Kweli mnawalipa hivi watawala wenu? Kwa wanaojua hesabu

Sasa hii ndiyo changamoto na kazi ya wale wanaodhani wao ni wazalendo na wanaoliweka Taifa mbele zaidi ya kitu kingine chochote. Nimesikia Muungwana kaagiza watu wafuatwe nyumba hadi nyumba sijui ni kwa ajili gani sikuwa na interest ya kusoma. Kwa mfano huo huo wanaolitakia mema Taifa hili inabidi wajipange kwenda nyumba hadi nyumba kuelezea kwa wananchi juu ya madhambi haya ya Serikali ya CCM. Wananchi walipe kodi viongozi wajinufaishe kwa mishahara minono na marupurupu juu!!

Naamini CCJ ni Chama kilichoamua kuweka Taifa mbele kuliko kitu kingine chochote. Wote wenye nia njema na wanaoamini kwamba kwao wao maslahi ya Taifa na wananchi kwa ujumla ndio kipaumbele kwao basi wajiunge na CCJ tulikomboe taifa!
 
Mie nafikiri, mnachonga tu lakini mkipewa nafasi hizo nanyi mtapukuchua na kupekenya kwa staili hiyohiyo na miondoko ileile kwa malingo yaleyale.

Binafsi, sioni kama tatizo ni la viongozi ama chama, tatizo letu ni sisi wote ndo tulivyo, oops yeah! wapo wachache wasivyo kuwa hivyo. Hapa cha mhimu ni kupigania mfumo ambao ni wa kuwajibishana hizo za mishahara zitakuja balance zenyewe tu kukiwa na mfumo sahihi wa kutawalana.

Binafsi mimi nafikiri wafanyakazi wanakila sababu na kila uwezo wa kufanya hilo kuwezekana badala ya kupigania masilahi yao binafsi tena yenye mionjo ya mda mfupi.
Na bado naamini, sisi waafrika hasa watanzania cha kuanza nacho ni kupokonya wabunge kuwa mawaziri na kuwapokonya wao wabunge kupanga mishahara yao na ya wengine. Na badala yake nafikiri wabunge ndo wawe wanateua mawaziri kulingana na qualification na hao mawaziri wasiwe wabunge.
 
Baada ya kuishabikia CCJ nimeenda kufanya hesabu za Mzee Mwanakijiji, kama nimekosea mtanisahihisha. Nimepata hivi:

Kwa hesabu hizo, tunao jumla ya viongozi 524 wa ngazi za juu za kisiasa (Rais, Makamu, Mawaziri, Manaibu Waziri, Wabunge. Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya n.k.) Bila shaka MMKJJ ametubandikia mishahara ya kila mmoja wao kwa mwezi. Ukizidisha hiyo mishahara yao kwa mwezi na kuijumilisha utapata hesabu ya Shs. 10,321,404,000 kwa mwezi. Jumla hiyo ya mishahara ya viongozi wetu kwa mwezi ukizidisha kwa miezi 12 kupata wanacholipwa kwa mwaka utapata jumla ya Shs. 123,856,848,000 kwa mwaka.

Tukichukua idadi hiyohiyo ya 524 na ku-assume kwamba ndio wafanyakazi wa kima cha chini wanaostahili Sh. 315,000 inayodaiwa na TUCTA utapata jumla ya Sh. 165,060,000 kwa mwezi na kwa mwaka ni Sh. 1,980,720,000.

Kwa hesabu hizo basi jumla ya mishahara wanayopata viongozi wetu kwa mwaka ni approximately mara 62.5 ya jumla ya mishahara watakayopata idadi hiyohiyo ya wafanyakazi wa kima cha chini wakilipwa mshahara wa 315,000/= kwa mwezi ama jumla ya Sh. 1,980,720,000 kwa mwaka!

Pia endapo wafanyakazi wa kima cha chini watalipwa Shs. 135,000 inayodaiwa kwamba ndicho kiwango Serikali inapendekeza walipwe jumla ya malipo ya wafanyakazi 524 itakuwa ni Sh. 70,740,000 kwa mwezi na Sh. 848,880,000 kwa mwaka. Ukilinganisha na jumla ya mishahara ya viongozi wetu kwa mwaka na ile wanayopata wa kima cha chini mishahara ya viongozi itakuwa approximately ni mara 145.9....

Hesabu zilizotolewa ni mishahara tu ya viongozi wetu hawa. Bado marupurupu mengine ya posho, mafuta, simu, entertainment allowances, n.k. Halafu wakubwa hawa wanatuambia kwamba watumishi wa kima cha chini wakilipwa kiwango wanachodai watakuwa wametumia mapato yote ya nchi!

Kujilipa mishahara mikubwa kiasi hicho ni unyonyaji mkubwa kwa upande wa Serikali dhidi ya wananchi ambao hata hawapati hizo huduma za jamii zinazodaiwa kulipiwa kutoka kwenye pato la Serikali.

Kwa wale waliozaliwa juzi: Wakati nchi inapata Uhuru mishahara ya juu kabisa nchini (mishahara iliyowekwa na wakoloni) ilikuwa inazidi ile ya kima cha chini kwa mara 50. Mwaka 1967 wakati Azimio la Arusha linatangazwa, mishahara ya juu ilikuwa imeshashushwa hadi kuwa mara 29 ya mshahara wa kima cha chini. Kwa viongozi wa wakati huo mishahara hiyo ilikuwa bado ni mikubwa. Miaka 10 baada ya Azimio la Arusha i.e. 1976 (kutokana na siasa za Ujamaa na Kujitegemea) aliyekuwa akipata mshahara wa juu nchini alikuwa anamzidi mtu wa kima cha chini mara tisa tu. Na hesabu hiyo ilionekana bado ni kubwa. Wananchi waliishi kwa amani na utulivu mkubwa wakijua kwamba keki ya Taifa hata kama ni ndogo kiasi gani inagawanywa kwa uwiano unaostahili. Watoto wa mkulima na mfanyakazi waliweza kusoma bila adha ya kulipa karo, matibabu yalikuwa bure na yalipatikana bila adha pia. pembejeo za kilimo ziligawiwa bure n.k. n.k.

Sasa hawa viongozi wetu watuambie wao wana haki gani ya kupata mishahara ambayo ni mara 100 na zaidi ya ile ya kima cha chini? Hivi kweli ni haki kwa viongozi kujimegea pande kubwa namna hiyo la keki ya Taifa ambayo inatokana na kodi wanazotowa wananchi wote hata yule wa kima cha chini?

Sera za kibepari ndivyo zilivyo – mimi kwanza wengine shauri yao! Ujamaa ni utu kwanza mengine baadaye!
 
Zote hizi ni kwa mwezi: [24 x 2,422,000 = 21 x 2,046,000 = 27 x 2,080,000 = 1 x 4,850,000 = 1 x 4,850,000 = 323 x 1,921,000 = 127 x 1,921,000 =] [12] The process is also known as "the order of operation"... Ukipata jibu.. utakuwa na weekend mbaya kweli!

24 x 2,422,000 = 58,128,000 (Mawaziri)
21 x 2,046,000 = 42,966,000 (Manaibu Waziri)
27 x 2,080,000 = 56,160,000 (Wakuu wa Mikoa)
1 x 4,850,000 = 4,850,000 (Waziri Mkuu)
1x 4,850,0000 = 4,850,000 (Makamu wa Rais)
323 x 1,921,000 = 620,483,000 (Wabunge)
127 x 1921,000 = 243,967,000 (Wakuu wa Wilaya)
JUMLA 1,031,404,000 X 12 = 12,376,848,000

Sijui nimepata? Lakini bora nikose weekend yangu isije kuwa mbaya alivyosema mwanakijiji
 
Mshahara wa Rais ni kiasi gani?
 
viongozi wa tanzania wana raha kwani wametupata raia baridi sana,
tunavumilia kila lijalo, wepesi wa kustuka na rahisi wa kusahau,
Cha ajabu kwa upumbavu wetu tunafikiri kuwa kwa kuwa raia baridi ndo tunawawekea mazingira mazuri viongozi wetu ili watufanyie yale tunayohitaji. kumbe wanafanya kinyume chake. Sasa busara ni kuwa raia moto.
Sasa hivi kuna mbinu mpya ya kula. Watu wa hazina wakishirikiana na wizara mbalimbali wanavitumia vyuo vya serikali kama mifereji ya kupitishia pesa. Mafungu kati 50,000,000 na 200,000,000 yanapitia katika vyuo mara moja au mbili kila mwezi na kisha kuhamishiwa kwenye a/c na wakulu hao. Bila kufanya hivyo chuo chako hakitapewa fungu lake.Habari ndo hiyo. Mwenye source afuatilie UD, IMF, DMI na vingine lukuki
 
akini jamani si tunawachagua wenyewe??............. nawkwambieni uchaguzi bila eimu ya uraia ni "UCHAFUZI"............ kinachotoa mchozi kabisa ni kuwa hao waheshimiwa tayari wana uhakika wa kushinda tena uchaguzi wa mwaka huu.......... tena kwa kishindo!!!!!!!!
 
Samahani sikuweka mshahara wa Rais, Waziri Mkuu au Makamu wa Rais, sikuweka mshahara wa Majaji wote, sikuweka mshahara wa Wakuu wa majeshi hadi ngazi ya Luteni Genererali, au Polisi na Magereza hadi ngazi ya ACP, sikuweka mishahara ya wakuu wa Mashirika au taasisi za umma, wakuu wabodi mbalimbali n.k Na vile vile hatujaweka mishahara ya Makatibu Wakuu, hatujaweka mishahara ya Mabalozi, mishahara ya Wasaidizi wa ngazi za juu katika wizara na idara mbalimbali Na kama walivyosema wengine sikuingiza kabisa marupurupu na posho yoyote ile.
 
Baada ya kuishabikia CCJ nimeenda kufanya hesabu za Mzee Mwanakijiji, kama nimekosea mtanisahihisha. Nimepata hivi:

Kwa hesabu hizo, tunao jumla ya viongozi 524 wa ngazi za juu za kisiasa (Rais, Makamu, Mawaziri, Manaibu Waziri, Wabunge. Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya n.k.) Bila shaka MMKJJ ametubandikia mishahara ya kila mmoja wao kwa mwezi. Ukizidisha hiyo mishahara yao kwa mwezi na kuijumilisha utapata hesabu ya Shs. 10,321,404,000 kwa mwezi. Jumla hiyo ya mishahara ya viongozi wetu kwa mwezi ukizidisha kwa miezi 12 kupata wanacholipwa kwa mwaka utapata jumla ya Shs. 123,856,848,000 kwa mwaka.

Tukichukua idadi hiyohiyo ya 524 na ku-assume kwamba ndio wafanyakazi wa kima cha chini wanaostahili Sh. 315,000 inayodaiwa na TUCTA utapata jumla ya Sh. 165,060,000 kwa mwezi na kwa mwaka ni Sh. 1,980,720,000.

Kwa hesabu hizo basi jumla ya mishahara wanayopata viongozi wetu kwa mwaka ni approximately mara 62.5 ya jumla ya mishahara watakayopata idadi hiyohiyo ya wafanyakazi wa kima cha chini wakilipwa mshahara wa 315,000/= kwa mwezi ama jumla ya Sh. 1,980,720,000 kwa mwaka!

