Lori kulikuwa na kaka wa Rostam, ambaye ni mfanya biashara maarufu wa malori makubwa ya usafirishaji, ambaye ndani ya malori yake husafiri na walinzi wenye silaha, ndio aliyemuokoa mama Kilango, sasa kama mama alibakwa kama unavyodai huyu kaka wa Rostam ndiye angekuwa wa kwanza kusema, ndiye aliyewapeleka Morogoro Mjini, na muda si mrefu askari wengi wakaja lile eneo kuwaska wale majambazi.

  5. Simu ya mtoto wa Mama Kilango, ndiyo iliyowaponza wale majambazi ikiwa ni pamoja mbwa wa polisi, ambao walikwenda mpaka kumkuta jambazi mmojawapo akiwa amelala ndani ya nyumba, wengine walikammatwa wakiwa tayari kwenye mabasi wakielekea Dar, baada ya polisi kufuatilia mawasliano ya simu za mtoto wa mama Kilango, na ile ya Dreva Mzee Habibu, walizowapora na kuanza kuzitumia, majambazi wote walirudishwa Mrogoro na kufikishwa mhakamani, ambako walijitetea wenyewe kama mawakili wao, sasa kama kungekuwa na ubakaji basi haya yangessemwa wazi hapa, kwa sababu at one point majambazi wenyewe kwa wenyewe walianza kugeukana, mbele ya sheria, haikusemwa hata mara moja!

  6. Huu ulikuwa ni wakati wa kuelekea uchaguzi wa rais, ambako kambi mbili ya Malecela na Muungwana zilikuwa zinachuana kila kona, ni wakati huu Rostam alimnunua muandishi mmoja na kumpa maneno ya kuandika against mama Kilango, alichosema ni kuwa Mama Kilango, alienda US kutengeneza sura yake kama Michael Jackson, akijitayarisha na u-first lady, sasa knowing kwamba ni kaka yake yeye Rostam ndiye aliyemuokoa Mama Kilango na majambazi, alishindwa nini kusema kuwa alibakwa pia kwenye kuvamiwa na kaka yaka ndiye aliyeona? Nani angebisha?

  Mama kilango, alichofanya ni kumfuata Rostam bungeni na kumwambia kuwa waambie waandike tena kuwa niliuytmia dola laki moja kutengenza sura maana wamekosea kuandika, na Rostam akajaribu kujitetea sana kuwa hahusiki na hiyo article.

  That is the end of the truth ya hii story, na kesho yake tena majambazi wengine hapo hapo wakamshika Makongoro Nyerere na kumpora kila kitu, sasa je yeye hawakumbaka?

  Mkuu unayeeneza hizi sumu hapa, kama una tatizo na mama kilango, basi jaribu kutafuta ukweli wa mapungufu yake uyaweke hapa, mama Kilango ni bin-adam kama sisi wengine wote ana mapungufu mengi sana kama huyajui unaweza kuuliza ukapewa, ili umchafue kuliko kujaribu kuihadaaa hii forum na maneno ya uongo, Kikwete alishidna urais kwa kuwa na hela nyingi za kampeni kuliko wagombea wote, haya mengine ya ujinga ujingani uzushi mtupu, muwe mnauliza ili msaidiwe kuelewa, maana wenye ukweli siku zote wapo hapa JF,

  Mkuu kama una ushaidi zaidi naomba uniwekee kwenye PM, halafu nikupe namba ya kaka wa Rostam aliyemuokoa mama Kilango, ili akueleze alimkuta katika hali gani, pia nitakupatia na namba za wale walinzi wake aliokuwa nao kwenye gari maana wote walihojiwa mkuu na maaandishi yapo wazi kule polisi!

  Acha uzushi huu uwanja ni mkubwa sana na mpana sana mkuu na hizi sumu zako!

  Ahsante Mkuu!
   
 3. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Huuu ni uzushi tena ujinga wa hali ya juu sana, muungwana alikuwa akiutmia pesa hakuwahi kutumia mbinu za kijinga kama hizi, majmbazi aliompora hela mama Kilango, wote wako jela na wote walikuwa wakazi wa Morogoro, kiongozi wao ambaye jina lake sio Gogo kama unavyosema, alikamatwa akiwa amelala ndani ya nyumba moja kule kijijini karibu na mahali ulpofanyikia ujambazi huo,

  Ni kweli kuna machafu mengi sana muungwana aliyafanya kwenye uchaguzi, so hata wagombea wengine pia, lakini haya ni uzushi wa kitoto tena usingeruhusiwa kuwekwa hapa JF, maana ni too low, mbinu zote za muungwana na urais tuliziweka kule BCS tena zote hata kabla hazitolewa na media yoyote ile, huu wako mkuu ni uzushi na uongo wa kitoto sana, uliza unaweza unaweza kusaidiwa ukweli!

  Ahsante Tena Mkuu!
   
 4. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,543
  Likes Received: 1,892
  Trophy Points: 280

  Kina Kikwete watatu wachuana Bagamoyo
  Ridhiwani Kikwete apitishwa

  na Albert Kawogo, Bagamoyo  RIDHIWANI Kikwete, ambaye ni mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, ni mmoja wa wanachama 322 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani, ambao wamepitishwa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika Wilaya ya Bagamoyo.
  Ridhiwani, ambaye anagombea nafasi ya uwakilishi wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM kutoka Bagamoyo, pia anapambana na baba yake mdogo, ambaye ni mdogo wa mwisho wa Rais Kikwete aitwaye Yusuf katika nafasi hiyo hiyo yenye washindani 15.
  Mbali na Ridhiwani na Yusuf kuingia kwa pamoja kwenye mpambano huo, Mohamed Kikwete, ambaye pia ni mdogo wa Rais Kikwete, naye amepitishwa kugombea nafasi ya Katibu wa Siasa na Uenezi wa Wilaya ya Bagamoyo, nafasi ambayo anaishikilia yeye mwenyewe kwa sasa. Wagombea wengine kwenye nafasi hiyo ni Amri Amri na Elizabeth Shija.
  Watu wengine waliojitosa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika Mkoa wa Pwani ni pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa tume ya rais ya kukusanya maoni ya wananchi kuhusu uundwaji wa Shirikisho la Afrika Mashariki, Profesa Samwel Wangwe, ambaye anagombea ujumbe wa Halmashauri ya CCM Wilaya ya Kibaha kupitia Jumuiya ya Wazazi.
  Wengine ni mwandishi wa habari, Selina Wilson anayegombea ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Kibaha Mjini kupitia UWT pamoja na mkuu wa zamani wa Wilaya ya Kibaha, Mtoro Katele, ambaye anagombea ujumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM kutokea Wilaya ya Kibaha Mjini.
  Joto la uchaguzi kwa nafasi ya uenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Bagamoyo limepoa baada ya jina la mwanasiasa machachari aliyerejea CCM mwaka juzi akitokea Chama cha Wananchi (CUF), ambaye pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha TLP Mkoa wa Pwani, Kassim Gogo kuenguliwa na Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa. Hata hivyo, baadhi ya watu wamedai kuwa hatua hiyo imepunguza msisimko wa uchaguzi katika nafasi hiyo. Akitangaza majina ya wanachama waliopitishwa kugombea nafasi mbalimbali, Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Pwani, Jabir Massenga, alisema jumla ya wanachama 665 wa CCM Mkoa Pwani walijitokeza kuomba nafasi za uongozi wakiwemo wanawake 147 na wanaume 498.
   
 5. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #5
  Jul 22, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,543
  Likes Received: 1,892
  Trophy Points: 280


  Kwa jinsi mwenendo wa kampeni za kina RA na JK unavyoelekea...Na kwa kuwa ukweli ni kuwa Huyu Hamis Gogo ni mshirika wake mkuu...Basi huyu Gogo ni MUJAHIDINA!
  Chuki za kidini na Kikabila dhidi ya wachagga ambao wamekuwa mwiba kwa kila aina ya mkoloni zinaelekea kuzaa matunda kwani kuna mamluki kama kina Wangwe ambao walikutana kwenye hoteli hiyo ya waarabu huko Serengeti!
  Watanzania tukatae.
   
