Penye nia pana njia: Ni wiki ya 5 sasa sijatia soda mdomoni, kumbe inawezakana kabisa

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
35,845
40,433
Mara ya kwanza nilipojaribu nile chakula bila kunywa soda niliona maisha magumu sana, chakula hakishuki, sina hamu ya maji wala juisi ya matumda wala chochote kile, yaani natamani soda tu, hapa ndipo nilipogundua kumbe hii ni shida, ni kama madawa ya kulevya, nina mashaka kuna kitu wanaweka mule, hii si kawaida.

Mwezi uliopita nikasema hata ikibidi nife kwa kukosa soda, so be it, ila sinywi hata iweje, ni wiki ya 5 leo sijanywa soda, napitia wakati mgumu sana, ila namshukuru Mungu, naendelea vizuri.

============================

============================
Update: 09/11/2021

==========================
Update: 05/02/2023

___________________________

🤣 ila watu tunatofautiana aisee yani soda nayo mpk uparangane..! Mi sijui namiezi mingapi tu! Wengine tusipokunywa hayo maji hapakaliki Yani kila siku walau ninywe lita kadhaa alasivyo koo huwa linakorofisha hatari!! Ukimaliza hilo uache na sukari ujizoeshe.
 
Ukiona mtu anang'ang'ana kuacha kitu fulani basi ujue limemkuta jambo. Vivyo hivyo kwa walevi ukiona anatafuta msaada wa kuacha pombe ni ama imwmfilisi au alijikojolea kitandani au kufanya kitu cha aibu kilichomshuhia heshima au kumfanya aishi kwa hatia moyoni
 
Mara ya kwanza nilipojaribu nile chakula bila kunywa soda niliona maisha magumu sana, chakula hakishuki, sina hamu ya maji wala juisi ya matumda wala chochote kile, yaani natamani soda tu, hapa ndipo nilipogundua kumbe hii ni shida, ni kama madawa ya kulevya, nina mashaka kuna kitu wanaweka mule, hii si kawaida.

Mwezi uliopita nikasema hata ikibidi nife kwa kukosa soda, so be it, ila sinywi hata iweje, ni wiki ya 5 leo sijanywa soda, napitia wakati mgumu sana, ila namshukuru Mungu, naendelea vizuri.
Mkuu we acha tu hiyo misoda ila usijekutushawishi tuache minduki...
 
Mimi muhanga wa energy's drink, nilitia nia 2019, sasa iv nina miaka miwili sijatumia. Kwaio kwa maana rahisi nimeweza kuacha.Kuhusu soda week zilizopita nlikua n maombi ya kufunga 21days,

Lkn nilipokua jion nafungulia baada ya kula nikinywa soda nilikuw nashindwa kumaliza ht nusu wkt sio kawaida,nikawa na agiza juice ya miwa tu na izi za viwandani atheist nilikua namaliza

Nakusudia pia kuacha soda,hata hivyo mi sio mpenzi sana lkn soda 2 au 3 kwa mwez nilikua na tumia.
 
Addiction ni kila mahali, mm siwezi kulala bila kuona hata nembo ya CCM, yaani CCM imejaa rohoni na moyoni, nikisikia mtu anaisema vibaya CCM moyo unaniuma sana, sbb nimezaliwa nayo na nimekulia nayo. Ndio maisha yangu, bila CCM Imara nchi yetu ingeyumba sanaa huenda leo tungekuwa kama nchi za waafrika wenzetu, vita kila kona, CCM daima na milele, Mungu nisaidie, Amen.
 
34 Reactions
Reply
Back
Top Bottom