Pia endapo wafanyakazi wa kima cha chini watalipwa Shs. 135,000 inayodaiwa kwamba ndicho kiwango Serikali inapendekeza walipwe jumla ya malipo ya wafanyakazi 524 itakuwa ni Sh. 70,740,000 kwa mwezi na Sh. 848,880,000 kwa mwaka. Ukilinganisha na jumla ya mishahara ya viongozi wetu kwa mwaka na ile wanayopata wa kima cha chini mishahara ya viongozi itakuwa approximately ni mara 145.9....

Hesabu zilizotolewa ni mishahara tu ya viongozi wetu hawa. Bado marupurupu mengine ya posho, mafuta, simu, entertainment allowances, n.k. Halafu wakubwa hawa wanatuambia kwamba watumishi wa kima cha chini wakilipwa kiwango wanachodai watakuwa wametumia mapato yote ya nchi!

Kujilipa mishahara mikubwa kiasi hicho ni unyonyaji mkubwa kwa upande wa Serikali dhidi ya wananchi ambao hata hawapati hizo huduma za jamii zinazodaiwa kulipiwa kutoka kwenye pato la Serikali.

Kwa wale waliozaliwa juzi: Wakati nchi inapata Uhuru mishahara ya juu kabisa nchini (mishahara iliyowekwa na wakoloni) ilikuwa inazidi ile ya kima cha chini kwa mara 50. Mwaka 1967 wakati Azimio la Arusha linatangazwa, mishahara ya juu ilikuwa imeshashushwa hadi kuwa mara 29 ya mshahara wa kima cha chini. Kwa viongozi wa wakati huo mishahara hiyo ilikuwa bado ni mikubwa. Miaka 10 baada ya Azimio la Arusha i.e. 1976 (kutokana na siasa za Ujamaa na Kujitegemea) aliyekuwa akipata mshahara wa juu nchini alikuwa anamzidi mtu wa kima cha chini mara tisa tu. Na hesabu hiyo ilionekana bado ni kubwa. Wananchi waliishi kwa amani na utulivu mkubwa wakijua kwamba keki ya Taifa hata kama ni ndogo kiasi gani inagawanywa kwa uwiano unaostahili. Watoto wa mkulima na mfanyakazi waliweza kusoma bila adha ya kulipa karo, matibabu yalikuwa bure na yalipatikana bila adha pia. pembejeo za kilimo ziligawiwa bure n.k. n.k.

Sasa hawa viongozi wetu watuambie wao wana haki gani ya kupata mishahara ambayo ni mara 100 na zaidi ya ile ya kima cha chini? Hivi kweli ni haki kwa viongozi kujimegea pande kubwa namna hiyo la keki ya Taifa ambayo inatokana na kodi wanazotowa wananchi wote hata yule wa kima cha chini?

Sera za kibepari ndivyo zilivyo – mimi kwanza wengine shauri yao! Ujamaa ni utu kwanza mengine baadaye!

Safi kabisa bora maisha.. wewe MAGAZIJUTO unaziweza...
 
Nadhani inabidi wambiwe nawakumbushwe wasilinganishe mishahara yao na ya nchi nyingine. walanganishe mishahara yao na KCC( INazidi mara ngapi Kima cha chini),walinganishe mishahara yao na GDP halisi ya taifa . watafute ratio wapige hesabu

Kama kuna umuhimu wa kulinganisha mishahara yetu na wakenya au waganda basi twende mbali tujiulize je Pato halisi la taifa na wale tunajilinganisha nao linafanana.

Hatuwezi kuwa na maendeleo katika taifa amabalo Most top paying jobs ni za kisiasa au za watu walichaguliwa kisiasa badala ya usahili. Sidahni kama David Cameroon au Barrack Obama wamo hata kwenye top 50list ya watu wanaopokea mshahara mkubwa nchini mwao. Why ????

Sidhani kama Mbunge wa UK an USA ndio mtu anayepokea mshaahara mkubwa jimboni kwake . Whyy???? Huu ndio upande mwingine wa shilingi wabunge mawaziri , utumishi inabidi waangalie.

