Kweli ndio tumefikia huku?

Kipenseli

JF-Expert Member
Feb 9, 2020
800
1,050
Mwanamume aitwae Muhammad Malik (29) wa London Uingereza ameweka mabango kwenye miji ya Birmingham na London Uingereza akitangaza kutafuta Mke, bango likisomeka "niokoe kutoka kwenye ndoa iliyopangwa" akimaanisha hayupo tayari kuchaguliwa Mke kama ilivyozoeleka kwenye Jamii yake bali anataka kupata chaguo lake yeye.

Katika kuonesha kwamba Malik yuko serious na utafutaji huo, amefungua website ya findMALIKawife.com ambayo anaamini itasaidia Watu kumrahisishia kumpata huyo Mke anaemtaka.

"Mpenzi wangu mzuri nataka awe Muislamu na awe kwenye miaka yake ya 20 na ambaye anajitahidi kuboresha dini yake, niko tayari kupokea Mwanamke wa kabila lolote lakini nina familia yenye kelele ya Kipunjabi, sitanii, natafuta Mke kweli, siko kinyume na dhana ya Mke wa kuchaguliwa na familia lakini ningependa kutafuta wa peke yangu"
FB_IMG_1641746458364_1.jpg
 
Mwanamume aitwae Muhammad Malik (29) wa London Uingereza ameweka mabango kwenye miji ya Birmingham na London Uingereza akitangaza kutafuta Mke, bango likisomeka "niokoe kutoka kwenye ndoa iliyopangwa" akimaanisha hayupo tayari kuchaguliwa Mke kama ilivyozoeleka kwenye Jamii yake bali anataka kupata chaguo lake yeye.

Katika kuonesha kwamba Malik yuko serious na utafutaji huo, amefungua website ya findMALIKawife.com ambayo anaamini itasaidia Watu kumrahisishia kumpata huyo Mke anaemtaka.

"Mpenzi wangu mzuri nataka awe Muislamu na awe kwenye miaka yake ya 20 na ambaye anajitahidi kuboresha dini yake, niko tayari kupokea Mwanamke wa kabila lolote lakini nina familia yenye kelele ya Kipunjabi, sitanii, natafuta Mke kweli, siko kinyume na dhana ya Mke wa kuchaguliwa na familia lakini ningependa kutafuta wa peke yangu"View attachment 2074995
Mbona hata Dar ilitokea kwa mzee mmi. Kuweka tangazo na akapata mke,

kipi Cha ajabu?
 
Ngojw uone, Watakuja kuulizia
"Kwani nauli ya uingereza Bei gan?"
 
Akitoka nje ya formula atakufa masikini,, akubali tu kumuoa aliyechaguliwa na wazazi,, kama ni kumpenda atampendea mbele ya safari,, tamaduni za kihindi na kiarabu ni za ajabu sana,,
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom