Kweli sasa nimeamini kuwa CCM ni sikio la kufa halisikii dawa.................

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,422
911,172
Ungeliwategemea CC ya CCM kuwa imejifunza kutokana kujiingiza katika kudumaza demokrasia hapa nchini pale ambapo waliwachagulia waliotoa maoni ndani ya CCM wale wagombea ambao hawauziki na kusababisha maumivu dhidi ya chama hicho na kupoteza viti vingi bungeni...............................

Lakini uteuzi wa majina matatu ya wanawake kabla ya kuwauliza wabunge wenyewe wapige kura ya maoni na kujichagulia kati ya wale walioomba ni itikadi ya mfumo wa chama kimoja cha siasa.........na tuliitarajia CC sasa ingelibadilika na kwenda na wakati lakini si hivyo hata chembe......................

Wabunge wa CCM bado wanageuzwa ni muhuri tu wa kuunga mkono matakwa ya CC ambayo wengi wake kwenye chombo hicho hata hawawezi kusimama mbele ya wapigakura kutokana na kuchokwa kuliko kithiri.......................

Kwa tabia hii ya kukataa kusoma alama za nyakati, CCM ni chama ambacho kipo ICU na ni dola tu ndiko CCM kinakopumulia vinginevyo kaburi lake CCM ni siku nyingi wapigakura walikwisha kulichimba na jeneza lake walilinua na kilichobaki ni tarehe tu ambayo dola itachoka kubeba mzigo huu wa CCM usiobebeka wa hii CCM.................na hivyo kuizika CCM rasmi....

Ama kwa hakika sikio la kufa kweli halisikii dawa..............
 
The end has come for our beloved CCM, yaani hawana akili. Mimi nilidhani kuwa wamejifunza kumbe ni mazoba wakubwa. Wamesahau kuwa hizi ni zama nyingine kabisa.

Naombeni mnijuze jamani,

Hivi Chadema nao wanaweza kusimamisha mgombea wa spika kwa mujibu wa katiba? Maana CCM hakuna spika hadi hapo tu!
 
mfa maji haishi kutapatapa, hili genge la mafisadi ndo linakaribia kuzama. buriani much hated ccm zealots. mkifa kwa kuweka kumbukumbu ntamwita mbwa wangu CCM.
 
Njia pekee ya kuendeleza mageuzi na demokrasia iliyoanzishwa ndani ya bunge na Spika Aliyemaliza muda wake ni kumchagua Mabere Nyaucho Marando hasa wabunge wa CCM ambayo watakuwa na wakati mgumu
 
Kwani kura za uchaguzi wa spika hazichakachuliwi?

Kura zaanza kuchakachuliwa pale ambapo CC inapowapandikizia wabunge wa CCM matakwa yao badala ya kuwauliza wao wangelipenda nani kati yao awe kinara wao bungeni........hii mitazamo ya mfumo mmoja wa kisiasa ndiyo inaleta shida ndani ya CCM........kuwa CC ndiyo wanajua na wengine hawajui.....................kama kweli CC wangelikuwa wanajua viongozi wazuri nchi hii isingelikuwa na lindi la umasikini wa kutupwa kama ilivyo hivi sasa........................
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom