Kweli Muda wa mabadiriko umefika! Hata Maggid Mjengwa Kabadirika! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kweli Muda wa mabadiriko umefika! Hata Maggid Mjengwa Kabadirika!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jibaba Bonge, Mar 4, 2011.

 1. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2011
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Maggid Mjengwa na Neno La Leo: Afrika Kuku Hachimbiwi Kaburi!

  [​IMG]
  Ndugu Zangu, AFRIKA viongozi ni wengi wanaopatwa na vigugumizi wanapoombwa watoe maoni yao kwa kile anachofanya mwenzao Ghadaffi kwa watu wake.

  Vigugumizi hivyo vina tafsiri nyingi; moja kuu ni ukweli, kuwa kuna viongozi Afrika wanaofanana fanana naye. Kwamba nao wasingesita kufanya kama alivyofanya Ghadaffi pale inapotokea watu wao wanapoamua kuingia mitaani kuonyesha hisia zao kwa amani kabisa.

  Watatafuta visingizio vya kuwatwanga risasi watu wao ili kuwatishia wengine. Ndio, kinachotokea Afrika ni hiki; kwanza, mtawala atawaita waandamanaji ‘kuku’ na majina mengineyo. Kisha ataamrisha vikosi vyake vitumie risasi za moto kuwadhibiti ‘kuku’ waandamanaji.

  Si tunajua, kuwa Afrika kuku hachimbiwi kaburi? Viongozi Afrika watambue sasa, kuwa Afrika kuna kimbunga kimelipuka. Ni kimbunga kinachosambaa. Kimeanzia Tunisia, kikaenda Misri na kimetua Libya.

  Kinasambaa. Ni kimbunga cha mabadiliko. Waafrika wengi wanaokandamizwa na watawala au vyama tawala katika nchi zao, leo wana kiu kubwa ya kuwa na ‘ Tahrir’ zao ili nao wajikomboe.

  Kiongozi makini, mwenye busara na mapenzi ya dhati kwa nchi yake, hatosubiri watu wake wafikie ukomo wa uvumilivu ili afanye mabadiliko hitajika na yenye kukidhi matakwa ya wakati husika.

  Nimepata kuandika kuwa katika nchi, mabadiliko ya amani yanawezekana; lakini kwa anayejaribu kuyazuia atambue kuwa mabadiliko yenye vurugu hayaepukiki.

  Maana tumeona Wamisri na Walibya wamefikia ukomo wa uvumilivu wa kukandamizwa. Na watu wa Afrika wameshaibaini siri ya kuwatoa madarakani wakandamizaji wao; ni kutoka mitaani kwa wingi na kuandamana kudai haki zao. Ndio, Waafrika wameamka usingizini.

  Wameshatambua kuwa hakuna risasi au kombora la mtawala litakaloweza kushinda nguvu ya umma uliodhamiria kutaka mabadiliko.

  Yametokea Tunisia, Misri, Libya. Yanaweza kutokea popote pale Afrika. Busara ni kuenenda na wakati uliobadilika.
   
 2. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #2
  Mar 4, 2011
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Sio kabadilika! Maoni yake siku zote yako pande mbili, kusifu panapostahili na kukosoa panapostahili pia!
   
 3. M

  Mzee wa Usafi JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2011
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 634
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Tatizo lake ni uccm umemzidi badala ya Utanzania...CCM haiko kwa ajili ya maslahi ya watanzania bali kwa wateule wachache kama yeye....kwani kuanzia kwa yule ndugu yake dc, mujeshi....na bwana kilimo kule Ikandana.....zidumu fikra za mwenyekiti
   
Loading...