Kweli mke wa mtu sumu, nikikumbuka siku nilivyofumaniwa nilikuwa kama pilitoni

Siasa Basi

JF-Expert Member
Jul 10, 2016
1,493
4,278
Habari wakuu. Twende kwenye mada

Hiki ni kisa cha muda kidogo, wakati huo nikiwa bado naishi kwa wazazi. Nakumbuka nikiwa nimeisha maliza chuo nimekaa tu nyumbani sina ramani yeyote. Jirani yetu kulikuwa na binti ambaye alikuwa ni mke wa mtu, yule mwanamke alikuwa kicheche sana. Na mume wake alikuwa ni dereva wa gari, hivyo muda wake akitoka saa 11 asubuh kurudi saa 6 usiku. Alikuwa na mazoea sana yakuja hapo nyumbani kupiga stori na Mama na wadogo zangu wa kike.

Siku moja nimekaa ilikuwa Jumapili wengine wameenda kanisani, akajipitisha nikamuita nikarusha mistari, akasema ngoja kama nusu saa hivi nitakujibu. Mwanaume nikatulia aijapita dk kumi huyo, akasema nimekubari lkn uwe mwangalifu siunajua mi mke Mtu? Nikamwambia usijali nitakuwa mwangalifu. Wakati huo sikuwa hata na kitu. Pesa nilikuwa napata baada ya kutumwa bonga sokoni na nyanya ile chechi inayobaki natia mfukoni kama ya vocha. Mliomaliza vyuo mlioko nyumbani kama hamjishugulishi mnalijua hilo.

Siku hiyo hiyo majira saa 12 jioni nikamshitua binti akasema tukafanyie wapi, nikamjaribu kwako hapo si pako poa, akasema ni wewe tu. Maana alikuwa anakaa peke yake na mtoto wake mmoja mwenye umri wa miaka 2. Basi mi mtu mzima nikajitupa kwenye mjengo, nikampa mtoto 200 ya pipi akasepa kwenda kucheza na wenzake, nikabaki na mama yake ndani. Akanivutia fasta chumbani kwake tukaanza kusuguana ngozi, dah! Gemu lilikuwa hatari nilipiga viwili lkn vya hatari. Binti alisifia akasema mume wake toka amekuwa nae hajawahi kumkuna kiasi hicho, amekuwa hakimpa kimoja tu tena cha dk 5 kachoka na harudii tena mpaka baada wiki. Mi nikajiona kidume cha mbegu.

Binti akanikabidhi moyo wake ikawa kama mazoe, binti akanipenda sana kila muda anataka akunwe. Kama mwezi ulipita tunakunjana tu, mpaka mama alishitukia hilo dili lkn alikuwa ameishachelewa mapenzi yameishanoga kwa mke wa mtu. Akienda Kariakoo ananinulia shati safi analeta, pesa ya vocha napewa, ilikuwa raha kweli.

Siku moja, majira ya saa kumi jioni akaniita kwenda kumkuna kama kawaida yetu, Mara nyingi anapokuwa na mm anavaa kanga peke yake bila hata chupi. Nimefika nikamkuta yuko kwenye kanga Kama kawaida yake akamtoa mtoto akacheze. Tumeingia chumbani tumeanza kushikana pale akashusha kanga akawa utupu, sasa Mimi roho yangu siku hiyo ikawa nzito sana, nikawa mzito kuvua nguo, nilivua kwa shigo upande. Wakati naigiza dudu washa ndani mlango wa nje ukafunguliwa alikuwa ameegesha tu. Huku ndani tulianza kuhaha, ila yeye akanitoa hofu kwamba kuna binti alimwambia aje hamsuke yawezekana ni yeye, akavaa nguo zake kaenda. Kufika sebuleni kumbe ni shemeji yake Kaka yake mkubwa na mume wake. Balaa kubwa hilo, kaanza kutetemeka, akaja chumbani akaniambia Leo tumekwisha maana atajua ndani kuna mume kwa sababu viatu nilikuwa nimeacha sebule ni. Huku ndani nilitafuta pa kutokea sikupaona, niliingia uvunguni Mwa kitanda nikatulie huko natetemeka kweli. Na shemeji yake ni mtu wa Tarime yaana kurya man panga njenje, Nikasema Leo nikitoka salama sirudii tena kutembea na mke wa mtu.

Sasa yeye akabaki sebuleni na shemeji yake, shemeji anamuuliza kwani viatu hivi vya nani? Ndani humu kuna nani? Maana mume wako yuko kazini sasa aliyomo humu ndani ni nani? Kadri ya maswali yalivyozidi mi natetemeka tu. Gafla wanabishana akaingia yule binti ambaye alimwambia aje hamsuke, Binti yule alikuwa ni mzuri sana na shemeji yake aliishawahi kumtongoza binti akakataa. Shemeji yake alipomuona yule binti akatilia kama barafu. Binti akaingia ndani wakakaa, sasa yule shemeji yake mke wa mdogo wake ndio akapata njia ya kusolve tatizo fasta, akamkonyeza yule binti aliyeingia ndani kwa sababu yule binti alikuwa anajua mi ndie nakula mzigo na alipoingia akakuta viatu vile akajua nimo ndani. Ikabidi sasa mke wa shemeji yake afunguke, akamwambia shemeji ni kweli humu ndani kuna mtu alikuwa anamsubiri huyu binti. Nilikuwa nakukatalia kwamba humu hakuna mtu kwa sababu ningekubari ungesema ni wangu tu. Kosa langu shemeji nikuruhusu hawa watu wakutane hapa, nisamehee shemeji yangu. kwa sababu jamaa alikuwa amemzimikia yule demu alipoteza network akasema hamna shida, lakn umefanya vibaya kumficha chumbani. Yule mke kanifuata ndani akasema mambo yako poa, nikatoka kwa kupotezea nikamkubatia yule binti, binti alijua hili ni gemu akusita kunikumbatia na yeye. Jamaa kuona hivyo akamwita shemeji yake nje akamwambia Mimi huyu binti nampenda sana, Sasa jamaa kamchukua unanisaidiaje? Mi taratibu nikatoka na yule binti nimemkumbatia lile jamaa likabaki likiachama mdomo tukatokomea. Toka siku.hiyo mke wa mtu marufuku.
 
hshahaha unajua katika maisha kuna story huwa zinakuja na ukihadithia watu wanaweza kusema hadithi lakini ni ukweli,
Hongera kupitia changamoto za ujana
Siku nikitulia ntakuleteeni yangu inatisha imekaa kama hadithi vile
 
hshahaha unajua katika maisha kuna story huwa zinakuja na ukihadithia watu wanaweza kusema hadithi lakini ni ukweli,
Hongera kupitia changamoto za ujana
Siku nikitulia ntakuleteeni yangu inatisha imekaa kama hadithi vile
Kweli mkuu haya mambo yapo tena sana, mi nimekoma sirudii tena.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom