Kweli nimeamini CHADEMA ni noma!

Mimi leo nimeamini CDM ni noma. Ni chama cha kwanza cha upinzani kusambaratisha CCM hadi kuvua watu uongozi,ni chama cha kwanza upinzani kufuta ajira za watu ccm,ni chama cha kwanza kukikosesha chama cha ccm na ni chama ambacho Makamba na Chiligati hawatakisahau.

Aminia chalii,
CDM ndio dira ya taifa.....CCM itake isitake!
Usisahau hata JK alinusurika pa uzi wa sindano na hatasahau kamwe alivyotumia nguvu ya dola kukwiba nguvu na ushindi wa umma ambao ndio uliotoa picha halisi ya jinsi CCM inavyokufa, na kuamua kujitangazia kuivua gamba! Lakini mtoto wa joka la kibisa ni joka tu...hivyo CCM mpya haina upya ila ni kupaka rangi chungu cha zamani wakati kwa ndani ni uzee uleule...CCM ni ufisadi kwa sana! Hawaponi ng'o! labda woooote wakapate 'kikombe cha babu' na kuikana ile dhambi ya ibilisi...yaani wizi na ufisadi wa mali za raia maskini wa taifa hili. La sivyo...CCM ni itakuwa mfu tu! Mukama kakabidhiwa mahututi!
 
CHADEMA whaaaaaaaaaaaat? kwa ninavyokua mimi CHADEMA ni chama kinachosapotiwa na makada waaasi wa CCM,CHENYEWE KAMA CHENYEWE HAKIWEZI KUSIMAMA.sasa CCM INAANZA KUJIPANGA maana yake kifo cha chadema chaja
 
CCM ipo imara kama chuma cha pua, si rahisi kukisambaratisha

Nani kasema? Siku zao zina hesabika upako wa uongozi hawana tena, kila mahali shati ya kijani, kofia ya njano ikisimama inaonekana kama mavi. Ndio maana hakuna hata kiongozi mwenye ujasiri wa chama cha Chukua Chako Mapema wa kusimama mbele ya wachambua hoja na kuzungumza cha maana. I real wish if i could help them in this difficult time, i real pity them 'CCM'.
 
Mzee Makamba siku moja alinipa hadithi ya Tumbili na Komba, eti tumbili alikutana na komba akamuuliza vipi bana mbona macho mekundu, komba akamuambia eti sababu ya vilio, amepata misiba mingi sana, wakati wanaagana Komba akaona makalio ya tumbili naye akamuuliza vipi bwana mbona hapo kwenye makalio hakuna manyoya, tumbili akamjibu ni vikao bana eti siku hizi amekuwa ni mbunge wa viti maalum wa CDM, kila kukicha, vikao, maandamano, makongamano na semina. Mwisho mzee Makamba akasema wote tumbili na komba ni waongo wakubwa.

Kwa hiyo makamba pia alikuwa charecter kwenye hiyo hadithi ya Tumbili na Komba? halafu Komba gani unayemsema wewe, huyu wa TOT Plus
 
Back
Top Bottom