Kweli Serikali imeamua kutumia nguvu kubwa hivi kupambana na kiduku?

KAKADO

JF-Expert Member
Nov 8, 2012
230
336
Katika hali isiyo ya kawaida katika mji wa Moshi nimepata kushuhudia uzalilishaji usio wa kawaida uliofaywa na askari Polisi waliovalia kiraia, askari walimzunguka kijana aliyevalia kiutanashati kumvua kofia na kumnyoa nywele mbele ya umati kwa kisingizio kuwa ni kiduku, huu ni udhalilishaji mkubwa sitaki kuamini kilichofanyika ni sera ya kitaifa naamini ni utashi wa na ufanisi wa polisi wa Moshi pekee.

AsKari hawa wameamua kuchoma mafuta ya serikali kuzunguka kutafuta wanyoa viduku kweli??

Kwann tunatumia rasilimali pesa na rasilimali nguvu kupambana na vitu vidogo visivyo na tija kwa jamii yetu?

Kwanini watumishi wa umma hawashirikishi akili pale wanapomkoti muheshimiwa Rais? Kwanini wanatekeleza kauli ya Rais kwa mihemko??

Critically thinking
1.Nani aliwahi kusema kunyoa kipara ndio Maadili? ?
2.Nani aliwahi kusema na ku prove kuwa na nywele ndefu ni Kosa?
3.Kwanini tunahukumu watu kutokana na upeo na maono yetu?

Kupangiwa staili ya kunyoa nikuturudisha miaka ya sabini, haitofautiani na wakati ule tulivyokuwa tunapangiwa siku za kunywa chai yenye sukari wote tunakumbuka ununuzi wa sukari ulikuwa ni wa masharti ya lazima upange mstari mara mbili kwa wiki..naamini kabisa serikali kuu imeeleweka vibaya embu ijitokeze kufafanua vizuri, vijana wanadhalilishwa kwa jambo lisilo na maslahi mapana kwa Taifa letu.
 
Kiduku ni style tu unyoaji wa vijana Wala siyo uhuni, hata Babu zetu walikua wanaguga manywele mengi na kuvaa !asuluali makubwaa Kama fashen yao
 
Mbona Babu zetu na baba zetu walikua wanafuga mwele,wananyoa Afro nao pia walikua hawana maadili, na hao maaskar mbona wana nyoa style flani ivi wa ache kuonea watu mtu anahitaji uhuru binafsi
 
Back
Top Bottom