 6. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  ,
  Kazi ipo......
  Alizitoa wapi?
   
 7. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #7
  Jul 22, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,543
  Likes Received: 1,892
  Trophy Points: 280
  Yo Yo huu ni wakati wa ku connect the dots.
  Sasa tumeshajuwa ni kwanini JK ana shida na wamarekani kwani RA ni mwarabu mbaya aliyetumwa.
  Na sasa keshaoa huko na kuuza nchi.
  Sasa kumbe hata kwenye ule uchunguzi wa Iran kununuwa uranium ya nyuklia kutoka kwa Kabila kwa kupitia RA na kwa baraka za shemeji yake aliyempa Tanzania...Na pesa hizo zinazosemekana kutoka kwa Kabila ni hizo hizo zilizotoka Iran kwani uranium ya Iran ilipitishiwa kwenye bandari yetu na biashara hiyo ilikuwa ikiendelea toka JK akiwa waziri!
  Sasa na watoto wao ndio usalama wa taifa halafu halafu kuna mtu anasema tuko HURU KWELI?
   
 8. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #8
  Jul 22, 2008
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Asante kwa ukweli, ubarikiwe
   
 9. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #9
  Jul 22, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,543
  Likes Received: 1,892
  Trophy Points: 280
  Hapo juu ni mauzo hayo ya Uranium ambayo serikali yetu ilikuwa ikiyajuwa!
  Kweli sijuwi nani alimwua Lauraa kabila...Lakini pesa zilizotoka huko Zaire ni kicbacks kutoka Irani kwa ccm kwa kukubali bandari yetu isafirishe uranium.
  JK AJIUZULU NA WATOTO WA VIGOGO WAKAE PEMBENI

   
 10. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #10
  Jul 22, 2008
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 135
  FMES hapa ndipo ulipoharibu, wewe sumu zako za ushahidi umezianika hapa jamvini na kila mtu kazisoma, kwanini basi usimpe huyu bwana nafasi ya kuanika kila kitu hapa kama ulivyofanya wewe na badala yake unataka akutumie PM?
   
 11. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #11
  Jul 22, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Kambi zote za uchaguzi wa rais uliopita kuanzia CCM mpaka upinzani zilipewa hela toka kona mbali mbali za dunia, sasa vipi ukiziongelea na zingine?

  Tanzania hatuna sheria inayokataza au inayouliza mgombea amepata wapi hela za uchaguzi, kwa sababu ingekuwepo basi wagombea wengi wasingeruhusiwa kugombea uchaguzi uliopita, kuanzia CCM mpaka Upinzani, wote walikuwa wakipewa pesa toka nje, kwenye hili mkuu huna hoja nzito kwa sababu kama una ukweli, basi ni nusu tu huyu anayekupa hizi quotes mwambie kuwa ni muongo na agenda zake mkuu ambazo hawezi kuzikamilisha au kuzipitisha kupitia hii JF, maana kuna ambao tulishiriki kwa 100%, kwenye ule uchaguzi na tunajua all the games na tulizisema kwa mara ya kwanza kule BCS, hatutakuwa na tatizo kurudia kuuweka ukweli wazi,

  Lakini kuchafua majina ya viongozi bila sababu ni kujishusha hadhi tu, na hii anti-watoto wa viongozi naona kuna mnaoona kuwa ni ushujaa sana kuipigia filimbi, lakini ukweli ni kwamba inaonyesha tu kuwa baadhi yetu hapa mliokata tamaa either na maisha au siasa za taifa letu, kwa sababu naona for the last three weeks sasa tuna ishus za watoto wa viongozi as if ni kweli wote wanaishi kifahari, mkuu nomba nikumabie ukweli ni kwamba ni watoto wa Lowassa, Idd Simba, na Karamagi ndio kidogo wanaishi maisha ambayo sio ya kwaida kwa m-Tanzania wa kawaida wengine wote huenda kuna kati yao wenye ka-nafasi ka kula milo mitatu kwa siku na labda kulala vizuri, kitu ambacho wa-Tanzania wengi sasa wanakifanya pia ingawa sio watoto wa wakubwa au vigogo,