Matokeo yakeTunaona walimu, madaktari wahandisi tunachukia career zetu na kuwa na ndoto ya kuhamia kwenye siasa..
 
Samahani sikuweka mshahara wa Rais, Waziri Mkuu au Makamu wa Rais, sikuweka mshahara wa Majaji wote, sikuweka mshahara wa Wakuu wa majeshi hadi ngazi ya Luteni Genererali, au Polisi na Magereza hadi ngazi ya ACP, sikuweka mishahara ya wakuu wa Mashirika au taasisi za umma, wakuu wabodi mbalimbali n.k Na vile vile hatujaweka mishahara ya Makatibu Wakuu, hatujaweka mishahara ya Mabalozi, mishahara ya Wasaidizi wa ngazi za juu katika wizara na idara mbalimbali Na kama walivyosema wengine sikuingiza kabisa marupurupu na posho yoyote ile.
Kazi nzuri MM. Hii inaitwa habari ya awali, malizia. Kazi hii uliyoanza ni muhimu sana katika kuimarisha uwajibikaji wa hawa wanasiasa kwa wananchi. Tafadhali kusanya taarifa kulingana na muda wako, jumlisha wakuu wote. Ukimaliza rusha kwenye magazeti yetu ukieleza sehemu ya bajeti ambayo hawa wanasiasa wanachukua. Ukishirikiana na wachumi wengine jumulisha pia na posho zao zinazofahamika. Habari hii inatoa kitabu Mwanakijiji kitakachokuwa rejea ya namna uchumi unavyoweza kuhudumia wanasiasa badala ya wananchi.
 
Kuna mwenye

diclofenac jamani anisaidie

Ha ha ha!! Hii statement yako tu imeniondolea maumivu. Na WKD vodka with coke nilikuwa nimekaanza naona kameisha nguvu kabisa. Na hapo huo mshahara hauguswi; utaguswa na nani wakati mahitaji ya nyumbani, wafanyakazi, karo za shule, mafuta ya gari nk vinalipiwa na mlipa kodi?

Hawa watu tuwapotezee tu, iko siku.

Tanzania tunachohitaji sasa si vyama vipya vya upinzani tena, tunahitaji (civilian) pressure groups - sijui zinaitwaje kwa Kiswahili safi.

Laleni salama jamani
 
Nani wa kumjibu MkamaP naona wote mmekaa kimya kweli mmepata maumivu poleni sana. Mi ninazo asprin kwa anayetaka kutuliza maumivu.
 
Boramaisha kwa hesabu hizi je viongozi wa dini wasiiseme serikali kwa sababu amani itaondoka?
Je wanyamaze na kufyata mkia maana uchaguzi uko karibu? Lakini wanaoumia ni waumini wao. ahahahahahahahaha!!!!!!!!! Nasikia maumivu, ngoja nisogeze asprini karibu na mdomo.
aghhhhhhhhhhhhhhhhrrrrrrrrrrrrrr
 
24 x 2,422,000 = 58,128,000 (Mawaziri)
21 x 2,046,000 = 42,966,000 (Manaibu Waziri)
27 x 2,080,000 = 56,160,000 (Wakuu wa Mikoa)
1 x 4,850,000 = 4,850,000 (Waziri Mkuu)
1x 4,850,0000 = 4,850,000 (Makamu wa Rais)
323 x 1,921,000 = 620,483,000 (Wabunge)
127 x 1921,000 = 243,967,000 (Wakuu wa Wilaya)
JUMLA 1,031,404,000 X 12 = 12,376,848,000

Sijui nimepata? Lakini bora nikose weekend yangu isije kuwa mbaya alivyosema mwanakijiji

Hao wawili ni Spika na Jaji Mkuu!

source hii hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...abunge-mawaziri-na-majaji-juu.html#post562847
au tafuta Mwananchi la tarehe 25/8/2009!

Wikiendi njema na mbarikiwe!
 
Back
Top Bottom