  Otherwise, kulilia something ambacho hakipo na wala huna uhakika nacho kuhusu watoto wa viongozi ni ku-reveal inferior zetu au kushindwa maisha na kujaribu kusingizia watoto wa viongozi au vigogo, wana-JF tunapaswa kuwa na big thiniking kuliko this low minds!
   
 12. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #12
  Jul 22, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Aliyeharibu hapa ni wewe, kama una ushahidi zaidi ya nilioutoa uweke hapa au niwekee kwenye PM, kama huna basi ni bora unyamaze tu!

  Kwa sababu kama kweli una uwezo mkubwa wa kufikiri na kusoma, basi ungeelwa kuwa mimi sio niliyeanza kutoa hizi sumu, wewe ndiye uliyeanza na kusema kuwa utatoa ushidi zaidi kwenye PM,

  Sasa ninarudia tena kuwa ninakupa nafasi tena sema hapa kama una mengine zaidi ya ushahidi au utume kwenye PM kama ulivyoahidi, mkuu hapa ni suala la ukweli au uongo wa sumu zilizotemwa, sio PM wala hizo nonesense zako, kama una ukweli zaidi uweke hapa usipoteze muda wa wananchi hapa na maneno matupu, na mijadala isiyokuwa na kichwa wakati kichwa kimewekwa tayari,

  Aliyeharibu hapa ni wewe ambaye huna hoja, ila kazi kurukia tu as soon unapoona jina la Mama Kilango limetajwa, sasa weka ukweli mkuu wa hizi sumu!
   
 13. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #13
  Jul 22, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,543
  Likes Received: 1,892
  Trophy Points: 280
  Maoni yangu kwasasa at least ni kwamba kama RA asipokamatwa basi JK hawezi kuja Washington...Hilo liko wazi.
  Sasa connection ya watoto wa vigogo?
  Na Kubenea ni akaunti za kina nani alikuwa nazo?
  Haya mambo bana huwezi wadanganya wabongo tena!
  Hao wanapeta tu kwa mali za watanzania na jasho lao!
  Maisha ya Kiongozi na familia zao yatakuwaje ya kitajiri na huku wakizunguka na kusema sisi ni masikini?
  Mifano miwili tofauti kama tu ya watumishi wa Mungu mafisadi amabao wanasema fuata nachosema ila si nachofanya!
   
 14. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #14
  Jul 23, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Off-topic!
   
 15. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #15
  Jul 23, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kwenye mjadala wa "Watoto wa Vigogo/Mafisadi wakianza kutekwa" unaibua Wachaga na Wakristo na Wakoloni na Wakabila na lile na hili na lile, almuradi bora liende!

  All over the map!
   
 16. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #16
  Jul 23, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Kama una ukweli zaidi uweke mkuu, kama huna waachie wenye topic waendelee nayo! Ndiyo hasa niliyoyasema kuwa itaishia kupoteza muda wa wananchi hapa,

  Sasa wewe sio yeye, sasa umerukiaje something ambacho hukijui? Yeye amesema kuwa ana ukweli zaidi na yuko radhi kuutuma kwenye PM, mimi nimeuomba anitumie kwenye PM na akibidi auweke hapa wazi, wewe unanirukia kuwa nimeharibu kwa kusema hivyo sasa unachotaka hasa ni nini mkuu ndio maana nimekuomba kuwa kama una ukweli zaidi uweke hapa wazi au niutmie kwenye PM, au?

  Unajua huwa hatutishwi na uongo hata siku moja mkuu!
   
 17. w

  wajinga Senior Member

  #17
  Aug 26, 2008
  Joined: Jun 25, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  not yet uhuru my friend
   
Loading...